- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Cape Verde: Midahalo Kuhusu Vijana na Siasa Inayoendelea Huko Ureno

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ulaya Magharibi, Cape Verde, Ureno, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhamiaji na Uhamaji, Vijana

Kuna kundi la raia wa Cape Verde ambalo huandaa mikutano mjini Lisbon ili kujadili uhusiano kati ya vijana na siasa, kama anavyoeleza Suzano Costa katika video [1] [pt] kama ilivyowekwa tena na Amilcar Tavares. Katika blogu yao – Tertúlia Crioula [2] [pt] – unaweza kusoma maelezo yaliyochukuliwa kutoka “Cape Verde katika Mdahalo” kadhalika unaweza kusoma majadiliano mengine kuhusu masuala muhimu.