- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Urusi: Habari za Mwanzo za Milipuko ya Mabomu

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Urusi, Habari za Hivi Punde, Siasa, Vita na Migogoro, Vyombo na Uandishi wa Habari, RuNet Echo

Utaratibu wa Jumatatu asubuhi mjini Moscow ulivunjwa leo na milipuko miwili ya mabomu ya kujiua [1] [EN], ambayo yaliua watu wapatao 38 na kujeruhi kwa uchache watu 70 (wengi wa walioathirika walikuwa ni wanafunzi wenye umri wa chini ya miaka 40). Milipuko hiyo ya mabomu ya kujiua ilifanywa na wanawake wawili wanaodaiwa kuwa na uhusiano na Waasi wa Caucasus Kaskazini [2] [EN]. Wanablogu walikuwa ni miongozni mwa watu wa kwanza kusambaza habari kuhusu tukio hilo baya, na hivyo kuwa chombo cha habari imara wakati tovuti nyingi za vyombo vikubwa vya habari viliposhindwa kutoa huduma kutokana na msululu mkubwa (wa watumiaji wa mtandao) na idhaa za televisheni zilikuwa taratibu mno katika kutayarisha maudhui katika wakati unaotakiwa. Kama vile mtumiaji wa Twita Krassnova alivyoona [3] [RUS], alama ya twita ya #metro29 [4] [RUS, EN] ilikuwa na jumbe 40 kwa sekunde wakati idhaa za televisheni ziliweza kuandaa habari 4 tu. Chini ya masaa mawili tovuti ya metro29.ru [5] iliundwa ili kupasha habari kuhusu tukio hilo.

Mmoja kati ya wanablogu wa kwanza kutangaza habari hii alikuwa Marina Litvinovich (ambaye pia ni mtumiaji wa LJ abstract2001), mwanablogu wa upinzani, ambaye alituma picha kutoka kituo cha treni cha Lubyanka [6] [RUS], palipotokea mlipuko wa kwanza:

Ukumbi wa stesheni ya  Lubyanka, picha na abstract2001

Ukumbi wa stesheni ya "Lubyanka", picha na abstract2001

Hapa pia kuna video ya YouTube inayoonyesha abiria wanavookolewa kutoka katika stesheni ya treni ya Park Kultury [7], palipotokea mlipuko wa pili, kama ilivyotumwa na mtumiaji baranovweb:

Kuanguka kwa muda mfupi kwa mawasiliano na usafiri kulifuata. Wakati Wakazi waliokuwa na hofu wa jiji la Moscow walipoanza kuangalia kama ndugu na marafiki wapo hai, mtandao wa simu za mikononi katikati ya jiji la Moscow ulikatika. Mtumiaji wa LJ offnet alilalamika [8] kwamba moja ya sababu za kukatika kwa mtandao wa simu za mkononi ilikuwa ni utaratibu wa kimangimeza ambo ulihitaji usimikaji wa kituo kingine cha ziada cha kurushia matangazo hata katika wakati wa wa hali mbaya zaidi. Mtumiaji wa Habrahabr, rubyrabbit alitengeneza orodha nzima [9] ya tovuti za habari zilizozimika.

Reli ya Sokolnicheskaya ilifungwa kabisa kwa ajili ya uchunguzi. Wanblogu walituma video za msongamano [10] katika kituo cha Komsomolskaya. Wakati huo huo watu walitahadhari kutumia huduma za usafiri wa treni, japokuwa njia nyingine za treni zilikuwa bado zinafanya kazi. Mwanablogu mashuhuri Nikolay Danilov (ambaye pia ni mtumiaji wa LJ anayejulikana kama nl) alituma picha za umati [11] wa [RUS] wasafiri wakitembea kwa miguu kuelekea kazini:

Wakazi wa Moscow wakielekea kazini, picha na Nikolay Danilov (nl)

Wakazi wa Moscow wakielekea kazini, picha na Nikolay Danilov (nl)

Idhaa za televisheni hazikuwa tu na kasi ndogo bali poia zimeshutumiwa kwa kukosa mtazamo unaofaa katika upashaji wao habari kuhusu tukio hili. Mwanablogu mwingine mashuhuri, Anton Nossik (ambaye pia ni mtumiaji wa LJ anayejulikana kama dolboeb), aliandika [12][RUS]:

в 12:00 по Первому каналу начался плановый выпуск новостей. Не спеша, рассказывают о взрывах метро в Токио (1995), Баку, Париже, Дюссельдорфе, Лондоне, о соболезнованиях Януковича, депутатов Верховной Рады, Ангелы Меркель, передают заявление Бернара Кушнера. Затем скороговоркой дали recap, довольно чёткий, всех основных событий в Москве, длиной в полторы минуты: 35 погибших, 70 раненых, метро не ходит от Комсомольской до Спортивной, в центре города пробки, правительство требует усилить безопасность всех российских аэропортов. На минуту включили Тимура Серазиева с Лубянской площади, и тут же пошла реклама здоровой пищи, пепси-колы, какого-то Антистакса, шоколада «Вдохновение», сока «Любимый»,синтетических моторных масел Mobil1, средства для мытья окон, нового йогурта «Яблоко Мюсли», Афобазола от тревоги и напряжения, кофе Jakobs Monarch, хлопьев от Nestle с цельными злаками. Каждый из роликов был длинней прямого включения с Лубянки. После завершения семиминутной рекламной паузы досрочно началось часовое ток-шоу «Участок».

