- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ghana: Tangazo la Kibaguzi la Kombe la Dunia

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ulaya Magharibi, Ghana, Ujerumani, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi

Sokari anaandika kuhusu tangazo la biashara la Kombe la Dunia la kibaguzi lililotengenezwa na wakodishaji wa magari wa Kijerumani SIXT [1]: “Tangazo hilo hapo juu lilitumwa kwangu na rafiki kutoka Ujerumani ambaye alifafanua hivi: Linacheza kauli mbiu kadhaa zenye mtazamo wa kiUlaya, mtazamo unaodharau Uafrika kuhusiana na mchezo wa mpira unaokuja kati ya Ghana/Ujerumani.”