Ghana: Mapendekezo ya Kuvutia Kwenye Mapitio ya Katiba

Mwaka 2008, wakati wa Uchaguzi wa rais, wagombea waliwaahidi Waghana kuwa wangeitazama tena katiba ya nchi hiyo. Jambo lililoifanya ahadi hii kuonekana kama ni ya kweli lilikuwa ni nia ya wagombea – pamoja na Rais John Atta Mills – ya kuwashirikisha Waghana katika mchakato huo wa kuitathmini katiba. Inaonekana kuwa rais ametimiza ahadi hiyo, na sasa mapendekezo mapya yanachochea mijadala ya kuvutia.

Katika makala iliyotumwa na Ghana Pundit yenye kichwa kinachosema, “Msiongeze Muda Wa Rais Madarakani,” Prof. Kofi Quashigah, Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Cha Ghana, anasema:

Mfumo wa mihula miwili ya miaka minne minne ni mrefu wa kutosha kumwezesha mtu mwenye nia kama akiwa rais kuacha msukumo wake katika vyombo vya demokrasi. Mfumo wa mihula miwili ya miaka mitano mitano utakuwa ni mwanzo wa kutengeneza miungu wa bati. Ni uimarishaji wa taasisi za utawala ambao unapaswa kuzikamata fikra zetu ili kwamba watu binafsi wasiweze kuwa wa muhimu zaidi… kipindi cha miaka minne kinaonekana kuwa kinatosha tu ili kuepusha mtu kukaa kwa muda mrefu na kuanza kuridhika.

Maoni haya yanatokana na moja ya mapendekezo ya marekebisho ya katiba yanayotazamwa na Kamati ya Kuipitia Katiba ya Ghana: kuongeza muhula wa sasa wa urais kutoka miaka minne kwenda miaka mitano.

Quashigah anaongeza:

Mfumo unapaswa kudumishwa ili kuepuka kuundwa kwa hali ya kutegemewa katika watu ambao wanakuwa marais.

Na je Rais Atta Mills anaendeleaje na ahadi yake ya kuwahusisha watu katika mchakato wa huu kuitazama katiba?
Je Waghana wamelipokeaje wazo hilo?

Ghana Pundit anaripoti katika makala yake ya Februari 11:

Kuna mwanasheria aliyependekeza kwamba maopitio ya katiba ni lazima yahakikishe kwamba madaraka yanabaki katika mikono ya wananchi kwa kupitia taasisi na vyombo vyenye miundo mizuri na mfumo mzuri kabisa wa mabunge ya majimbo.

Mwanasheria, Nana Addo-Aikens, anaendelea:

Marekebisho ya katiba, ambayo Ghana inayahitaji leo, hayapaswi kuwa ya juu ya uso au ya urembo au ya fahari ya macho bali yanatakiwa kuwa katika namna ya katiba, ambayo itakumbatia yote na itakayofikia kila nyanja ili kwamba yasipoteze fursa hii ya nadra ya mabadiliko.

Kisha anaongeza:

Mfumo wa vizingiti na mizani unaofanya kazi sawa pamoja na miundo fanisi ya utanganishaji wa madaraka ni masuala kadhaa ambayo yanahitaji kutazamwa kwa makini na tume hii.

Katika makala kuhusu marekebisho ya katiba katika tovuti ya shirika la Habari la IPS, Osabutey Anny anamnukuu mwanasheria na katibu mtendaji wa tume hiyo, Dkt. Raymond Atuguba,, akisema:

Kila pendekezo litakalowekwa mbele ya tume litachunguzwa vizuri. Mapendekezo yaliyotolewa ni ya maana.

Anny anaripoti:

Mapendekezo yaliyopokewa mpaka hivi sasa ni mengi na yanajumuisha tathmini ya nguvu za serikali.

Kwa mujibu wa Anny, Atuguba alidai kuwa,

Idadi ya mapendekezo yaliyopokelewa na tume yanaonyesha upeo ambao umma unasuburi matokeo

Kutokana na ripoti ni wazi kuwa Waghana wapo tayari kujihusisha katika mchakato unaokua wa demokrasi wa taifa hili tangu katiba yake ilipoanza mwaka 1993.

Anny analisifia taifa hili la Afrika katika makala yake:

Nchi hii imepiga hatua kubwa tangu wakati huo. Ghana ilikuwa ni nchi bora ya saba katika bara katika utawala bora kwa mujibu wa orodha ya Ibrahim ya Utawala wa Afrika 2009. Orodha hiyo ilipima, pamoja na mambo mengine, utoaji vifaa na huduma za jamii unaofanywa na serikali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.