- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

South Africa: Mauaji ya kiongozi wa Afrikaner Resistance Movement

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Kusini, Siasa, Ubaguzi wa Rangi

Usiku wa Tarehe 3, Aprili 2010, kiongozi wa kundi la watetezi wa waafrika kusini wenye asili ya udachi (Afrikaans Weerstandsbeweging (AWB), an Afrikaner resistance movement), Eugene Terre'Blanche, aliuawa [1] . Hii imetokea wakati kukiwa na mjadala mkubwa unaohusiana na ubaguzi wa rangi kufuatia wimbo wa ‘kill the boer’ (uwa mkaburu), wimbo wa zamani wa kupinga ubaguzi wa rangi wa rangi ulioimbwa na kiongozi wa vijana wa ANC, Julius Malema [2].

Hebu na tuone jinsi raia wa Afrika ya kusini wanavyosema mtandaoni kuhusu kifo cha kiongozi huyo na mustakabali wa baadae kuhusiana na rangi ya ngozi nchini humo.

From the Old amefuatilia vizuri mpango huo wa aibu wa mauaji na hapa ni yale aliyoyatuma kwa Chama cha Skauti cha Afrika ya Kusini:
“Maelezo ya Verkenners Beweging van Suid-Afrika kuhusu mauaji ya Eugene Terreblanche” [3]

TAFADHALI TAMBUA KUWA TAFSIRI YA KWANZA KUTOKA LUGHA YA KIAFRIKAANS KWENDA KIINGEREZA ILIKUWA YA JUU JUU, TOLEO RASMI LITAWEKWA BAADA YA DAKIKA CHACHE.

Chama cha Maskauti wa Afrika Kusini wamepokea kwa uchungu mauaji ya kikatili ya mzee wetu Eugene Terre'Blanche. Mr. Terre'Blanche aliyatoa maisha yake kuwatumikia watu wake ambao aliwapenda sana.Ni huzuni kuwa maisha yake yamepotea, kwa utumishi wake.

Ni muhimu kutambua kuwa mauaji yametokea wiki chache tu baada ya Mal-emma kwa mara ya kwanza ilipoimba “shoot the farmer” (uwa wakulima). Hii imetokea siku mbili tu baada ya kutolewa amri ya mahakama ikimpinga Malema na ni haki pia kuuliza iwapo hii amri ya mahakama ilihamasisha mauaji ya mjomba wetu Eugene. Iwapo kuna uhusiano baina ya kifo cha mkomunisti Hani Paassaterdag cha mwaka 1993 na mauaji ya Mjomba Eugene Paassaterdag mwaka 2010 (hiyo sababu) haijalishi kwa Chama cha Maskauti. Ukweli ni kwamba, mkulima mzee asiye na kinga akiwa kitandani kwake kwa namna ya kikatili kabisa kwa fimbo na panga alipigwa hadi kifo na utawala wa leo, mazingira yaliyoandaliwa kwa ajili ya mauaji haya yametekelezwa makusudi ili kuwaangamiza ndugu zetu.

Uhusiano baina ya matamko ya kichokozi [2] ya Julius Malema na mauaji ya Eugnene Terre'blanche ni majadala wa kudumu hasa ukiangalia makala husika katika Blogu. DBS kwenye MyDigitalLife analiita tukio hili kama fursa kubwa [4]:

Mauaji ya Eugene Terreblanche ni fursa kubwa kwa Waafrika Kusini.

Huu ni wakati mzuri wa kuanza upya na kuuonyesha ulimwengu kuwa tuna uwezo wa kuwa watu wenye akili timamu, wenye kufikiri kabla kufungua midomo na kuongea sisi kwa sisi kabla ya kufanya kitu chochote chenye madhara kwa binaadamu.

Chuki iliyochochewa na viongozi mbalimbali miezi iliyopita si nzuri kwa taifa. Hebu na tutumie kifo hiki cha mtu wetu kama wakati wa kubadili mwelekeo ili kujipatanisha na mitazamo tofauti ya watu wa nchi yetu badala la kuishia kumtupia lawama mtu aliyeimba wimbo.

Je tunaweza kufanya hivyo? Ndio tunaweza! Je tutafanya? Sawa lakini kwa bahati mbaya nadhani hatutafanya.

