Habari kutoka 1 Machi 2010
Video: Tetemeko la Ardhi Chile Kwa Kupitia Macho ya Raia
Wakati siku inakaribia kuisha, video zaidi za tetemeko la ukubwa wa 8.8 ambalo liliikumba Chile majira ya saa 9.30 usiku zinajitokeza. Tetemeko hilo, ambalo halikuathiri maeneo ya bara pekee kwa njia ya kusogea sogea kwa ardhi, kadhalika lilisababisha mawimbi ya tsunami mabyo yalizua tahadhari katika eneo zima la Pasifiki huku mataifa mbalimbali yakijiandaa kwa mawimbi hayo pindi yatakapofika kwenye fukwe zao.