Saa 6:00 za mchana, Channel One walianza taarifa yao ya kawaida ya habari. Bila haraka, walisimulia kuhusu milipuko ya mabomu kwenye treni huko Tokio (1995), Baku, Paris, Dusselsdorf, London, rambi rambi [za rais wa Ukraine Victor Yanukovich], kuhusu rambirambi zilizotumwa na [watunga sheria wa Ukraine], na Angela Markel, Bernard Kushner. Halafu, kwa haraka sana, wakatoa taarifa fupi ya matukio yote muhimu jijini Moscow, kwa dakika moja na nusu: 35 wafariki, 70 wajeruhiwa, hakuna usafiri wa treni kutokea Komsomolskaya mpaka Sportivnaya, kuna msongamano wa magari katikati ya jiji, serikali inataka kuongeza ulinzi katika viwanja vyote vya ndege. Kwa sekunde chache, walikuwa na [mwanahabari] Timur Seraziev akiripoti moja kwa moja kutokea viwanja vya Lubyanka, halafu wakaweka matangazo ya vyakula vya afya, Pepsi, Antistax Chokleti, maji ya matunda ya The Loved One, mafuta ya Mobil1, dawa za kusafisha madirisha, uji wa aina mpya ya mtindi wa matofaa, Afabazol – dawa ya ugonjwa wa wasiwasi pamoja na shinikizo, coffee Jacobs Monarch, wholegrain Nestle cornflakes. Kila tangazo la biashara lilikuwa refu kuliko matangazo ya moja kwa moja kutokea Lubyanka. Baada ya mwisho wa matangazo ya biashara ya dakika 7, wakaanza kipindi cha maongezi ambacho hakikuwa kwenye ratiba, “District.”

Wote, wanablogu na tovuti za habari walizaidia kujaza ombwe lililojitokeza. Tovuti ya habari ya lifenews.ru ilituma kusanyo la picha [13] [RUS] ambazo zilijumuisha picha za mabehewa ya treni yaliyolipuliwa [14] [RUS]. Mtumiaji wa LJ seg_o alituma picha [15] [RUS] kutokea katika eneo lililo Karibu na kituo cha treni cha Park Kultury. BBC na Guardian waliunda ukurasa wa blogu za moja kwa moja – LiveBlog [16] [EN] na Live Coverage [17] [EN] – ili kufuatilia kila tukio muhimu linalotokea. LiveJournal ilifungua mkondo maalum [18] [RUS] ili kutangaza jambo hili. Zifuatazo ni baadhi ya ripoti kutoka kwa wale walionusurika katika milipuko hiyo:

oyolin [19]:

Я работаю на Лубянке. В школе. Начинаю работать в 8. В 7.50 я приехала на Кузнецкий Мост. Хотела перейти на Лубянку, но там всё было в думу, людей не пускали. Вышла через Кузнецкий Мост. На Лубянской площаде сразу же всё перегородили, приехали спасатели. На работе до сих пор кризисная ситуация. Родители звонят, беспокоятся, мамы плачут. Это ужасно.

Ninafanya Kazi Lubyanka. Kwenye shule. Ninaanza kazi saa 2 asubuhi. Niliwasili Kuznetsky (stesheni ya treni) saa 1:50 asubuhi. Nilitaka nibadilishe nielekee Lubyanka, lakini kila kitu kilikuwa katika moshi pale, watu hawakuruhusiwa kuingia. Nikatoka Kuznetsky. Katika viwanja vya Lubyanka walizuia kila kitu, timu za waokoaji ziliwasili. Tunahali ngumu hapa kazini. Wazazi wanapiga simu, wakiwa na mashaka sana, akina mama wanalia. Hii ni hali mbaya.

kotikeksik [20]:

Время 14.40. Я только-только собрала в кучу голову. Меня перестало трясти, когда я встаю со стула, и я больше не плачу. Пытаюсь заставить себя поработать.

Ni saa 8:40 mchana. Nimeweza kujikusanya. Sitetemeki tena ninaposimama kutoka kwenye kiti, silii tena. Ninajaribu kufanya kazi.

davete [21]:

Выхожу на Парке Культуры. Поднимаюсь уже было к выходу. Рядом идут сотрудники милиции. К ним обращается какая-то женщина:
-Что случилось то?
-Ой, да авария какая-то, технические причины.
В эту же секунду прогремел взрыв.
Противоположный от моего поезд, по направлению к станции Кропоткинская.
Взорвался где-то в середине.
Людей было не много, давки не было. Но взрыв очень мощный. Не сомневаюсь, эта бомба – военного стандарта.

Nilikuwa ninaelekea Park Kultury (stesheni ya treni). Nilikuwa nikitaka kutoka nje ya stesheni. Maofisa wa polisi wanatembea pembeni yangu. Mwanamke mmoja anawauliza:
– pametokea nini
– Aam, ajali, masuala ya kiufundi
Wakati huo huo mlipuko ukanguruma. Ndani ya treni inayoelekea upande mwingine, kuelekea stesheni ya Kropotkinskaya. Ulilipuka sehemu fulani katikati. Hapakuwa na watu wengi sana, hakuna kukanyagana. Lakini mlipuko huo ulikuwa mkubwa. Bila ya shaka, bomu hili lilikuwa ni la kijeshi.