Ni dhahiri kuwa kuna jambo la kugombana na AWB. KickMugabeOut anatumai kuwa aliyekuwa kiongozi wa AWB anapata mateso ya milele [5]. Anaandika habari zikiambatana na picha za kuvutia pamoja na maoni. Picha moja inamuonyesha jamaa akiwa kavalia fulana na bendera ya zamani ya kibaguzi huku akiwa na bendera ya Israeli kwenye ugo.

Rais wa Afrika ya kusini, Jacob Zuma, ametoa tamko juu mauaji ya Eugene Terre'Blanche. Imeandikwa hapa na blogu ya Live Times [6]. Na habari nyingine kuhusu tamko la Jacob Zuma zimeandikwa na From The Old [7]:

Leo Jacob Zuma atazungumza na Afrika Kusini saa 8 mchana.

Anategemewa kuwaambia Waafrika Kusini kusahau tukio hilo na kwamba tuendelea mbele, hata hivyo wengi wanasema hilo haliwezekani kwani makaburu wako chini ya mashambulizi.

Pia, Jacob Zuma amesema leo kuwa “Waafrika kusini wasiruhusu wachochezi kutumia tukio hili na kuchochea au kutia mafuta chuki za misingi ya rangi”.

Lakini ni kama amesahau kuwa wiki chache zilizopita watu weupe wa Afrika Kusini wamekuwa wakishambuliwa na Julius Malema na hilo halionyeshi kuwa linaweza kukomesha chuki za misingi ya rangi na kuwashutumu watu weupe.

From The Old pia anaandika juu ya kauli nyingine [8], hii ya sasa ni ya AWB, na kudai kuwa mauaji yalikuwa ya kisiasa:

AWB ilijitokeza katika mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa mauaji kwa hakika yalikuwa ni ya kisiasa na kwamba watamlipizia Julius Malema ambaye wanaamini kuwa ndio sababu ya mauaji.

Julius Malema wiki chache zilizopita alichochea chuki dhidi ya watu weupe wa Afrika ya Kusini na Makaburu kwa kuimba wimbo unaoitwa “uwa kaburu.”

Wakati hali ya wasiwasi ikikua Afrika Kusini kombe la dunia nalo liko njiani kuelekea huku. Ndani ya chini ya miezi miwili ijayo Afrika kusini itakuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya kimichezo kuliko yote ambayo Afrika imewahi kuandaa wakati hali ya kibaguzi ikiendelea kukua.

Ikiendelea katika mistari hiyo hiyo, Common Dialogue inahoji, “Je damu Terre Blanchie ipo mikononi mwa Malema? [9]”:

Eugene Terre Blanche amekufa kifo kibaya na inadaiwa kuwa aliuawa na mikono ya vibarua wa shambani kwake. Je haya ni matokeo ya Malema kuimba “uwa kaburu”?

Inadaiwa kuwaTerre Blanche alikatwa katwa na kubondwa hadi kufa katika shamba lake karibu na Ventersdorp, katika jimbo la Kaskazini Magharibi, bila shaka na wafanyakazi wake kutokana na mabishano juu ya randi 600.
Hisia zinazaidi kukua na baadhi ya wale wenye mrengo wa kulia wakiahidi hata kulipiza kisasi. Swali ni kwamba “miujiza” ya mpito wa Afrika Kusini kutoka sera za kibaguzi Kufikia demokrasia ilikuwaje?
Na ni kwa hatari kiasi gani matamko yenye hisia za ubaguzi wa rangi yanayotolewa na watu kama Malema na wanasiasa wengine ambao wanaopenda siasa za kibaguzi?

From The Old, ameandika maelezo mengi juu ya kesi hii kwenye blogu yake, amelizungumzia tena hili katika mtazamo wa AWB [10] anakubaliana na mtazamo ulioonyeshwa kwenye Facebook:

“AWB ipo pamoja na familia ya Eugene Terreblanche na inataka kusisitiza kuwa tukio hilo lilichochewa na Malema na lilikuwa la kisiasa kama ilivyowekwa dhahiri katika Facebook”

Wakulima Weupe pote Afrika Kusini bado wapo chini ya mashambulizi, sasa mmoja wa makaburu anayefahamika sana ameuawa katika shamba lake mwenyewe kutokana na ugomvi wa malipo ya mshahara kama inavyodaiwa. Wengi wanapata shida kuamini ugomvi wa kawaida wa malipo unaweza kuwa sabau ya kifo cha Eugene Terreblanche kiongozi na mwanzilishi wa AWB.

