Malaysia: Harakati za Kutovaa Nguo za Ndani Wakati Wa Siku ya Valentino

Wiki mbili zilizopita, wanafunzi kadhaa wa kike nchini Malysia walitangaza “mwamko wa harakati za wasiovaa nguo za ndani” wakati wa siku ya Valentino. Lengo la “kutangazwa kwa wasiovaa nguo za ndani” ni kuonyesha jinsi ambavyo wanawake wanavyowapenda marafiki zao wa kiume. Kampeni hiyo ilifikia umaarufu kwa kupitia ujumbe wa mdomo pamoja na intaneti.

lurveangel anapingana na kampeni hiyo:

Hawajaelimika sana hawa, au? Kama wameelimika, inawapasa wajue tu kuwa kutokuvaa nguo za ndani hakuthibitishi mapenzi ya kweli, sawa? Ni hamu ya ngono tu – bila ya shaka ni jambo la kuvutia kiaina unapojua kuwa mpenzi wako hajavaa kitu chochote ndani, lakini kwa nini ulifanye (jambo hilo) kuwa wazi kwa umma mzima?? Wana tatizo gani watu hawa??!!

Mapenzi ya kweli hayahusu kwamba mtu amejisitiri kila inchi au yu uchi wa mnyama wakati akiwa na mpenzi wake. Watu wanaochanganya mambo haya bila hakika hawajawahi kuwa katika mapenzi, au kupendwa. Au hata kujua maana ya “mapenzi ya kweli”.

Idara ya Masuala ya Kiislamu ya Selangor (JAIS) na mamlaka nyingine za maadili ya umma vimekasirika sana. Wameahidi kuwasaka wale watakaojiunga na harakati hizo za kutovaa nguo za ndani kwa kuwa kusherehekea siku ya Valentino ni kinyume na mafundisho ya Kiislamu.

Ms Daffodil anazishutumu mamlaka hizo kwa kulichukulia swala hilo katika uzito mkubwa kuliko linavyostahili:

OK…. Dhahiri ni upumbavu mkubwa kutembea bila nguo za ndani ili kuonyesha mapenzi yako kwa mtu fulani…….. na yule aliyefikiria uchafu huu inawezekana kabisa akawa ni amfibia mwenye ukame anayejificha nyuma ya manyasi karibu na ngazi za umeme akiwa na kioo au simu yenye kamera…

Lakini kwa polisi wetu wa maadili kurukia na kutoa onyo kuhusu ubaya wa Siku ya Valentino!!!??? Huku ndio “kulichukulia swala katika uzito mkubwa kuliko linavyostahili” … Yaani, fikiria kwa dakika hapa… kama wakitaka, wanaweza kwenda bila ya nguo za ndani siku yoyote, au sio?

Josh anasisitiza kuwa kutovaa nguo za ndani hakutakuwa tatizo kwa wengine

Hebu nikuulize swali moja, kwa jinsi gani mtu asipovaa nguo za ndani aanweza kukuathiri wewe kama mtu. Je unaweza hata kugundua? Je unaweza hata kujua? Unawezaje kujua kuwa watu uliokutana nao mitaani leo kuwa wamevaa nguo za ndani? Hivyo zogo la nini wakati kuna uwezekano kuwa hauwezi kutambua ikiwa mtu amevaa nguo za ndani na hivyo hauwezi kuathirika na jambo hilo. Kwa kuanzia, hili suala halina uzito. Kitu watu wanachhovaa nguoni ni masuala yao wenyewe na hayatuhusu.


Mumsie
anajiuliza kwa jinsi gani mamlaka zinaweza kuwatambua wanafunzi wasiovaa nguo za ndani. Je watapandisha sketi za wanafunzi juu?

Ama kweli, hili ni jambo jipya na ninajiuliza ni vipi hapa duniani JAIS itaweza kuzuia jambo kutokea?!.. je watawasaka hawa wanafunzi “wasio na nguo za ndani” kwa kuchungulia chini ya kila sketi?!! Hilo litakuwa kosa la wazi la kijinsia, au siyo? Naweza kuona kuwa kila mwanafunzi wa kiume siku hiyo atakuwa anaweka dau na kuhisi ni mwanafunzi yupi wa kike ambaye hajavaa nguo za ndani!…;-)

Malaysia Nyingine inatambua upekee wa kitendo hicho:

1. Maandalizi ya ‘tukio’ hili yalikuwa ya kujitokeza bila kupangwa na yaliyojineemesha yenyewe, hayakuchochewa na chama chochote cha siasa au mwanasiasa maarufu;

2. Njia za maandalizi ya tukio hili zilitengenezwa kwa kutumia ujumbe wa mdomo na intaneti, kunakoashiria umuhimu unaojitokeza wa intaneti, jumbe za maandishi na namna nyingine za miundombinu ya mawasiliano ambazo zilisimikwa kama sehemu ya maendeleo ya haraka nchini Malaysia kelekea kuwa uchumi wa viwanda.

3. Asili ya maadhimisho/upinzani huo hata hivyo inabakia kuwa si ya kisiasa nay a kibinafsi, kwani iliazimia kuwa namna ya kuonyesha mapenzi ya mmoja kwa mwenzake.

Je harakati za kutovaa nguo za ndani ni ‘upinzani bubu’?

… unaweza kuwa upinzani bubu dhidi ya nafasi ya ukiritimba wa kidini ambayo katika kuichunga jamii kimaadili imetokea kujulikana sana na kuwa korofi. (Kumbuka kuwa hii ni nadharia tu kwa upande wetu)

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.