Vazi la Burka Lauelemea Utaratibu wa Tamaduni Mbalimbali Kuishi Pamoja

Tangu mapendekezo ya kupiga marufuku uvaaji wa burqa au hijab huko Ufaransa, suala hilo limekuwa likitokota katika ulimwengu wa bloghu wa Australia. Mtangazaji wa redio katika mtindo wa kushtua umma, ambaye pia ni askari polisi wa zamani, alishutumiwa hivi karibuni juu ya kupinga kuvaliwa kwa hilo vazi la burqa.

Michael Smith alidai kuwa wafanyakazi wa benki na wahudumu madukani wanahofia matumizi mabaya yanayoweza kutokea ya vazi hilo. Pia alisema kuwa watoto wadogo huogopa wanapokuna na wanawake waliovaa “vazi zima la burqa”, alilinganisha kuogopa huko na “watoto wanapolia, wanapoogopa sana wanapomuona Santa Claus”. Mahojiano ya redio na Smith yanaweza kusikika kwenye blogu ya Michael Smith Meets the Press.

Wakati pendekezo la kupigwa marufuku kwa vazi hilo lilipotolewa katikati ya mwaka 2009, mwanahabari wa Canberra Virginia Haussegger alitaka vazi hilo lipigwe marufuku katika blugu yake katika musing ya usawa wa kijinsia:

Kwa kujifunika ndani ya burka, mwanamke huiacha haki yake ya kujieleza kama mwanamke. Anakubali kuikandamiza jinsia yake mwenyewe.

Hakuna nafasi ya burka. Waaustralia ni lazima wajipange ili kwamba burka ipigwe marufuku. Piga marufuku Burka.

Anna Greer katika blogu ya The Punch abnablogu kuhusu, “haki za binadamu na masuala ya haki za jamii na… hali ya dunia”. Ana mtazamo tofauti kabisa juu ya haki za wanawake:

Haidhuru unafikiriaje juu ya kujifunika kwa Kiislamu jambo moja ni la hakika – kuwatia hatiani wanawake wanaovaa burqa au niqab kutawafanya wanawake hao wazidi kutoonekana.

… kuchagua chagua masuala ya kutilia maanani katika haki za wanawake ni njia tu ya watu kuweka bayana ubaguzi wa kitaifa na silica hiyo inaweza kuonekana katika kila ngazi ya jamii – katika umma wa kawaida, katika vyombo vya habari, katika serikali.

Anna anamalizia kwa kejeli:

Kushinikiza sheria za mavazi kwa watu ili kupinga kushinikiza sheria za mavazi kwa watu hakuna manufaa kabisa, na kama nilivyoeleza hapo juu, hiyo siyo sababu ambayo inapelekea kuangaliwa kwa sheria hizo, au?
Kupiga marufuku Burqa kunatokana na hofu zetu na si ukandamizaji wao

Mtazamo wa Smith ulichunguzwa na tovuti ya Andrew Landeryou VexNews:

Ni mjadala unaotisha ambao Smith ameuanzisha katika ngazi moja kwa sababu kuwadhihaki watu katika misingi ya dini au kwa desturi zao za dini ambazo haziwadhuru wengine kunaweza kukawa kama bonde lenye utelezi.

…sehemu ya utata ni kuwa baadhi ya Waislamu – na dini nyingine kwa msingi huu – wanavaa mavazi yanayoziba nywele kama sehemu ya utamaduni wa dini zao. Nadhani hakuna mmoja zaidi ya wabaguzi wenye tatizo na hilo.

Natumaini suala halali la kupigia kampeni hofu za kiusalama kwenye benki au katika maeneo mengine nyeti ambayo yanaweza kuwa malengo ya ugaidi au unyanganyi hayatapotoshwa na ajenda ya wale ambao wana hamu ya kutia dosari moja ya dini kubwa duniani.
UGOMVI WA UPIGAJI MARUFUKU BURKA: Mtangazaji redio asema marufuku kujifunika kwenye benki lakini je anatupa ndoana ya ubaguzi wa rangi?

Katika makala ndefu zaidi katika Online Opinion, Sadanand Dhume, mwandishi wa kitabu cha Rafiki yangu Mkereketwa: Safarini pamoja na Muislamu wa Indonesia, anapigia kampeni pande zote za suala hili lenye hisia. Anahitimisha na mtazamo chanya wa mjadala wa Ufaransa:

Mwishowe, japokuwa mfumo wa jamii isiyo na dini wa Ufaransa unaweza kushutumiwa na wote, Waislamu na waliberali wa Magharibi, uzoefu wa nchi hiyo una mafunzo yenye thamani kwa ulimwenu mzima.

Ufaransa haijakumbwa na shambulio lolote kubwa la ugaidi tangu msukosuko wa mabomu katika miaka ya 1990 iliyohusiana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Aljeria. Na katika mwaka 2006 wakati taasisi ya Pew ilipokuwa inakusanya maoni juu ya silika au tabia za Waislamu, ufaransa ndiyo ilikuwa nchi pekee kubwa ya ulaya ambako Karibu nusu ya Waislamu wote walijihisi kuwa wananchi wa nchi hiyo kabla ya kuwa waumini wa dini yao. (Katika Ujerumani, uingereza na Hispania, kundi kubwa la walio wengi lilidai kuwa na utii kwa Uslamu kwanza.) Mwishowe, rekodi hii zaidi ya jambo jingine lolote itaiongoza sera ya katika suala hili nyeti.
Kupigwa marufuku burqa huko Ufaransa: mgongano wa kiutamaduni wafunuliwa

Kwa bahati nzuri ‘wabaguzi’ hawaungwi mkono na vyama vikuu vya siasa vya Australia. Hata hivyo, palikuwa na hofu hivi karibuni wakati Tony Abbott, kiongozi wa upinzani wa taifa, alipozua swali kuhusu haki za wachache na jamii za tamaduni tofauti kuishi pamoja.

Wahamiaji wangepata umaarufu zaidi ikiwa viongozi wa walio wachache wangewahamasisha kufuata maadili yaw alio wengi na kutii sheria, alisema.

“Jambo la chini kabisa lisiloepukika ambalo tunalisisitiza ni utii wa sheria,” alisema Bw. Abbott. “Lingesaidia kuimarisha kuungwa mkono kwa uhamiaji na kukubalika kwa utofauti wa jamii ikiwa viongozi zaidi wa walio wachache wangekuwa tayari kuwaonyesha heshima kwa maadili ya Waaustralia walio wengi kama vile wanavyotaka (maadili) yao yaheshimiwe.”
Tiini sheria, Abbott awaambia wahamiaji

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.