Urusi: Maandamano ya Kupinga Serikali Yaripotiwa na Wanablogu, Yasusiwa na Vyombo Vikuu vya Habari

Wanaandamanaji wasiopungua 7,000 walikusanyika kwenye mitaa ya Kaliningrad, mji ulio magharibi zaidi mwa nchi hiyo, Januari 30 ili kudaii, pamoja na mambo mengine, kujiuzulu kwa gavana wa mkoa Georgy Boos [ENG] na Waziri Mkuu wa Urusi Vladimir Putin. Lakini usivitegemee vyombo vya habari vya Urusi kukwambia hayo.

Idhaa kubwa na maarufu za televisheni zimekuwa kimya. Magazeti makubwa na vituo vya redio vimeyapuuza maandamano hayo na vinaendelea na shughuli zao kama vile hakuna kilichotokea. Lakini inakuchukua mtipitio mmoja tu katika posti maarufu kwenye RuNet (Mtandao wa Urusi) kutambua kuwa maandamano ya mjini Kaliningrad ni mada moto moto ya siku. Viongozi maarufu wa siasa, waandishi wa habari na watumiaji wa kawaida wa mtandao wa tarakilishi walifurika kwenye uwanja wa blogu wakiwa na mitazamo yao kuhusu maandamano hayo.

Boris Nemtsov (anayejulikana pia kama mtumiaji wa LJ b-nemtsov), Naibu Waziri wa zamani wa Urusi, aliandika posti yenye mguso wa pekee “Kaliningrad ni tumaini la Urusi iliyo huru” ambapo alisisitiza upekee wa maandamano hayo ya Kaliningrad [RUS]:

Такого грандиозного митинга я не видел лет так 10. На митинге четко и ясно были выдвинуты политические требования: отставка Путина и губернатора Бооса.
Исключительной особенностью калининградского феномена стало участие всех оппозиционных сил области в протестной акции.

Sijaona maandamano makubwa hivyo kwa miaka kumi iliyopita. Katika maandamamo, watu walieleza madai yao ya kisiasa: kujiuzulu kwa Putin na gavana Boos. Upekee wa dhana ya Kaliningrad ni ushirikishwaji wa makundi yote pinzani ya mkoa huo kwenye maandamano.

Mwanablogu alegmakarov aliongeza [RUS] kwamba, tofauti na ilivyokuwa zamani, vikosi vya polisi katika mji huo hata havikuthubutu kuwazuia watu kuandamana. Nemtson baadae alaizungumzia kuhusu urafiki usio wa kawaida wa polisi katika video fupi [RUS] iliyopigwa wakati akiwa kizuizini mjini Moscow mnamo Januari 31. Ilja Yashin (anayejulikana pia kama mtumiaji wa LJ yashin), mwanaharakati wa kisiasa na mwandishi wa makala kwenye gazeti la upinzani la Kirusi “Novaya Gazeta,” alieleza tabia ya kirafiki ya polisi:

Совершенно спокойно вела себя милиция. Никакой агрессии, четкое соблюдение законов, ОМОН мирно дремал в автозаках, припаркованных в стороне. Причина очевидна: когда на площади собирается больше десяти тысяч человек – милиция с народом. Потому что разогнать сто человек легко. А 12 тысяч сами кого хочешь разгонят, если понадобится.

Polisi walikuwa watulivu. Hapakuwa na matumizi ya nguvu, wakifuata sheria, Askari wa Kikosi cha Dharura walilala kwa amani kwenye magari makubwa yalikuwa yameegeshwa pembeni. Sababu ni wazi: wakati watu zaidi ya 10,000 wanapokusanyika kwa maandamano, polisi huungana nao. Kwa sababu ni rahisi kuwatawanya watu 100. Na watu 12,000 wanaweza kuwatawanya watu wowote kama watataka.

Mamia ya maoni kwenye blogu hizo yanazungumzia hisia za aina mbalimbali. Watu wengi wanaonekana kuamini kwamba maandamano hayo yatabadili hali katika nchi kuwa nzuri zaidi. Wanablogu wengi wanakubaliana na madai kwamba kitu kama hiki hakikufikirika miaka kadhaa iliyopita wakati umaarufu wa kukubalika wa Vladimir Putin ulikuwa juu. Watu wengi wanaona maandamano haya kama alama ya mabadiliko makubwa kwenye uwanda wa siasa za nchi hiyo.

Lakini si kila mmoja kwenye blogu ana matumaini. Nikolay Troitsky (a.p.k mtumiaji wa LJ _kutuzov), mchambuzi wa siasa wa Wakala wa Habari wa Urusi, hajasisimka [RUS] na matokeo ya maanadamano hayo:

Много народу вышло протестовать в Калининграде, немало недвольных выходили во Владивостоке, может выйти на улицы хоть весь Тамбов, Липецк, Петропавловск-Камчатский – всё это неважно.
Ничего не сдвинется и не изменится, пока на массовые акции протеста не начнут выходить в Москве. И не 9-12 тысяч, это чепуха, это мало, а хотя бы тысяч 50 для начала. Как это было в 1989-91 годах

Watu wengi walienda kuandamana mjini Kalininrad, watu wengi wasio na furaha walijitokeza katika Vladivostok, mji mzima wa Tambov, Lipetsk ana Petropavlosk-Kamchatsky wanaweza kwenda mitaani. Haya yote si ya muhimu. Hakuna kitakachosonga, na hakuna kitakachobadilika mpaka maandamano haya ya halaiki yatakapoanza kutokea Moscow. Na sio 9,000-12,000. Upuuzi. Ni kidogo sana. Angalau iwe 50,000 kwa kuanzia. Namna ile ile ilivyotokea mwaka 1989-1991.

Mtumiaji wa LJ clen_lj alimjibu Troitsky:

Большое начинается с малого. Пару лет тому назад трудно было представить выход десятка тысяч человек различных политических взглядов в том числе и под лозунгом отставки Путина.

Kila kikubwa huanza na kilicho kidogo. Miaka michache nyuma, ilikuwa vigumu kufikiri kwamba watu 10,000 wenye mitazamo tofauti ya kisiasa wangetoka mitaani wakipiga mbiu ya kujiuzulu kwa Putin.

Lakini Troitsky bado hajashawishika:

Так еще лет 10-15 будет начинаться с малого.

Itachukua miaka mingine 10-15 kwa kila kikubwa kuanza kutokea kwenye kidogo.

makala inayohusu kutokuwepo kwa uhabarishaji wa maandamano hayo pia zimeibuka kwenye uwanja wa blogu. Mwanablogu kt-withlove aliandika [RUS]:

Почему митинг с 10 000 человек освещен только в Lenta.ru ?
rian молчит vesti.ru молчит… Чувствуется цензурка то)))

Kwa nini maandamano yenye watu 10,000 yaarifiwe tu na Lenta.ru? RIAN [Wakala wa Habari Urusi] wako kimya. Vesti.ru [wavuti ya habari kwenye chaneli ya runinga Urusi] nao wako kimya. Mtu anaweza kuhisi kusiwa kwa habari hizo))).

Lakini inaonekana kama mgomo wa vyombokale vya habari wa kutokuripoti hauwezi kufananishwa na habari huria kwenye mtandao ambapo Warusi wanaweza kujizoesha kusema kwa uhuru. Lakini kama wanablogu wa Kirusi wanavyoendelea hatua kwa hatua kuchukua nafasi, swali ni je, itachukua muda gani kwa serikali kuanza kuzichukulia(blogu) kwa namna inavyovichukulia vyombokale vya habari.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.