Tangazo la Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010

Tunayo furaha kutangaza Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010! Mwaka huu mkutano wetu utafanyika mjini Santiago, Chile tarehe 6-7, 2010.

Tembelea tovuti ya Mkutano kwa habari zaidi juu ya malengo ya mkutano, programu ya matukio, maelekezo ya kujiandikisha na maelezo juu ya mji mchangamfu wa Santiago. Kati ya vivutio vya mkutano huo kitakuwa ni kutangazwa kwa washindi wa Tuzo Ya Kuvunja Mipaka, tuzo mpya iliyoundwa na Google pamoja na Global Voices ili kuenzi miradi ya kipekee katika wavuti iliyoanzishwa na watu au vikundi vinavyoonyesha ujasiri, ari na uwezo wa kutumia Intaneti ili kukuza uhuru wa kujieleza.

Katika siku na majuma machache yajayo tutakuwa tunaiamba programu, kwa kuongeza wajihi wa watoa mada, orodha ya wahudhuriaji na mengine mengi – na endelea kupitia pitia tovuti ili kusoma makala za blogu na maoni kutoka kwa washiriki wa mkutano na wengine, na ili kushiriki katika mazungumzo vile vile.

Pia unaweza kusambaza habari kuhusu Mkutano wa Global Voices kwa kubandika moja ya vibeji au tangazo kwenye blogu au tovuti yako.

Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010 umewezekana kutokana na msaada wa MacArthur Foundation, Google, Open Society Institute, Knight Foundation na Yahoo!.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.