- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Chile: Tetemeko la Ardhi Lafichua Ukosefu wa usawa Katika Jamii

Mada za Habari: Amerika Kusini, Chile, Maendeleo, Majanga, Mwitikio wa Kihisani, Uchumi na Biashara

Tetemeko la ardhi lililotokea Februari 27 nchini Chile [1] liliwapotezea makazi zaidi ya watu milioni mbili, kwa uchache vifo 497 viliripotiwa [es] [2], na makadirio ya hasara ya dola 30 bilioni [3]. Hata hivyo, uvunjaji sheria uliojitokeza baada ya tetemeko pia uliwaacha watu wa Chile na swali la kimaadili: je jamii ya Chile ina usawa?

Baada ya tetemeko kutokea, wengi wa watu wa Chile waliwasaidia wenzano, waliwasaidia majirani zao wenye shida, walishirikiana kwa chakula cha ziada, na walichanga fedha katika njia zilizozidi viwango [4]. Hata hivyo, kuna wachache, bila kujali ni wachache kiasi gani, walipora vifaa na mahitaji yasiyo ya msingi, walifanya ujambazi majumbani, na kwa makusudi walichoma moto maduka [5], bila kujali ukweli kwamba serikali ya Chile iliruhusu watu kuchukua mahitaji, kama vile maziwa, maziwa ya unga ya watoto, mikate na unga.

Picha ya soko tupu huko Concepción iliyopigwa na heedmane na kutumika kwa leseni ya Haki Hiliki Huru (creative commons).

Picha ya soko tupu huko Concepción iliyopigwa na heedmane na kutumika kwa leseni ya Haki Hiliki Huru (creative commons).

Vituo vya Televisheni vya Chile viliufikisha ukweli huu kwenye mamilioni ya ngumba kwa mtindo sahihi [es] [6], na hivyo waChile walijionea jinsi baadhi walivyojisaidia kuchukua televisheni za kisasa za plasma, majokofu na vichezea DVD. Taswira za jinai na uporaji, na hasa uporaji wa mahitaji yasiyo ya lazima, zilianzisha mjadala wa taifa kuhusu kutokuwepo kwa usawa kijamii na kiuchumi nchini Chile.

Katika makala yenye kichwa kinachosema “Ni aina ipi ya mti tulioumbwa nao? [es] [7],” Ricardo Carbone, mwanablogu, profesa, na Mkurugenzi wa Kituo Cha Tathmini ya Jamii na Harakati [es] [8] katika Chuo kikuu cha Hurtado, anadai kwamba tetemeko liliweka wazi matatizo makubwa ya kijamii, na kwamba ilivunja ugo unaopendeza wa nje na muonekano wa jamii ya Chile. Hapa Carbone anamaanisha ugo unaopendeza wa nje wa watu waliopora mahitaji yasiyo ya lazima na kuharibu zaidi hali ambayo ilikuwa tayari ni mbaya:

…al igual que en los edificios que cayeron, la fachada era de ciudadanos bien formados y conectados con el mundo y el consumo, pero el interior no estaba soportado por valores sólidos ni principios fuertes. Rápidamente y ante la primera dificultad corrieron a tomar lo que pudieron.

… kama majengo yaliyoporomoka, sura ya nje ya [watu wa Chile] ilikuwa ni ile ya watu walioelimika vizuri ambao wana uhusiano mzuri na dunia pamoja na soko la walaji, lakini undani wao haukuwa na kanuni imara wala msingi madhubuti kimaadili. Kwa haraka, na baada ya ishara ya kwanza ya matatizo, waliharakia kupora walichoweza.

Mwanablogu huyu anawahimiza watu wa Chile wasijenge miundombinu yao tu, bali pia wasimike tena maadili ambayo yatajenga jamii bora zaidi na iliyo shirikishi. Pia aliwauliza wasomaji:

¿podemos esperar algo distinto en un sistema que genera segmentación y exclusión social?, ¿es el producto de una sociedad que obliga a competir y arreglárselas solo?

Je tunaweza kutegemea kitu tofauti katika mfumo ambao unatengeza utengano na watu kutengwa katika jamii? Je hili ni zao la jamii ambayo inalazimisha ushindani na utatuzi wa mambo unaomtegemea mtu mwenyewe?

Wasomaji wengi wa blogu hii waliafikiana na dhana ya kwamba Chile inahitaji jitihada kubwa katika elimu na mafunzo ya maadili. Msomaji mmoja miongoni mwao alikuwa Alejandra Muñoz:

Se nos rompio la burbuja y duele ver la verdad. Ahora hay que entenderla, asumirla y trabajar por recontruir nuestros edificios y nuestra sociedad. Se puede perdonar, pero no podemos olvidar lo que ha pasado, ya que habra una proxima vez y no nos puede pillar sin aprender de lo errores.

Kupasuka kwa povu letu na ukweli unauma. Na sasa inatupasa tuelewe hilo, na kulikubali, na kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi mpya wa majengo yet una jamii. Tunaweza kusamehe, lakini hatuwezi kusahau yale yaliyotokea, kwani kutakuwa wakati mwingine na wakati huo hautatukuta bila ya mafunzo yaliyotokana na makosa yetu.

Japokuwa watu wengi wa Chile wanakubali kuwa mfumo wa elimu wa umma haujafanikiwa katika kutoa fursa sawa kwa wa-Chile wote, uporaji wa mahitaji yasiyo ya lazima hakukutokana na kutokuwepo kwa “maadili mema” peke yake.

