- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali ya Japani: Kuhusu Kuanguka kwa Mfumo wa Ajira

Mada za Habari: Asia Mashariki, Japan, Habari za Wafanyakazi, Uchumi na Biashara

Chombo kinachotumika kufanya tafakari nzito cha Baraza la Mawaziri la Japani, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (内閣府 経済社会総合研究所 [1])(ESRI) kimechapisha matokeo ya utafiti [2] yaliyopima hadhi ya sasa ya ajira ya maisha na ulipaji ujira kwa kutumia cheo cha mtu (yaani, mfumo wa ajira wa Kijapani [3]). Walitumia data (1989 – 2008) kutokana na Taftishi ya Msingi ya Mfumo wa Ujira (賃金構造基本統計調査 [4]) inayojulikana kama BSWS ya Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi wa Jamii. Matokeo na Maoni yanayopimika yanaashiria uwepo mdogo sana wa uzuiaji unaofanywa na serikali wa mfumo wa ajira wa kimapokeo.

Utafiti huo umechapishwa hapa [5].

Moja ya matokeo waliyoyapima yalikuwa “upinde wa ujira.” Huu, kimsingi, ni Ujira wa Kati uliowekwa katika kiwango fulani kwa wafanyakazi kwa mujibu wa umri wao. ESRI ilionyesha kwamba upinde wa ujira “hufutilia mbali tofauti” kadiri muda unavyopita. Jambo hili linaashiria kwamba wafanyakazi vijana wanapojitolea sadaka baadhi ya malipo kwa ajili ya kupata mtindo fulani wa maisha usioyumba hapo baadae, kwa kweli hawaishii kupata thamani inayostahili katika hali ya sasa ya maisha. Tazama jedwali lifuatalo: (tafadhali libofye ili kulikuza!)

Kwa upande mwingine, matokeo ya pili yanatoka kwenye data za kiasi cha wafanyakazi wa kudumu wa kampuni fulani. Takwimu zinaonyesha kiwango kikubwa cha kushuka kwa mwenendo miongoni mwa wafanyakazi vijana. Jambo hili linaashiria kuwepo kwa viwango vya chini vya kumweka mfanyakazi kwa wafanyakazi vijana na wafanyakazi watu wazima wanaoendelea kubaki katika kazi zao za zamani kwa kuwa ni jambo la kuhatarisha sana kujaribu kutafuta kazi nyingine. Kwa namna ya pekee, tunaona anguko kubwa kwa mwaka 2004 kwa makampuni makubwa, kwa kuwa huo ndiyo mwaka ambao serikali iliwezesha kutumiwa kwa wafanyakazi wa muda [6] katika viwanda vya uzalishaji bidhaa. Jambo hili linamaanisha kwamba uendelezaji wa mfumo huo unaweza usiwe endelevu. Tazama jedwali lifuatalo: (tafadhali libofye ili kulikuza!)

Mwanablogu, mwandishi wa vitabu na mshauri wa biashara, Jo Shigeyuki, anafikiri kwamba ni jambo kubwa [7] kwamba Serikali hatimaye imekiri “kuanguka” kwa mfumo wa Japani wa ajira. Lakini pia anakasirishwa na kukosekana kwa umakini na kwa kazi ya kuzibaziba tu viraka iliyofanyika (kama vile kuruhusu kwa wafanyakazi wa muda [8]) kulikoonyeshwa katika kujaribu kuuweka sawa mfumo huo. Hapa chini anaonya kuhusu uwezekano wa kutokueleweka kwa matokeo ya utafiti wa ESRI:

賃金カーブの低下を指して「中高年も賃下げされている」と屁理屈を述べる労働組合関係者がたまにいるが、中高年は賃下げされたのではなく逃げ切ったというのが正しい。90年頃、「若い間は辛抱辛抱」と言い聞かせて頑張った元若者は、20年近く経って、かつての上司・先輩より 3割以上も給料が安い結果に終わったということだ。

バブル崩壊後に、年功ではなく働きに応じて支給する仕組みにシフトしておけば、彼の生涯賃金はもう少し多かったろうが、そういう努力を怠ったということで自己責任というしかない。

さて、このように身をもって日本型雇用の破綻ぶりを演じてくれている世代がいるのだから、20代は同じ轍を踏まないように気をつけないといけない。というわけで、働きを基準としている組織に自分で移るか、それが出来るよう準備しておくことをおススメする

