Jamhuri ya Dominika: Upinzani Dhidi ya Shughuli za Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Barrick

Mnamo mwaka 2009, watu wa Dominika walisimama kidete kukipiga vita kiwanda cha sementi ambacho kilikuwa kianzishwe katika Hifadhi ya Taifa ya Los Haitises. Katika mwaka huu wa 2010, yaelekea kuna harakati zinazowahamasisha maelfu ya vijana na watu wazima – kuhusu uwepo wa makubaliano ya uchimbaji dhahabu na Kampuni ya Barrick huko Cotuí, mji ambao ni manispaa kubwa zaidi katika jimbo la Sánchez Ramírez, ambayo ni moja ya sehemu zenye shughuli kubwa zaidi za uchimbaji madini ulimwenguni: la Pueblo Viejo (Mji wa Zamani) huku eneo hilo likikadiriwa kuwa na troi milioni 24 za onsi za dhahabu. Wanaharakati wana wasiwasi kuhusu makubaliano yaliyofikiwa na Dola la Dominika na vilevile nini yanaweza kuwa madhara kwa mazingira.

Picha imetumiwa kwa ruhusa ya NO A LA BARRICK, BATEALA DEL PAIS

Picha imetumiwa kwa ruhusa ya NO A LA BARRICK, BATEALA DEL PAIS

Historia ya miongo ya karibuni ya machimbo ya dhahabu ya Pueblo Viejo,ambayo hutoa oksidi ya dhahabu kwa upande wa juu na sulfidi ya dhahabu kwa upande wa chini, inaanzia mwaka 1975 chini ya Shirika la Maliasili la Rosario, kampuni ambayo hapo baadaye ilikuja kumilikiwa na Dola la Dominika chini ya jina la Rosario Dominicana, ambapo shughuli zake zilisitishwa moja kwa moja mnamo mwaka 1999 kwa sababu za kiuchumi na kimazingira. Mnamo mwaka 2002, mgodi huo ulipata mmiliki mwingine aliyekodishwa uendeshaji, Kampuni ya Kikanada ya Placer Dome, ambayo iliingia makubaliano ya miaka 33 kabla haijanunuliwa na kampuni nyingine ya Kikanada ya Uchimbaji Dhahabu ya Barrick mnamo mwaka 2006. Tangu wakati huo Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Barrick imekuwa si jina geni miongoni wa raia wa Dominika hasa baada ya taarifa fulani kuhusu mkataba iliotia saini na Dola la Dominika kuwekwa hadharani, na mkataba huo uliridhiwa mwishoni mwa mwaka 2009 na Bunge kwa kupata idadi kubwa ya kura za wabunge.

Marihal, anayeshughulika na blogu inayoitwa Desde la República Dominicana [es], anasisitiza vipengele vifuatavyo kuhusu mkataba uliotiwa saini upya:

La Barrick Gold es la empresa minera más grande del mundo, en materia de oro, y adquirió a la Placer Dome en el año 2006, esta última compañía tenía un contrato que firmó en el 2002 con el Gobierno dominicano donde se había establecido que el Estado dominicano iba a recibir un 25% de las utilidades, sin incluir los impuestos y otros beneficios que alcanzaban el 3.2%. Sorpresivamente, la Barrick Gold consigue unos cabilderos (…) que logran que el 25% que recibiría el Estado dominicano con la Placer Dome subiera a 28% con la Barrick Gold, pero siempre y cuando se recupere toda la inversión y que la tasa de retorno sea superior al 10 por ciento.

Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Barrick ndiyo kampuni inayoongoza duniani, hasa kwa kuzingatia kiasi cha dhahabu na baada ya kuwa imeinunua Placer Dome mnamo mwaka 2006. Kampuni hiyo ya pili mnamo mwaka 2002 ilikuwa imetiliana saini na serikali ya Domonika ambapo katika makubaliano hayo, Dola la Dominika lingestahili kupokea 25% ya faida, bila ya kujumlisha kodi na mafao mengine yanayofikia 3.2%, ambalo ni jambo la kushangaza, Kampuni ya Dhahabu ya Barrick ilipata wa kuipigia debe (…) ambao walipiga chapuo kwamba asiliamia 25 ambayo Dola la Dominika lingepata chini ya Placer Dome ingeongezeka na kufika 25% chini ya Kampuni ya Dhahabu ya Barrick, lakini ni baada tu ya kuwa gharama za uwekezeaji na kiwango cha urejeshaji gharama kuzidi 10%.

