Habari kutoka 21 Machi 2010
Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka
“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa...
Uganda: Wanafunzi Wacharuka, Kampala Yawaka Moto
Jumanne, majanga mawili tofauti yaliikumba Kampala, mji mkuu wa Uganda: wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere walifanya ghasia baada ya wanafunzi wenzao wawili kupigwa risasi. Na makaburi ya Kasubi, ambayo ni sehemu ya Urithi wa Dunia ya UNESCO na eneo la kaburi la mfalme wa moja ya makabila makubwa zaidi ya Uganda, liliteketea kwa moto.
Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma
Mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao katika mtandao unaosomwa sana wa jiji la Cairo unaojulikana kwa jina la Islamonline baada ya kuwa wafanyakazi wapatao 250 wamefukuzwa kazi. Kwa mara ya kwanza, wagomaji wanatumia kwa ufanisi na vizuri kabisa aina mpya ya chombo cha habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono katika kile wanachokipigania, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.