Januari, 2010

Habari kutoka Januari, 2010

Togo Yaondolewa Kwenye Mashindano ya Kombe la Afrika baada ya Shambulizi Baya

Timu ya Taifa ya Togo sasa imeondolewa rasmi kutoka kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia shambulizi lililoelekezwa kwa msafara wa timu hiyo Ijumaa iliyopita katika eneo la Kabinda lililo nchini Angola na ambalo liko kwenye ukanda wa mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi wanaotaka kujitenga. Huku kukiwa na shutuma nyingi kutoka kwenye serikali ya Angola na maafisa wanaosimamia soka barani Afrika, wanablogu wa Ki-Togo wanauliza maswali magumu kuhusu msiba huo.

Misri: Mauaji ya Kinyama ya Naga Hammady

Wanablogu wa Misri wanaelezea kustuka kwao na hasira kwa kuuwawa kwa Wakristu wa dhehebu la Koptiki wakati wa mkesha wa sikukuu yao ya krismasi huko Naga hammady, katika Misri ya Juu. Mhalifu asiyejulikana alipiga risasi hovyo hovyo kwenye umati watu baada ya waumini kumaliza maombi na wakiwa wanaelekea majumbani kwao.

Thailand: “Tumechoshwa na Wizara ya Utamaduni”

  12 Januari 2010

Ukurasa wa wapenzi wa Facebook umezinduliwa na raia wa mtandaoni wanaokosa njia na sera za Wizara ya Utamaduni ya Thailand. Wizara hiyo imekuwa ikidhibiti sana uhamasishaji na usimamizi wa utamaduni wa asili wa Ki-Thai katika tovuti za vyombo vya habari vya kizamani na hata vile vya kisasa.

Georgia: Hebu Tuongelee Tendo la Ngono…

  9 Januari 2010

Pengine mada iliyotawala katika vyombo vya uanahabari wa kijamii vya Georgia haikuwa siasa, uchaguzi, matatizo, matetemeko ya ardhi au majanga. Badala yake, mada iliyojadiliwa sana ilikuwa inahusu kipindi kipya cha televisheni, Ghame Shorenastan. Kinachoonyeshwa kwenye Imedi TV, jina la kipindi hicho linatafsirika kama Usiku pamoja na Shorena na kinaongelea mada zinazohusu tendo la ngono.

Msumbiji: Kifo Cha Mradi Mkubwa wa Mazao Nishati

Mwishoni mwa mwezi Disemba, Baraza la Mawaziri la Msumbiji lilitoa tamko muhimu. Kibali cha kutumia Hekta 30,000 za ardhi kwa kampuni ya mazao nishati (biofuels) Procana, kimebatilishwa. Shauri la Mradi wa Procana, ulipo kwenye eneo kubwa linalopakana na Mbuga ya Taifa ya Limpopo ambayo imetanda mpaka nje mpaka wa nchi, lilikuwa na utata pamoja na mvutano mkubwa tangu (shauri hilo) lilipoanza mwanzoni mwa mwaka 2007.

Australia: Mauaji ya Mhindi Yazua Mzozo

  9 Januari 2010

Mauaji ya mtu mwenye asili ya India mjini Melbourne yamewasha tena mjadala kuhusu ubaguzi wa rangi nchini Australia na usalama wa wanafunzi kutoka ng’ambo. Kadhalika yameathiri uhusiano kati ya Australia na India. Mwandishi wa GV Kevin Rennie anakusanya maoni ya wanablogu wa Australia.