Habari kutoka Machi, 2010
Kenya: Mafuriko Makubwa Yapasua Kingo za Mto Ewaso Nyiro Huko Samburu
Alfajiri siku ya Alhamisi, tarehe 4 Machi 2010, mafuriko makubwa yaliikumba Samburu huko kaskazini mwa Kenya na kuharibu nyumba 6 za kulala watalii watalii, baadhi ya kambi za utafiti wa wanyama pori na kuwaacha maelfu wakiwa katika paa za nyumba na kwenye miti. Wimbi hili la maji ya mafuriko lilikuja...
Video: Tetemeko la Ardhi Chile Kwa Kupitia Macho ya Raia
Wakati siku inakaribia kuisha, video zaidi za tetemeko la ukubwa wa 8.8 ambalo liliikumba Chile majira ya saa 9.30 usiku zinajitokeza. Tetemeko hilo, ambalo halikuathiri maeneo ya bara pekee kwa njia ya kusogea sogea kwa ardhi, kadhalika lilisababisha mawimbi ya tsunami mabyo yalizua tahadhari katika eneo zima la Pasifiki huku mataifa mbalimbali yakijiandaa kwa mawimbi hayo pindi yatakapofika kwenye fukwe zao.