Harakati za kutaka mkataba mpya na Dola la Dominika mara baada ya Kampuni ya Dhahabu ya Barrick kuinunua Placer Dome lilikuja baada ya bei ya dhahabu kupanda, na ambayo imekuwa ikipanda kwa kiasi kilekile tangu mwaka 2002 kufuatia migogoro ya chakula na kifedha – yote miwili ikiwa ni katika ngazi ya dunia, ambapo ilipanda hata kufikia bei ya dola ya Marekani 1,000 kwa onsi moja, jambo ambalo lilikuwa na maana kwamba kadiri bei ilivyokuwa juu katika soko, ndivyo faida ilivyokuwa kubwa katika kipindi hicho. Mwanajiolojia na mwanablogu Osiris de León anaelezea jambo hili namna hii [es]:

(…) como el precio del oro ha ido en ascenso rápido y ha superado los 1,000 dólares por onza, ello implicaría una participación del Estado en las Utilidades Netas (PUN) de US$194 millones por año, fruto de que la Barrick piensa producir en Pueblo Viejo un millón de onzas de oro anualmente, y al multiplicar 1,000,000 de onzas de oro por US$775, que es el diferencial entre el precio del oro en este momento (US$1,050/onza) y el costo de producción (US$275/onza), y luego multiplicarlo por el 25%, obtenemos unos 194 millones de dólares anuales para el Estado. Y la Barrick se niega a entregar tanto dinero.

Por tal razón la Barrick Gold ha obligado al Estado Dominicano a una renegociación del contrato original, a fin de que esa participación estatal del 25% de las utilidades netas sea llevada a cero, óigase bien, a cero, mientras ellos no hayan obtenido una tasa interna de retorno (TIR) de un 10% y hasta haber recuperado los US$2,585 millones invertidos para desarrollar el proyecto, y a partir de ahí pagar un 28.75% como PUN, con lo cual la Barrick le quita 194 millones de dólares anuales al pueblo dominicano, durante al menos los primeros 6 años de operación, lo que implicaría que durante esos 6 años el pobre pueblo dominicano dejaría de percibir unos 1,164 millones de dólares, a los precios de hoy.

(…) Kwa kuwa bei ya dhahabu imekuwa ikipanda kwa kasi na sasa imepita dola za Marekani 1,000 kwa kila onsi, ina maana kuwa ushiriki wa Dola letu katika kila mapato yanayoingia (PUN) yanayofikia dola za Marekani milioni 194 kwa mwaka, na kwa kuwa Barrick wanafikiria kkwamba Pueblo Viejo itatoa onsi milioni moja kila mwaka, na ukizidisha onsi 1,000,000 za dhahabu na dola za Marekani 775, ambayo ndiyo tofauti kati ya bei ya dhahabu kwa sasa (dola za Marekani 1,050/kwa onsi moja) na gharama za uzalishaji (dola 275 kwa onsi) na kisha kuzidisha na 25%, tunapata kama dola za Marekani milioni 194 kwa mwaka kwa ajili ya Dola letu. Na Barrick wamekataa kulipa fedha hizo.

Kwa sababub hiyo, Kampuni ya Dhahabu ya Barrick imeilazimisha Dola ya Dominika kuingia upya kwenye mkataba dhidi ya ule wa awali, ili kwamba kile kiasi cha 25% cha faida ghafi cha Dola letu kipunguzwe mpaka kufika sifuri, hebu sikiliza kwa makini hapa, ipunguzwe mpaka sifuri, wakati ambapo bado hawajapata marejesho ya 10% na mpaka wawe wamejirejeshea dola za Marekani bilioni 2.585 walizowekeza katika mradi huu, na kisha ndiyo walipe PUN ya 28.75%, yaani Barrick wanachukua zile dola za Marekani milioni 194 kwa mwaka kutoka kwa watu wa Dominika kwa walau miaka 6 ya mwanzo y uzalishaji, jambo hili lina maana kwamba ndani ya kipindi hicho cha miaka 6, watu wa Dominika hawatapokea dola za Marekani bilioni 1.164 kwa bei ya sasa.

Wakati ambapo baadhi ya watu wanaamini kwamba mkataba huu unawaacha watu wa Jamhuri ya Dominika katika hasara, hii siyo sababu pekee ya kuipinga kampuni hiyo. Kuna wasiwasi kuhusu madhara ambayo yatasababishwa na shughuli za Kampuni ya Dhahabu ya Barrick katika mazingira, hasa kwa sababu ya sifa mbaya ambazo kampuni hilo kubwa kabisa limejizolea duniani kote, kitu ambacho hata watu wa Dominika wanakifahamu. Ama kwa hakika, kumekuwepo na kelele nyingi za umma zinazoipinga kampuni hii [es] na tayari kumekuwepo na makundi kadhaa yanayotumia ukurasa wa Facebook [es]. Pia kuna blogu imeanzishwa na kupewa jina la Domincana Contaminada [es] (Dominika Iliyochafuliwa) ambayo imejikita katika kuibua visa vyote vya uharibifu wa mazingira ambapo Kampuni ya Dhahabu ya Barrick imehusika navyo, kama vile kule Pascua Lama [es] huko nchini Chile na uchafuzi wa mazingira katika Ziwa Cowal kule Australia. Blogu hiyo pia inaweka bayana mkataba uliopitishwa na watunga sheria wa Jamhuri ya Dominika, kuondolewa kwa nguvu kwa wakazi wa eneo linalohusika, na kazi ambayo mpaka sasa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick imefanya ili kuupanga upya mgodi huo, jambo ambalo limegonga vichwa vya habari katika siku za karibuni kwa wafanyakazi zaidi ya 300 kupata sumu kwa sababu ambazo bado haziajelezwa. Wakati ambapo kampuni hiyo inazungumzia kupatikana kwa tatizo hilo la sumu kupitia chakula [es], wengine wanasisitiza kwamba sumu hiyo ilitokana na kulipuka kwa mtambo wa kuyeyusha miamba [es].

