Guatemala: Hadithi ya Maziwa Mawili, Macaws na Malkia

Hifadhi ya Taifa ya Laguna del Tigre – hifadhi muhimu ya nchi nyevu na nchi misitu ya kavu ya kitropiki – kwa sasa inatishiwa sana na uvamizi wa binadamu, mlipuko ya moto isiyoweza kudhibitiwa, na uchimbaji wa mafuta. Wakati mkataba wa miaka 25 umekwisha, kampuni ya Perenco Guatemala LTD inaomba tena mkataba huo, lakini wanamazingira na wanaharakati wanapinga vikali, wakiandaa kampeni hizo kwenye Facebook [es] na tovuti nyingine. Kwa niaba ya Guatemala, Kamati ya Kimataifa ya Wanasheria (ICJ) kwa ajili ya Guatemala ikiwa na wawakilishi kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria za Mazingira na Jamii [es](CALAS kifupisho chake kwa Kihispania), wamewasilisha maoni yao juu ya mazingira mbele ya Sekretarieti ya Mambo ya Mazingira wakieleza kuwa nchi inashindwa kutekeleza mpango wa kulinda maeneo na haiheshimu sheria kwa kurefusha mkataba wa uchimbaji mafuta 2-85 huko Hifadhi ya Haifa ya Laguna del Tigre kwenye hifadhi ya viumbe hai ya Maya.

Picha na MikeMurga kwa kibali cha CC.

Kwa maneno mengine, wengi wanaguswa na uharibifu huo wa makazi ya viumbe hai wengi, kama ilivyoelezwa na blogu ya Guatemalan Birdwatching :

Guatemala ina maeneo19 ya uoto asilia, 300 yenye hali ya hewa tofauti, zaidi ya maeneo ya volkeno 37, mito, maziwa na fukwe ambavyo vinaungana na utofauti wetu wa makabila na kuifanya nchi hii kuwa ya ajabu na ya kupendeza. Uwepo wa viumbe hai wengi tofauti umeiwezesha Guatemala kusimama kati ya nchi 25 zenye aina nyingi zaidi za hifadhi asilia duniani. Mamilioni ya aina mabalimbali ya viumbe wakiishi katika mazingira mbalimbali, zaidi ya aina 700 za ndege, mamalia kama Jaguar, tapir na aina nyingi za reptilia na wadudu.

Savia, shule ya kufunza kuheshimu na kuilinda sayari hii imetengeneza video, ambayo inatoa hadithi ya Laguna del Tigre na kueleza kwanini ni muhimu kulilinda eneo hilo (yenye vidokevya vya maandishi ya kiingereza).


Wito wa Laguna del Tigre

Kampeni na msukumo kutoka kwa wanamazingira vimekuwa na mafanikio – viliweza kuchelewesha maamuzi ya Rais Colom. Bado haijajulikana iwapo ataamua kurefusha mkataba wa kampuni ya kuchimba mafuta, kitu ambacho kitakuwa kinyume cha matakwa ya baraza lake la mawaziri, hasa kwa waziri wa mazingira Luis Ferraté, ambaye anapinga kabisa urefushwaji wa mkataba huo.

Hifadhi hii hulichukuliwa kama eneo la pekee la ndege wa aina ya macaw wekundu na waangalia ndege (wapenzi wa ndege) na ndiyo maana blogu ya shule ya kufundisha utunzaji ndege Guatemala inaeleza mashaka yake. Ina kadiriwa kuwa kuna jamii 300 tu za macaw wekundu waliobaki katika mazingira ya kibaiolojia ya Maya.

