Poland: Utata Kuhusu Sehemu Atakayozikwa Rais wa Poland

Tangazo la leo kuwa rais wa Poland na mke wake, waliofariki katika ajali mbaya ya ndege huko Smolensk Jumamosi iliyopita, watazikwa siku ya Jumapili saa 8 mchana katika Kasri la Wawel huko Krakow limezua utata mkubwa.

Familia ya Lech Kaczyński ilipewa machaguo matatu ya sehemu za kuzika: Kasri la Wawel mjini Krakow, vile vile Kanisa la Mt. Yohana na Makaburi ya Kijeshi ya Powazki mjini Warsaw. Stanisław Dziwisz, Askofu Kadinali wa Krakow, alitangaza [PL] leo kuwa wameamua na kuichagua Wawel, baadaye tangazo hilo lilichochea mfululizo wa upinzani wa umma.

Kadri ya waandamanaji 400 walikusanyika [PL] mbele ya Jengo la Kanisa Kuu (Jengo la jiji) la Krakow ili kueleza kero yao: uongozi kushindwa kujadiliana na taifa; ukweli kwamba Wawel ni makaburi ya wafalme, viongozi wa kijeshi, wawakilishi wa fasihi ya kiPoland na watu wengine mashuhuri katika historia ambao wanachukuliwa kama mashujaa wa taifa; ukweli ni kwamba hakuna hata mke mmoja wa mashujaa hao aliyezikwa hapo pamoja nao. Upinzani huo uliandaliwa na vikundi vya Facebook, kama vile hiki hapa (mpaka sasa kina mashabiki 2,143), hiki (mashabiki 23,369) na hiki (wanachama 11,782). Karibu watu 1,400 wamesaini katika waraka huu wa mtandaoni [PL] ambao kadhalika unahusiana na upinzani huo. Ukubwa wa upinzani huo kwenye Facebook haukupita bila kutupiwa macho na vyombo vikuu vya habari [PL].

Ili kuelewa hisia za waandamanaji, hebu tuangalie baadhi ya mitundiko yao kwenye Facebook. Maciej Sadkowski anaelezea maoni yanayotawala katika moja ya vikundi vinavyopinga uamuzi huo [PL]:

Ni HAPANAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!

Gabi Wielesik anasema [PL]:

Sio tu kwamba kwa ghafla mtu ambaye kila mmoja alimcheka anageuka kuwa shujaa wa taifa, na sasa… shuku … pengine tuwazike [Gosiewski], [Szmajdziński] na wengine huko Wawel, pia? Nao pia walifariki [katika ajali hiyo ya ndege]…

Paula Rettinger anaamini [PL] kwamba sehemu ya kuzikwa rais ni Warsaw:

Ninapinga kuzikwa kwa [Lech Kaczyński] huko Wawel. Kaka yake babu yangu alifariki Katyn. Kadhalika mjomba wake mama yangu. Mada hii ipo karibu na moyo wangu. Sababu pekee ya kumuita Kaczyński shujaa ni kifo chake katika ajali. Ni kutowajibika, na uamuzi wa kijinga uliochukuliwa chini ya shinikizo la mtiririko wa propaganda za salamu za rambirambi kwa wanandoa hao waliofariki. Kanisa kuu la Warsaw ndio mahali wanapozikwa marais, na ndipo hapo ambapo rais apumzishwe.

Izabela Wójcik anakumbusha [PL] jinsi Poland inavyoonekana nchi za nje:

Na mimi pia ninapinga (uamuzi huo), kadhalika marafiki zangu nilioongea nao. Lakini hili si suala la ndani kwa sababu sasa dunia nzima itaona ni jinsi gani baada ya kipindi kifupi cha umoja taifa la waPoland linatengana na kubishana tena. Jaribu kuangalia taswira hii: gwaride la heshima lenye wageni kutoka duniani kote na maandamano ya upinzani nyuma yake. Itaonekana vipi duniani? Kwa nini tuzidishe migogoro kwa maamuzi ya namna hii? Eh…

Piotr Tomula anaonyesha [PL] hisia za zamani za familia ya Kaczyński kuhusu Krakow:

Hakupokea uraia wa heshima wa Krakow, na sasa hivi kaka yake anamsukuma kwa kupitia mlango wa nyuma ili apate zaidi, na hivi ndivyo bata hawa [jina la mitaani la makaka hawa wa familia ya Kaczyński, limetokana na neno ‘kaczka’ – ‘bata’], HAKUNA HESHIMA, ni UBATILI tu…

Kuba Bielecki anaongea [PL] kwa kejeli:

Kama familia yangu itaamuani wapi nitakapozikwa, nitamwambia kaka yangu kuwa nataka mahali hapo pawe Wawel, lakini mkono kwa mkono na Sobieski, na hata Mickiewicz panaweza kuniridhisha pia.

Agata Kol ni moja ya sauti chache [PL] zinazounga mkono uamuzi huo:

Kaczyński alikuwa mkuu wa taifa, kama vile walivyokuwa wafalme kutoka katika familia za Piast au Jagello. Kadhalika alichaguliwa kidemokrasia.

Gazeta.pl imeweka tafiti [PL] juu ya mada hiyo, ikiutaka umma kutoa maoni yao. Haya ndio matokeo ya sasa (mpaka ilipofika saa 5 usiku):

Je Unafikiria nini kuhusu mipango ya kumzika Kaczyński huko Wawel?

63% Azikwe Warsaw

26% Vizuri sana, hii ndiyo sehemu yake hasa

11% haina shaka, familia yake ndio iamue


Ujumbe wa twita
wa Piotr Kowalczyk [PL] anatoa muhtasari wa muelekeo wa mjadala huu:

Wawel haitawaunganisha watu wa Poland, bali itawatenganisha.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.