Irani: Je Blogu Zimepoteza Umaarufu Tangu Uchaguzi

Wanablog wa Irani kumi na moja na wandishi wa habari wanaowakilisha sehemu tofauti za misimamo ya kisiasa wamejibu dodoso kuhusu mabadiliko uanahabari wa kiraia nchini Irani tangu Uchaguzi.

Kabla ya uchaguzi wa rais wa Juni 2009 misingi ya mabadiliko ya vyombo vya habari vya kiraia nchini Iran ilikuwa ni YouTube na blogu. Uchaguzi na mtafaruku uliofuataia ulizitambulisha Facebook na Twita kama njia nyingine mpya za raia kujieleza mtandaoni. Kwa muda mfupi wakati wa uchaguzi, Serikali ya Irani ilizuia upatikanaji wa Facebook, YouTube, Twita na tovuti nyingine kadhaa. Baadhi, akiwemo mwanablogu anayeongoza wa mlengo wa Kiislam [fa], iliita hali hii kama mkakati ambao haukupimwa vizuri ambao ulisaidia wapinzani nchini Iran kutawala eneo yakini. Licha ya majaribio ya utawala kuchuja tovuti za kijamii, ziliendelea kuwa njia yenye nguvu ya mawasiliano ya Harakati za Kijani.

Je Uchaguzi warais nchini Irani ulibadilisha matumizi ya zana za uanahabari wa kiraia na njia zake? Je Facebook na Twita ndio wadau wakubwa? Je blogu zinazidi kwa taratibu kuwa njia ya pili ya kushirikiana mawazo? Je ni vyombo vipi vinavyotumika zaidi na wanaharakati wa kisiasa?

Niliwataka mwanablogu mmoja anayeongoza wa mlengo wa Kiislam; wanablogu watatu wa mlengo wa kijani; mwanablogu mmoja wa mazingira; wanahabari watano; mwanablogu hai mmoja kushiriki katika kupitia maswali ya kuchagua. Kundi la raia wa matandaoni kumi na mmoja wasingeweza kuwakilisha ulimwengu mzima wa blogu wa Irani, lakini ni hatua ndogo kelekea kuelewa jambo zima.

1-Je ni tovuti zipi ulizozitembelea zaidi tangu uchaguzi?

Facebook ndiyo ilipendwa sana na kupata pointi sita, Twita ipo chini na ina pointi moja. Blogu zilipata pointi mbili na FriendFeed na YouTube tatu kila moja.

2-Je, kwa mtazamo wako ni tovuti zipi ambazo wanasiasa na wanaharakati wakijamii huzitumia zaidi?

Blog zinaendelea kuwa mfalme kwa kuwa na alama sita, Facebook alama tatu, you Tube alama mbili, FriendFeed alama moja, Twita ilipata sifuri, na hakuna ilipata alama moja.

Sita kati ya raia wetu wa mtandaoni wanaamini kuwa umuhimu wa blogu haukupungua baada ya Uchaguzi, wawili wanafikiri kuwa blogu zilidi kuwa na umuhimu, na watatu wanaamini kuwa umuhimu wake ulipungua.

Katika kundi lililofuata, wawili wanafikiri kwamba blogu zimepungua umaarufu kutokana na kukua kwa umaarufu wa Facebook, na mmoja anadhani kuwa Wanablogu wamepunguza kujishulisha.

3-ni tovuti zipi unazozipendelea kufanyia miadala yako muhimu?:

Blog zimetajwa mara 4, Facebook, mara 6, FriendFeed mara 3 na Twitter mara moja.

Kwa ujumla , ukisoma haya mapitio inaonesha kuwa baada ya Uchaguzi wa rais, raia wa mtandaoni nchini Iran wamekuwa zaidi na kwamba Facebook imekuwa uwanja wa wengi wao wakiwemo viongozi wa kisiasa. Utafiti pia unaonesha kuwa kile kiitwacho ‘mapinduzi ya twita’ ( angalau washiriki wote 11) labda ilikuwa na upashanaji habari wa kimagharibi zaidi na usingeleta athari halisi nchini Iran. Blog zinaendelea kuwa ni sehemu muhimu lakini zinapoteza eneo kwa washiriki wapya. Pengine Jambo moja ni hakika kuwa baada ya Uchaguzi wa rais Nchini Iran mambo hayako vile yalivyokuwa kwenye jumuiya ya waIrani, kwa mtazamo na uhalisia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.