Syria: Matembezi Kwenye Uwanja wa Blogu

Juma hili, bila utaratibu maalum, tutafanya ziara ya kutembea kwenye blogu mbalimbali, na mada anuai katika mchanganyiko wa tofauti kidogo na masoko holela ya Aleppo.

Kituo chetu cha kwanza kitakuwa kwenye Mwondoko wa Hanzala kwenda kwa Mungu, ambako anaandika kuhusu uamuzi wake wa kuacha kazi:

جرت العادة أن يحتفل أحدنا بعيد ميلاده بعيد الحب أو بعيد الشجرة حتى ، و لكني سأحتفل اليوم بمناسبة مرور عام على توظيفي في إحدى مؤسسات الدولة ، و أنا لن أوزع حلوى أو كاتو بل سأكتفي بهذه المقالة فحسب ، أكتب هذه الكلمات و إنه ليحز في نفسي كثيراً أن أكتبها ، لأن الواحد منا يركض طول العمر ليحصل على تلك الوظيفة و ينتهي بهم الأمر بعد عام كما هي حالي الآن أرفع كتاباً أطلب فيه إعفائي منها .

Kwa mazoea mtu anaweza akasherekea siku yake ya kuzaliwa, au Siku ya Wapendanao au hata siku ya Miti, lakini bado leo nitakuwa nikisherekea kumbukumbu ya mwaka mmoja ya ajira yangu kampuni ya umma. Sitatoa mishumaa au keki, makala haya yatatosha. Inaniuma sana kuandika maneno haya, kwa sababu mmoja wetu anagetumia maisha yake kuteseka kupata kazi hii, lakini wakiacha mwaka mmoja baadae, kama mimi sasa, nikiandika barua hii ya kuacha kazi.

Tunamwacha Hanzala akilalamikia unyanyasaji unaofanywa na sekta ya Umma ya Syria na uamuzi wake wa kuondoka, na kuiendea mada ndogo ya kufurahisha.

Kama ilivyo kila Ijumaa, uwanja wa blogu ulibarikiwa na toleo la simulizi shirikishi ya Sea Side inayoandikwa na Abufares na Mariyah. Katika Sehemu ya 29, utasoma:

Yasmina aliakaa kwenye kochi nyuma yangu. Dhahiri alikuwa na mvuto zaidi ya tabasamu ya kimapenzi. “Ah, Houssam. Uh mungu wangu, Houssam.” Hakuweza kuzuia machozi yake na kadri aliavyouliza moyo wake, nilijua nisingeweza kumwangusha. Ningepaswa tu kutumaini kuwa Youssef angenisamehe…siku moja.

“Tutaenda asubuhi, Yasmina. Nitakuwa hapa mapema. Sawa eh?” Nilisema kwa upole kama nilivyoweza.

Na kwenye mada ya mapenzi na Valentini, Untold Damascene Stories, blogu ya jarida la FW, linachapisha taarifa kuhusu kukua kwa u-biashara wa siku ya wapendanao kwenye mitaa ya Dameski:

Kwa Wasyria, ambao hawako salama dhidi ya mikono ya mfumo wa biashara, desturi za siku ya Valentino huanza mwezi mmoja kabla ya tarehe 14 Februari. Jamaa wanaanza kuwapigia rafiki zao kuwaomba fedha; Hakuna mtu anataka kuonekana hana fedha mbele ya rafiki wa kike kwenye siku ya wapendanao. Migahawa huanza matayarisho kwa kuweka mapambo na ofa maalumu “Kwa Familia Pekee,” “Hakuna kapera anaruhusiwa.” Maua ya waridi yauzwayo lira 50 ghafla kimiujiza yanaongezwa sifuri mwishoni na kuwa kueguka kuwa lira 500. Na mwishowe, makampuni ya simu huanza kuwatumia wateja wake meseji nyingi, kama vile: “Tuma ujumbe kwenda #### ikiwa na jina la mwenzi wako ili kushiriki ‘Mashindano ya Siku ya Wapendanao’ au ‘kuangalia kama mnafanana kihaiba.”

Siasa pia ni chakula kikuu katika mazungumzo yoyote, na blogu ya Syria Comment inatuletea taarifa za hivi karibuni na uchambuzi wake kutoka Syria na duniani kote, zikiwa na kichwa kinachofikirisha cha ‘Je, Washington imeamua kutilia mkazo suala la amani ya Syria na Waisraili?’:

Kwa kifupi, kurudi kwa balozi ni habari njema, lakini kuchezea mpango wa kutafuta amani ambao ni mrefu kimchakato na mfupi kiamani utakuwa mgumu kwa Syria, ambayo haina vyombo vya habari vyerevu kama ilivyonavyo Israili. Dameski bila shaka inahofia kwamba Mitchell atawataka Wasyria kukutana na Netanyahu bila masharti. Syria inaamini hii ni sawa na kurejesha mahusiano bila ya Waisraeli kulipia chochote.

Na mwishowe, tutakaa kitako na Syrian Foodie in London, na kumaliza ziara yetu kwa chakula kitamu cha Damascene, Ful Nabit:

Ful Nabit ni maharage yaliyochemshwa na chumvi na mdalasini. Muuzaji huwa na surufia kubwa lenye maharage lenye kupashwa moto taratibu. Maharage hupakuliwa katika bilauri au bakuli za kauri badala ya sahani za karatasi au za plasiti, ambazo mie huona zinaongeza mwonjo katika zoezi zima. Kwa kawaida unapata bilauri ya mchuzi na nusu ndimu kusindikiza mlo wako. Mchuzi huo huwa na chumvi, mdalasini na kamuo dogo la ndimu huufanya uwe mtamu (lakini si mzuri sana) kama kinywaji kinachoambatana na mlo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.