Habari kutoka Februari, 2010
Je, Ghana Ipo Tayari kwa Upigaji Kura wa Kwenye Mtandao?
Tukio la siku mbili lililoanza jana; linaratibiwa na Danquah Instite (DI), kituo cha kutafakari sera, utafiti na uchambuzi, kutengeneza jukwaa la kitaifa kwa washikadau kuongoza majadiliano kuhusu uwezekano wa uanzishwaji wa kuandikisha wapiga kura kwa njia za vipimo vya kibaiolojia na hatimaye mfumo wa upigaji kura kwa njia ya mtandao nchini Ghana.
Upinzani Waongezeka dhidi ya Mapendekezo ya Tanzania na Zambia katika Makubaliano ya CITES
Upinzani unaongezeka dhidi ya mapendekezo ya Zambia na Tanzania ya kuruhusiwa na Makubaliano ya Biashara ya Kimataifa ya Makundi ya Mimea na Wanyama Walio Katika Hatari ya Kutoweka (CITES), kuuza hifadhi ya pembe za ndovu walizonazo.
Ghana: Mapendekezo ya Kuvutia Kwenye Mapitio ya Katiba
Mwaka 2008, wakati wa Uchaguzi wa rais, wagombea waliwaahidi Waghana kuwa wangeitazama tena katiba ya nchi hiyo. Jambo lililoifanya ahadi hii kuonekana kama ni ya kweli lilikuwa ni nia ya wagombea – pamoja na Rais John Atta Mills – ya kuwashirikisha Waghana katika mchakato huo wa kuitathmini katiba. Inaonekana kuwa rais ametimiza ahadi hiyo, na sasa mapendekezo mapya yanachochea mijadala ya kuvutia.
India: Ugaidi Waikumba Pune
Mnamo majira ya saa 1:30 jioni (Februari 13, 2010) mlipuko wa bomuuliua watu 9 na kuwajeruhi wengine 57 katika mgahawa maarufu kwa watalii uliopo katika mji wa Magharibi wa Pune, India. Hisia ziko juu huku wanablogu na watumiaji wa twita wakitoa maoni.
Malaysia: Harakati za Kutovaa Nguo za Ndani Wakati Wa Siku ya Valentino
Wanafunzi kadhaa wa kike nchini Malaysia wanahamasisha "harakati za kutovaa nguo za ndani" katika siku ya Valentino. Kampeni hiyo imepata umaarufu mno kupitia ujumbe wa mtu kwa mtu na kwa kupitia intaneti. mamlaka za kidini hazijafurahishwa. Wanablogu wanatoa maoni.
China: Yatishiwa na Zuio la Mtandao Lililofanywa na Marekani
Maoni kutoka kwa watengeneza programu wa Kichina kuhusu uamuzi wa SourceForge.net wa kufuata sheria za Marekani na kuzuia watumiaji kutoka nchi kadhaa yanajumisha mapendekezo ya jinsi ya kuuzunguka uamuzi huo wa marekani kwenye wavuti wa dunia.
Syria: Matembezi Kwenye Uwanja wa Blogu
Juma hili, bila utaratibu maalum, Yazan Badran anafanya matembezi kwenye blogu mbalimbali, na mada anuai katika mchanganyiko wa tofauti kidogo na masoko holela ya Aleppo.
Misri: Sisi Ni Washindi
Timu ya kandanda ya Misri iliifunga Ghana katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na ikapata ushindi wake kwa mara ya tatu mfululizo. Huu pia ni ushindi wa saba tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo kwenye miaka ya hamsini. Wanablogu wanaungana na wananchi wa nchi hiyo kusherehekea mafanikio hayo.
Costa Rica: Video za Mtandaoni Zaongeza Vichekesho Katika Uchaguzi wa Rais
Uchaguzi wa Rais wa Costa Rica unafanyika Jumapili hii na kwa kupitia video, wananchi wengi wa Costa Rica wanatoa hisia zao kuhusu wagombea na mustakabali wa nchi yao kupitia vichekesho na utani.
Urusi: Maandamano ya Kupinga Serikali Yaripotiwa na Wanablogu, Yasusiwa na Vyombo Vikuu vya Habari

Wakati maandamano makubwa zaidi dhidi ya serikali nchini Urusi katika muongo uliopita yanazidi kudharauliwa na vyombo vikuu vya habari nchini humo, ulimwengu wa blogu unachemka na makala kadhaa juu ya maandamano hayo na athari zinazoweza kutokea.