Kwa kuchunguza upinde huo wa ujira, mara nyingine huwa ninawasikia baadhi ya watu walio katika vyamba vya wafanyakazi wakisema, “mishahara ya watu wa umri wa kati hadi wazee inakatwa,” lakini ni afadhali zaidi kueleza hali yao kwa kusema kwamba hao wamewahi kuepuka mambo tangu mapema. Katika miaka ya 90, wafanyakazi vijana wa enzi hizo walifanya kazi kwa bidii na kuishia kupata punguzo la asilimia 30 kwa kulinganisha na wakubwa zao, miaka 20 baadaye. [Kwa maelezo hayo anamaanisha kwamba ilikuwa ni punguzo tu la ujira na wala si kukuta hakuna kazi inayopatikana].
Baada ya mabadiliko makubwa ya mambo, kama mfanyakazi kijana wa hapo awali angeweza kuendana na mfumo unaotazama zaidi utendani kazi, ujira wao wa maisha ungekuwa bora zaidi. Lakini wanaopaswa kuwajibika ni wale ambao wenyewe hawakuchukua jukumu la kuandaa mfumo ulio bora zaidi.

Sasa, kwa vile kuna vizazi kamili vya wafanyakazi walioonja kuporomoka kwa mfumo wa ajira wa Japani, vijana wa sawa wenye umri wa miaka 20 hivi wanahitaji kuwa makini ili wasije kuangukia katika mtego kama huo. Kwa hiyo, ninawahimiza watu kubadili au kuwa tayari kubadili kazi kwa kwenda kwenye taasisi zinazothamini zaidi kazi.

Mwanablogu na mchumi Ikeda Nobuo anajenga nadharia fikirifu kuhusu sababu [9] zinazowafanya raia wa Japani kwa ujumla kuwa na tabia ya kukwepa hatari badala ya kurekebisha mambo. Mfumo wa ajira wa Japani ulikuwa matunda ya mashirika makubwa yaliyothamini kutoyumbayumba kwa haliya mambo:

[…]私の仮説は17世紀以降の株式会社のような有限責任の制度が日本になかったことが一つの原因ではないか、というものです。近代資本主義の成功をもたらした最大の要因が株式会社制度だったのではないか[…]

西欧圏でも株式は投機の手段として批判され、また現実にバブルや恐慌の原因となってきました。しかし資本主義を批判したマルクスは、株式会社制度を「生産の社会化」を進める制度として高く評価しました。これによってリスクが社会全体に分散されたことが、西欧圏の比類ない成長をもたらしたのです。

ところが日本では、株式を「銘柄」と呼ぶことでもわかるように、商品相場のような投機の対象として扱われ、戦前にはその9割が先物で、リスクは非常に高かった。株式が企業のリスクを分散する有限責任制度として活用されず、経営者は会社に無限責任を負い、会社がつぶれたらしばしば自殺します。他方、家計にとっては超ハイリスクの株式とリスクゼロの預金しかないため、ほとんどの人は危ない株には手を出さず、リスクを分散するという考え方も知らない。

Nadharia yangu [kwa tabia ya waJapani ya kuepa hatari] ni kwamba katika miaka baada ya karne ya 17, Japani hakuwa na mfumo wa uwajibikaji wenye kikomo kama mashirika makubwa ya hisa zilizoshikamanishwa. Naamini kigezo kikubwa kilicholeta mafanikio ya ubepari ilikuwa ni mashirika ya hisa zilizoshikamanishwa.
Kule Magharibi, hisa za soko la hisa zilikosolewa kama njia ya upekenyuzi, na sababu ya kuibuka na migogoro ya kifedha. Lakini pale Karl Marx alipoukosoa ubepari, mashirika ya masoko ya hisa yalimiminiwa sifa kama mfumo wa kufanya mchakato wa uzalishaji kama suala la kijamii. Kwa hiyo, hatari hiyo iligawanywa kwa jamii nzima kama ufunguo wa ukuaji usio na mipaka kule Magharibi.

Lakini kwa upande wa Japani, mashirika ya masoko ya hisa yaliyoshikamanishwa yalitazamwa kama alama na bei za bidhaa zilichukuliwa kama nyenzo za kufanya upekenyuzi; kabla ya vita, asilimia 90 ya bidhaa zilikuwa kwa ajili ya baadaye na kwa hiyo hatari ilikuwa juu zaidi. Hisa za mashirika hazikuchukuliwa kuwa kama nyenzo za kuepusha hatari na makampuni yalikuwa na wajibu usio na kikomo kwa kuwa yangeweza kujimaliza kama kuna mahali mambo yasingekwenda sawa. Kwa upande wa ngazi ya kaya, njia pekee iliyokuwepo ilikuwa ni kuendelea kubaki na hisa zilizo kwenye hatari kwelikweli au kutokuweka akiba, kwa hiyo kaya zilizo nyingi zilichagua njia hiyo ya pili.