Eugene Terreblanche inasemekana kuwa huwa halali kabisa shambani kwake na ukweli kuwa amegundulika kuwa alikuwa “amelala” pia unatia shaka ya juu ya nini hasa kilichotokea.

Kama hili tukio ni la kisiasa au la ni hadithi nyingine, mkulima mzungu aliyeajiri watu weusi ameuawa . Kitu cha kwanza kinachoingia akilini ni wimbo ambao ANC inafanya juu chini usipigwe marufuku. Wimbo huo huo ambao Julius Malema alizuiwa kuuimba na bado anaendelea kuuimba nchini Zimbabwe bila kujali amri ya mahakama.

Tony Lankester anatoa maoni yake katika “Je malema atafanya nini? [11]”:

Kwa hiyo Eugene Terreblanche ameuawa. Japo inaweza kuwa haina uhusiano, ukweli kwamba imetokea wakati nchi ikihangaika na mdahalo wa uhalali wa wimbo wa “uwa kaburu” utauweka mdahalo huo katiaka hali ngumu zaidi. Huu ni mfano halisi wa maisha wa kile ambacho wapinzani wa mashairi ya wimbo walichokuwa wakisema, na wanaomchukia Malema wataridhika katika G&T zao. Na wakati ni vigumu kuwezekana kuwa uimbaji usio na msingi wa wimbo huo ungeweza kumhamasisha mtu yeyote kumpiga risasi Mr Terreblanche usingizini, kila mmoja anatamani kujua Malema atachukua hatua gani? Je atashuka chini na kuacha kuimba? Je atayashutumu hadharani mauaji hayo na kusema kuwa hicho sicho alichomaanisha? Au atabaki na msimamo wake alioushikilia na kuuimba wimbo huo kila apatapo fursa?

FliMflaMfLiK anasema kuwa badala ya kushadidia wimbo wa “uwa kaburu” na badala yake tutilie mkazo katika ukweli huu: “Terreblanche = Dunia Nyeupe [12]”:

Kila mtu amekazania “wimbo” lakini hakuna anayeangalia “ukweli”. (Kufunga funga nguo za ndani) Kufanya mambo yawe magumu ndio kile ambacho watu wanaweza kukifanya vizuri zaidi, lakini kile wanachotakiwa kufanya ni kukaa chini na kuiangalia mantiki:
1. Walikuwa na umri wa miaka 16 na 21 kila mmoja – vijana sana.
2. Hawakukimbia, waliwasubiri polisi.
3. Walikasirishwa na kitendo cha kutokulipwa mshahara wao wa mwezi wa R300.00 kila mmoja (inatisha).
4. Inasemekana kuwa Eugine aliwatenda vibaya sana siku za nyuma (hili ninaweza kuamini). Alishawahi kuwatishia kuwauwa hapo kabla.
5. Kwa hayo hapo juu, je hawa vijana hawa wangliweza kufikiri (katika akili zao) kuwa walifanya hivyo ili kujikinga wenyewe?

Kwa sababu tu Eugine alikuwa anafahamika , hili limekuwa suala kubwa?

Hawa vijana wanaweza kuwa hawakujua uwepo wa wimbo wowote kwa upande wao. Hatujui.

Labda ni busara kukaa na kusubiri Ukweli mwingine utakavyojitokeza wenyewe?

Na mwisho, katika mpindisho wa kejeli, Azad Essa anatumia tukio la Terreblanche kubainisha mambo na imani maarufu juu ya watu katika Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Kusini katika makala yake kwenye safu za Thought Leader “Kiongozi wa Fikra” “Je gaidi'Blanche alikuwa Muislamu? [13]

Kwa ujumla wake ni kwamba, Mmoja kati ya viongozi wa watetezi wa Wazungu wa Afrika Kusini ameuawa kikatili.