Coyuntura Política [es] [9], blogu ya ki-Chile, ilichapisha makala Tetemeko la Ardhi na Mivunjiko ya Chile [10] iliandikwa na Jose Aylwin [11], Mkurugenzi mwezna wa Observario Ciudadano [es] [12], asasi isiyo ya kibiashara ya haki za binadamu iliyoko katika jimbo la Araucanía. Kuhusiana na uporaji wa mahitaji yasiyo ya lazima, Aylwin anaandika:

Tales saqueos, al menos en algunos casos, encuentran su explicación en la percepción de injusticia que existe en sectores de la población que, en momentos de emergencia como este, consideran válido vaciar los estantes de las grandes tiendas y supermercados que, con el aval del estado, han acumulado riquezas a sus expensas, mientras ellos permanecen empobrecidos.

Uporaji huu, japo katika visa vichache, unaweza kufafanuliwa na mtazamo wa ukosefu wa haki ambao upo katika mafungu ya watu ambayo, katika nyakati za dharura kama wakati huu, huchukulia kama ni haki kusafisha safu za maduka makubwa na masoko ambayo, pamoja na kuungwa mkono na serikali, yamejikusanyia utajiri kutokana na nguvu zao (waporaji), alhali wao (waporaji) wamebaki maskini.

Katika makala Uharibifu Ambao Haukukusudiwa [es] [13], Patricio Navia, mwanablogu ambaye pia ni profesa, anaeleza kwamba katika majanga ya asili kama haya katika nchi nyingine, ukiukwaji wa taratibu pia hutokea. Kwake, kosa linabaki kwa serikali.

De haber actuado en consecuencia con el discurso de la normalidad democrática y asumiendo como realidad las repetidas arengas sobre el buen funcionamiento de nuestras instituciones, Michelle Bachelet hubiera tomado las medidas necesarias- incluido el envío de tropas a las zonas afectadas- para asegurar la paz y el orden … mucho antes de que las imágenes de saqueos y pillajes se hayan convertido en parte dolorosa -y evitable- de esta tragedia que enluta al país en su bicentenario.

Kama Michelle Bachelet angetenda sawa na kauli za utaratibu wa kidemokrasia, na kuchukulia kama ukweli zile risala za jazba zinazorudiwa kila mara kuhusu utendaji unaotakikana wa taasisi zetu, basi angechukua hatua zinazohitajika, pamoja na kupeleka wanajeshi katika maeneo yaliyoathirika, ili kuhakikisha usalama … muda mrefu kabla ya picha za uporaji na uharamia kuwa maumivu na sehemu iliyoweza kuzuilika ya janga hili ambalo limeitia dosari nchi yetu waklati wa maadhimisho yake ya miaka mia mbili.

Video na mtumiaji wa YouTube IORITER1 [14] iliyopigwa sehemu za Concepción:

Katika blogu ya Humanism and Connectivity [es] [15], Andrés Schuschny aliweka makala yenye kichwa kinachosema Tetemeko [es] [15]. Aliezea uporaji kama ifuatavyo:

Es terrible como una catástrofe natural desenmascara el rostro de la desigualdad de un país cuyos dirigentes no quieren asumirla. Porque, por ejemplo, si el 10% de los ingresos del cobre se hubieran, hace años, destinado a la educación pública y los servicios sociales (deudas siempre pendientes en la región) y no a incrementar los presupuestos militares, las compras de armamento sofisticado y el pasaporte a vidas de lujo por parte de los militares de alto rango, tal vez otra sería la historia y los “comunicadores” del sistema no estarían ahora refiriéndose “al LUMPEN” como una caterba de extraterrestres desbocados que afloran sin razón.

Ni vibaya mno jinsi janga la asili linavyoweza kuumbua ukosefu wa haki katika nchi ambayo maofisa wake wanakataa kuikubali hali hiyo. Kwani, kwa mfano, ikiwa 10% ya mapato ya shaba, siku nyingi nyuma, yaliyotakiwa yaende kwenye elimu ya umma na huduma za jamii (madeni siku zote hubaki mikoani) na si kwenda kwenye bajeti zinazoongezeka za jeshi, ununuzi wa silaha za kisasa, na pasipoti za starehe kwa wanajeshi wenye vyeo vya juu, pengine historia ingelikuwa tofauti na “wana-mawasiliano” wa mfumo wasingekuwa wanawaita “LUMPEN” au WAHUNI (kundi la chini kabisa katika jamii) kana kwamba ni kundi la watu kutoka sayari nyingine ambao walijitokeza tu bila sababu yoyote.

Chile, yenye uchumi wenye neema na unaokua katika miongo iliyopita, inachukuliwa kama nchi yenye “maendeleo makubwa ya watu” na Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP). Pamoja na hayo, ukuaji huu wa kiuchumi unatiwa doa na kukosekana kwa usawa katika kipato cha watu. Takwimu katika Ripoti ya UNDP ya Maendeleo ya Watu ya 2009 (pdf) [16] inaonyesha kuwa katika nchi 147 zenye vipimo vinavyopima kukoseka usawa katika kipato cha watu nchini (Gini Coefficient [17]) , chile ni 124, pamoja na ukweli kwamba (Chile) ni nchi ya 44 katika vipimo vya maenbdeleo ya watu.