17 Machi 2010

Habari kutoka 17 Machi 2010

Afrika Kusini: Ubaguzi wa Julius Malema

Wakati tabia za Rais Jacob Zuma zimekuwa zikizua mijadala mikali na yenye uhai katika ulimwengu wa blogu wa Afrika Kusini, hivi sasa ni mwanasiasa mwenye utata ambaye pia ni rais wa Umoja wa Vijana wa ANC, Julius malema ambaye anatengeneza vichwa vya habari. Hivi karibuni, aliwaongoza wanafunzi katika kuimba wimbo wa zamani wa kupinga ubaguzi wa rangi unaoitwa Ua Kaburu.