Wanablogu wa Tunisia walizoea kuepuka kutumia Kiingereza (lugha ya tatu nchini mwao), na badala yake waliandika kwa Kiarabu (na wakati mwingine kwa lahaja za Tunisia) au Kifaransa. Hii, kwa namna fulani, imezuia hadhira ya nje na kukinza ufikiwaji wa mawazo na maoni na hadhira isiyozungumza Kiarabu au Kifaransa. Lakini hivi karibuni baadhi ya wanablogu wanatumia Kiingereza katika makala zao. Hapa kuna pitio la baadhi ya blogu za Kiingereza.
Katika makala yenye kichwa: Kutopatikana kwa AlJazeera.net nchini Tunisia, Amin Zayani ameeleza wazi utata wa kuzuiwa kwa AlJazeera.net: Watunisia wanaweza kutazama Al Jazeera bure kabisa ilihali tovuti yake ikichungwa. Anaandika:
Ukiwasha luninga yako na kipokea satelaiti nchini Tunisia unaweza kutazama Aljazeera, Aljazeera idhaa ya Kiingereza, Aljazeera kwa Watoto, Aljazeera idhaa ya filamu za Kuelimisha, Aljazeera Live, Aljazeera Michezo siku nzima.
Lakini ukiandika anwani ya tovuti yake kwenye mtandao huwezi kuipata. Ajabu, Au sio?
Ikiwa na kichwa: Tilikum The Killer Whale (Tilikum nyangumi muuaji), Foetus.me Anaandika kwa hadithi fupi inayohusu Uhuru:
Wakumbushe we ni nani. Wakumbushe ulivyo huru na silika ya mwituni. Hao watu wamekusahau mwindaji mkuu wa baharini. Usiwaachie, waliota ndoto za kutawala, wawaza utawala dhalimu kama walivyo wao, wakiuhusisha na chakula na ukatili. Waambie utawala wa kweli ni kuheshimu uhuru wa watu wengine na ujenge katika hilo. Waonyeshe kuwa wana wajibu. Uasilia utadumu rafiki yangu.
Amor akiblog katika ulimwengu wake aliandika kuhusuiana na kanuni mpya za China kwa vyombo vya habari vinayotangaza kuhusu mgogoro wake na Google:
Kanuni mpya na maagizo kutoka kwa serikali ya China yenyewe zinazozuia vyombo vya habari vya China kutokutangaza kitu chochote kuhusiana na tukio la hivi karibuni la Google kujiondoa nchin China.
Maagizo hayo, yaliyodakwa na China Digital Times, yanaorodhesha mfululizo wa amri ambazo zinaghasi kiasi kwa vyombo vya habari vinavyotangaza habari za Google. Wakati hili si jipya hata kidogo, serikali ya China inaendelea kutenda kwa mabavu na mamlaka yake kandamizi.
Sam’ s World anatupa mtazamo wake wa Kongamano la Kwanza la Kimtandao la Kiarabu, lilofanyika Beirut hivi karibuni. Anasema:
Kwa mara ya kwa kwanza, Wanamtandao wa Kiarabu wamefanya kongamano lililowajumuisha viongozi kutoka eneo lote la Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini, Ulaya na Bonde la Silicon ili kujadili maendeleo ya teknolojia ya mtandao na fursa zinazoambatana nayo.
Namna gani unaweza kuanzisha biashara ya kwenye mtandao au kumudu/ kuitangaza biashara yako ya kwenye mtandao? Kutangaza mtandaoni, uanahabari wa kijamii, ujasiriamali, kuanzisha biashara, fursa zinazoibuka … Haya na mengine yalijadiliwa katika tukio la siku mbili la Arabnet 2010 (Machi 25 &26)
Sula7fet, Mwanafunzi wa lugha ya Kiingereza na mgeni katika uwanja wa wanablogu wa Tunisia anatushirikisha kitabu anachokisoma kwa nukuu:
The Paranoid Style in American Politics na Richard Hoftasadter , niliposoma jina la kitabu nilifikiri kuwa mambo yaliyoandikwa yamelenga hasa wasomaji wa Marekani, nakumbuka kuwa ilinichukua muda kidogo, Nilisita kidogo, na ndipo nikauliza bei gani?
Natumai, huu mwelekeo mpya wa matumizi ya lugha kuelekea kutumia lugha ya Kiingerza, utawapa wanablogu wa Tunisia pumzi mpya na kuwatambulisha kwa wasomaji wapya ulimwenguni kote.