Dayamn anatushirikisha simulizi ya huzuni ya Poc Duck, ambao wamepotea sasa:

Inawezekana kuwa hili ni jina ambalo watu wengi hawajalisikia na hawataweza kilisikia. Hii aina nzuri ya bata ilitoweka muda mrefu kabla wengi wetu hatujazaliwa. Bata hao waliishi kwenye bwawa kubwa zaidi ya yote nchini. Mwaka 1966, mwanaikologia Anne LaBastille alianzisha kampeni ya kuokoa bata hao wasitoweke lakini juhudi zake zilipotea bure. Hifadhi alioianzisha haikuwa na uwezo wa kukabiliana na uharibifu tulioufanya katika mazingira na mwishowe mwaka 2004 baada ya uchunguzi uliofanywa na UICN kwa udhamini wa Shirika la Kimataifa la BirdLife, ndege hao walitangzwa rasmi kuwa wametoweka.

Na ziwa la Atitlan, mahali ambapo Poc duck walitoweka hadithi ni tofauti . Alan Mills anasema ziwa halikuharibiwa usiku mmoja, bali ni matokeo ya maendeleo ya hovyo ya utalii yaliyofanyika hapo, na chupa nyingi tupu za bia na uchafu ulioachwa na tafrija za usiku, ambazo hazikubadilisha umasikini uliotopea wa wanavijiji waliozunguka, na wala haukuongeza utalii mzuri kwa mazingira. Kwa Mtandao wa Mshikamano wa Guatemala, ziwa hilo linalia pia:

Mwandishi, Aldous Huxley, aliandika kwa umaarufu juu ya Ziwa Atitlán, ”ziwa Como, kwangu mimi naliona kama, linagusa upeo unaoruhusiwa katika uzuri wa mandhari, lakini Atitlán ni Como (eneo zuri la milima na maziwa asili yaliyotokana na volkeno) yenye vikorombwezo kadhaa vya volkeno. Hii sasa ni zaidi ya kitu kizuri. ”Japo sijawahi kufika kwenye ziwa Como lakini nimefika ziwa Atitlán na ni zuri na la kuvutia mno. Hata hivyo, kuna hofu kuwa ziwa hilo linakufa na litageuka kuwa ziwa la tope kwa sababu ya shughuli za kibinadamu. Shughuli hizo zinajumuisha, kwa mfano, kilimo, utalii, na kukosekana huduma za kijamii kudhibiti taka.

Wakati yapo maoni yanayosema kuwa hakuna kilichobaki kwenye Hifadhi ya Taifa ya Laguna del Tigre, wanaikiologia wanaofanya kazi katika eneo hilo na jamii za hapo waliweka wazi kuwa kuna paa za misitu ambayo bado zipo salama katika eneo lisilokaliwa.

Gavana wa Petén anajutia [es] kuwa hakuchukua hatua mapema ili kulinda pori letu. Hata hivyo, si katika kuhifadhi mazingira tu. Moja ya vitu vya thamani vya Laguna del Tigre's ni mji wa zamani wenye umri wa miaka 2,500 wa Maya ulioitwa Waka´(miaka 500 kabla ya Kristo) au El Peru. Unahifadhi pamoja na vitu vingine vya tahamana kaburi la Malkia wa Maya

¿Que te pasa Guatemala? [es] anataarifu kuwa CALAS wameilalamikia Wizara ya Nishati, ambayo inapendekeza kurefusha mkataba wa uchimbaji mafuta katikati ya msitu wa mvua. Mwanablogu Tokoloshte anapendekeza kutembelea Laguna Lachua ambayo “itageuzwa kuwa ya viwanda ” na serikali (watajenga barabara kibwa katikati ya hifadhi).

Manuel Boloma kijana wa Maya Q’eqchi’ [es] mwanasayansi wa jamii kutoka Kaskazini (karibu na hufadhi) anapinga kwa nguvu msimamo wa Rais na tabia ya kupuuzia ya watu, ya kutokufanya kitu chochote ili kuilinda kesho. Alisema kuwa hili sio jambo la kiuchumi au la kimazingira bali Serikali ilipotosha vipaumbele, ni kifo cha kujiua kwa Guatemala ya kesho. Anawataka Waguatemala kufunga macho ili kujionea wenyewe jinsi wanavyoharibu thamani ya maisha yao ya baadae.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.