Msumbiji: Kasheshe la Misaada

Msumbiji inategemea fedha kutoka serikali nyingine ambazo zinatoa msaada moja kwa moja kwenye bajeti yake ya Taifa, kuwezesha huduma muhimu kama afya na elimu.

Uhusiano kati ya nchi ‘wafadhili’, na serikali ya Msumbiji, ambayo bado inaendelea kuwa chini ya mikono ya chama tawala chenye nguvu, umekuwa unayumba yumba kwa miaka kadhaa. Na nchi wafidhili zinatofautiana, kuanzia Ulaya, Marekani Kaskazini na Asia, na kwa nadra sana hutenda kwa kauli moja.

Tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, nchi wafadhili nyingi kila mara zimekuwa zikidai ushahidi wa kuboreshwa kwa “utawala” – katika kile ambacho kinahusiana na ufisadi, uboreshwaji katika uwajibikaji na utawala wa sheria. Madai haya yaliwekwa bayana katika mikataba kati ya nchi wafadhili na Msumbiji.

Mauaji ya watu wawili mashuhuri waliokuwa wakipeleleza ufisadi mwaka 2000 na 2001 yanaendelea kutotatuliwa katika macho ya nchi wafadhili. Kesi za hivi karibuni za mameneja wa viwanja vya ndege vya Msumbiji, kufujwa kwa mamilioni ya dola ya fedha za taifa vilikumbusha kuwa ufisadi unaendelea kutokea katika ngazi za juu.

Picha kutoka kwa mtumiaji wa Flickr Sida – Shirika la Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa la Sweden

Hata hivyo, ni sawa kusema kuwa, mpaka Sweden ilipoamua kwamba itapunguza msaada wake kwenye bajeti ya msumbiji mwaka jana, misuguano kati ya nchi wafadhili na na serikali inayopokea viliendelea kubaki ndani ya milango iliyofungwa. Na kwa nyongeza, uchaguzi wa rais wa mwaka jana pia ulipandisha misuguano hiyo hadharani, kwani wafadhili walihoji jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa.

Joseph Hanlon, mchambuzi wa muda mrefu wa masuala ya Msumbiji, mwanahabari na Profesa katika Chuo Kikuu cha Wazi, ametoa sehemu nzima katika tovuti yake kuorodhesha “mgomo wa wafadhili” wa 2010. Ameatoa muhtasari Unaoeleza kuwa wafadhili wa bajeti

(G19) walituma barua mbili kwa serikali mnamo Disemba 2009, wakidai hatua za haraka kurekebisha sheria za uchaguzi, rushwa, migongano ya kimaslahi, na kuingiliana kati ya chama cha Frelimo na serikali. Msaada wa bajeti ulisitishwa. Mnamo tarehe 5 Februari 2010 Aiuba Cuereneia, Waziri wa Mipango na Maendeleo na mjumbe wa serikali anayeshauriana na wafadhili, alituma [barua] majibu kwa G19, iliyoeleza msimamo wa serikali na kutoa masharti nafuu. […] Mapatano ya mwanzoni mwa mwezi Machi yalipelekea makubaliano yaliyotangazwa tarehe 24 Machi na kuanza tena kwa mtiririko wa fedha.

Edigio Vaz alianzisha mjadala katika ulimwengu wa blogu za Msumbiji mwezi Machi [pt] juu ya kuvunjika kwa mawasiliano hivi karibuni kati ya mataifa wafadhili na serikali yake

O maior problema do Governo, segundo os doadores, foi sempre o de ter aceitado as metas, indicadores de desempenho e objectivos negociados com os doadores no âmbito do PAP sem que contra eles apresentasse qualquer resultado tangível ou relatório de progresso circunstanciado, como acordado.

A demora, as manobras dilatórias, as desculpas, os relatórios generalistas e muitas vezes prolixos, contrastam com o avantajado estado quase capturado em que o Estado se encontra, pela gang cleprocrata incrustada aos vários níveis da gestão da coisa pública.

Tatizo kubwa la Serikali, kwa mujibu wa wafadhili, siku zote lilikuwa ni kukubali madhumuni, viashiria vya mafanikio na malengo, yaliyojadiliwa na wadhili kwenye PAP [Ubia wa Programu ya Misaada], bila kuonyesha mafanikio bayana au ripoti inayoonyesha mazingira dhidi yao, kama ilivyokubaliwa.

Uchelevu, kujivuta-vuta, visingizio, ripoti zenye maneno mengi, vipo [sambamba] na kutekwa kwa Taifa na genge la mafisadi lililojiweka katika ngazi mbalimbali za utawala wa umma.

Vaz anaielezea barua ya serikali ya kurasa 18 kwa wafadhili, kama “risasi iliyofyatuliwa angani”. Lakini pia anazishutumu nchi wafadhili [Pt]

… A megalomania do grupo dos PAP foi manifesta, ao ponto de lhes ter entorpecido a inteligência, necessária para o discernimento entre factos, necessários para servir de base para a tomada de decisão

…Ugonjwa wa akili wa kundi la PAP ulionekana, na kufikia kiwango cha kupumbaza ufahamu wao, uliohitajika ili kuuona ukweli uliohitajika ili kufanya maamuzi

Kwa mtazamo wake, wafadhili waliiadhibu serikali ‘mpya” ya Frelimo iliyoingia baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba, iliyomjumuisha Waziri Mkuu mpya, na kuizuia kuanza upya na programu zake mpya za jamii.

Lakini wasomaji walimjibu Vaz, na kumkumbusha kuwa nchi nyingi wafadhili zinasumbuliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi. Zenaida Machado anaandika [Pt]

Em alguns países europeus há e haverá cortes drásticos de orçamento 2010/11 e que de certeza, irão afectar o OGE/2011 de Moçambique.

Mesmo assim, acho que esta ‘crise’ europeia veio mesmo a calhar e serve de castigo/lição para as nossas ‘instituições’ politicas e governamentais

Katika baadhi ya nchi za ulaya kuna na kutaendelea kuwepo kwa upunguzwaji mkubwa wa bajeti katika mwaka 2010/11 na kwa hakika, hii itaathiri bajeti ya taifa ya msumbiji mwaka 2011.

Hata hivyo, ninafikiri kuwa muda wa haya ‘matatizo” unatoa adhabu/somo kwa serikali na taasisi zetu za siasa.

Baadhi walikuwa na mtazamo wa masihara juu ya mambo haya, kama vile mchora katuni wa ridhaa aliyeonyeshwa na Carlos Serra, ambaye alicichora serikali ya Msumbiji ikipata mshituko kwenye “mashine ya fedha ya wafadhili” [pt].

Uchelevu uliotokana na majadiliano juu ya misaada mwaka huu, kwa mujibu wa serikali ya Msumbiji, hayakuathiri utoaji huduma huku bajeti ya mwaka 2010 ilipokuwa inahitimishwa wakati wa “mgomo wa wafadhili”. Hata hivyo Vaz anahitimisha kwamba [pt]

De uma ou de outra forma, fica claro que as duas partes precisam de aprimorar os mecanismos de comunicação, diálogo político e acima de tudo, serem realistas nas decisões e compromissos que acordarem.

Kwa njia moja au nyingine, ni wazi kuwa wote wanatakiwa kunoa njia za za mawasiliano, majadiliano ya kisiasa, na zaidi ya yote, wawe wakweli katika maamuzi na ahadi wanazoweka.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.