Kutokana na mashinikizo makali ambayo Kampuni ya Dhahabu ya Barrick imekuwa ikiyapata kutoka kwa raia wa Jamhuri ya Dominika, kampuni hiyo imeona umuhimu wa kuanzisha haraka programu za ujirani uhusiano na umma, na kwa hiyo wameanza kuja na vitu kama taarifa kwa vyombo vya habari ambayo kampuni hiyo inayalipia katika magazeti ya kitaifa na televisheni za kitaifa. Wawakilishi wao wanajitahidi kuonyesha manufaa yatakayotokana na kuwepo kwao huko Cotui.

Pamoja na juhudi hizo za uhusiano wa umma, bado watu wanaendelea kuipinga kampuni hiyo. Katika kipindi hiki cha Juma Kuu, hija ya siku nne imepangwa ambapo washiriki watatembea umbali wa km 9 kutoka Barabara Kuu ya Duarte kuelekea yalipo machimbo kule Cotuí. Waandaaji wa matembezi hayo wanatarajia kwamba zidi ya watu 10,000 watashiriki kutembea km 105 ili kuipinga Kampuni ya Dhahabu ya Barrick ili kulinda mazingira ya Cotuí, ambayo tayari yameharibiwa na shughuli za Rosario Dominicana, kama anavyoeleza Alexander Medina, ambaye ana uzoefu wa miaka 30 katika sekta ya uchimbaji madini [es].

Una vez procesados los óxidos de oro, los sulfuros quedaron expuestos y la mina fue abandonada a su suerte, permitiendo que esta drenara hasta la Presa de Hatillo aguas ácidas del río Margajita, producidas por la mezcla del agua de lluvia y el mineral de los sulfuros de oro que quedó al descubierto. Otro impacto ambiental negativo legado por Rosario es la acumulación de metales pesados como el hierro, cobre y mercurio en el sitio de la vieja planta y en los lodos del lecho de los ríos Mejita y Margajita.

Mara baada ya oksidi ya dhahabu kuchekechwa, sulfidi hubaki ikiwa wazi na kisha mgodi kutelekezwa kujiharibikia wenyewe, jambo hili husababisha maji yenye tindikali kutoka Mto Margajita kuisomba na kuipeleka katika bwawa la Hatillo, na kufanya mchanganyiko wa maji ya mvua na mabaki ya madini kutoka katika sulfidi ya dhahabu ambayo ilikuja kugunduliwa baadae. Mabaki mengine ya taathira mbaya ya kimazingira kutoka Rosario ni mkusanyiko wa madini nzito kama vile chuma, shaba, na zebaki katika mgodi huo wa zamani na slaji kutoka mito ya Mejita na Margajita.

Paola Mejía Sandoval, anayeongoza kundi la NO A LA BARRICK GOLD, BATEALA Y SACALA DEL PAIS [es] (Hapna kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick, wapige na wasukumie mbali watoke nchini) anahitimisha hisia za baadhi ya raia wa Dominika kuhusina na Kampuni ya Dhahabu ya Barrick:

Si no peleamos ahora por defender lo que es nuestro quizas manana dej de pertenecernos entonces, por que lucharemos??? nosotros debemos plantarnos en favor de nuestros ideales. NO A LA BARRICK GOLD EN REPUBLICA DOMINICANA.

Kama hatutapigana kutetea kilicho chetu, si ajabu kesho hakitakuwa chetu tena. Kwa nini tunapigana? Hebu tusimame tutetee ndoto zetu njema. Hatuitaki Kampuni ya Dhahabu ya Barrick katika Jamhuri ya Dominika.

2 maoni

  • bab liii

    sio sementi bali ni saruji

  • Bab Lii

    Asante sana kwa maoni yako. Ni kweli. Neno ‘saruji’ lina mashiko zaidi kama neno la Kiswahili kuliko ‘sementi’. Ndiyo. Mara nyingine katika kufanya tafsiri – hasa muda unapokuwa mdogo – kuna maneno yanakuwa mbali kichwani pamoja na kwamba unakuwa unafahamu maneno hayo.

    Nakualika kuwa mmoja wa watu wanaojitolea kutafsiri kwa ajili ya ukurasa huu wa Swahili lingua. Ukiperuzi vema utaona kwamba tunahitaji watu wengi zaidi wa kujitolea. Naamini una mapenzi na lugha ya Kiswahili na bila shaka upo tayari kuona kinaenea duniani pote na vilevile bila shaka unapenda kuwafahamisha wazungumzaji wa Kiswahili kuhusu yale yanayotokea mahali kwingineko duniani. Hii ni fursa moja muhimu. Karibu. Wasiliana na mhariri wetu naye atakupa maelekezo zaidi ya namna gani unaweza kujiunga.

Sitisha majibu

jiunge na Mazungumzo -> Deogratias Simba

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.