Mwanablogu na mwanafunzi katika chuo cha MIT, Lilac anatukumbusha kwamba miongo ipatayo miwili iliyopita Amerika [10] nayo ilikabiliana na hali ya namna hiyo hasa katika kuanguka kwa ushindani kwa baadhi ya makampuni (Kodak, Motorola, RCA). Anajaribu kutafakari kama ni bora zaidi kwa kampuni kubwa kujifanyia marekebisho au kukubali kuanguka na kisha kuanza kila kitu upya:

決して経営陣が技術を知らないバカなわけでも、技術者がツカえないわけでもないのだ。経営の舵取りを間違えただけで、これだけの技術と、研究者の努力が無駄になってしまう。大企業の組織を改変し、新しい技術に対応するように全体を変えていくのは、かくも難しいことなのだ。

「技術が優れてるから勝てる」わけではない、ということは、こうしてアメリカの企業たちは、日本企業やヨーロッパの企業に追いやられながら学んできていているのだ。

日本企業が、これらのアメリカ企業のように崩壊の一途をたどるか、IBMやGEがそうであったように再生するかは、今の経営の舵取りにかかっている。

[Kuhusu kuanguka kwa Kodak, n.k.] Sio kwamba menejimenti haikuelewa teknolojia au kwamba wahandishi walikosa ubunifu. Kosa katika kuendesha kampuni kuelekea upande usio sahihi husababisha hasara kubwa hasa katika juhudi za wahandisi na watafiti. Kubadilisha urekebishaji mambo wa makampuni makubwa na kujaribu kuendana na teknolojia mpya kwa kawaida ni jambo gumu.
Sio lazima kwamba mawazo bora na teknolojia ndiyo hushinda. Makampuni ya Marekani yamejifunza funzo gumu sana kutokana na makampuni yanayohangaika ya Ujapani na Ulaya.

Kwa makampuni ya Kijapani kufuata njia ya Kodak na mengineyo au makampuni yaliyofaulu kuendana na hali halisi (GE, IBM), yote inategemea uamuzi fulani kutoka juu ambao au unategemaza au unavunjilia mbali kampuni.

Mwanablogu na mfanyakazi wa Teknolojia ya Habari (IT) elm200 anapendekeza (kwa kejeli) suluhisho [11] ambalo halitavuruga manufaa yanayowafanya viongozi huko Ujapani wabaki walipo – kuanzisha jiji linalojitegemea ni kinyume cha hali za kazi nchini Japani:

結局のところ、この国は現状維持を望む人が多いのだ。現状維持を望んでいる人々が多数派であるなら、どうして制度をいじる必要があるだろうか。一部の若者が騒いだところで、それより数が多い中高年や老人は現状に満足しているのだから、ガラパゴスだろうが鎖国だろうが、好きにさせてあげるのが一番だ。

好きにさせてあげるのだから、こちらにも一つくらいわがままを許してくれてもいいだろう。既得権益には何一つ接触しないので、疑り深い老人たちも何もいわないだろうし。

日本にシンガポールを作るのだ。

Kimsingi, nchi hii ina maelfu ya watu wanaopendelea hali kama ilivyo. Kama wao ndiyo wengi zaidi, kwa nini iwe lazima kuurekebisha mfumo? Hata kama baadhi ya vijana watajaribu kuvuruga mchakato, walio wengi (wafanyakazi wenye umri wa kati na wazee) wanaridhika na hali ya mambo iliyopo, kwa hiyo njia nzuri zaidi ni kuacha mambo yaendelee.
Kwa sababu tunaruhusu hali iwe hivyo, basi halipaswi kuwa jambo la kupasua vichwa kwamba tuwe na ombi moja la kiuchoyouchoyo. Halitagusa maslahi yaliyopo kwa hiyo wale wazee wanaonufaika wasipate sababu ya kusema kitu.

Hebu tuijenge Singapore nchini Japani.

Japani ipo katika mkwamo mkubwa. Kuurekebisha mchakato wa ajira, watu wengi wanashauri uhamaji kazi, jambo linalolisha ujasiriamali. Kwa upande mwingine, ujasiriamali ni kiashiria chenye hadhi cha uhamaji kazi. Hivi karibuni niliandika makala kuhusu viwango vya ujasiriamali nchini Japani [12] na kukuta kwamba kiwango kiko chini sana ukilinganisha na nchi nyingine.

Mifululizo miwili inayovutia inayojadili makali ya ajira hivi sasa katika vyombo vya habari:

1. Nikkei Business: “Nafasi za kazi zilizofutwa – Ni kwa sababu hii niliingizwa mkenge” [13]
2. J-cast: “Kwako, ambaye una miaka 29 na bado unafanya kazi. Bado hujachelewa!” [14]