Mwishoni mwa Mwezi Disemba, Baraza la Mawaziri la Msumbiji lilitoa tamko muhimu. Kibali cha kutumia Hekta 30,000 za ardhi kwa kampuni ya mazao nishati (biofuels) Procana, kimebatilishwa.
Sheria ya Ardhi ya Msumbiji iliyopitishwa katika 1997, ni ya kipekee. Ardhi ilitaifishwa wakati wa uhuru, na Sheria ya Ardhi haikubadilisha jambo hilo. Inaipa serikali zana wazi kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya ardhi. Wawekezaji wa sekta binafsi wanalazimika kuomba mkataba wa kutumia ardhi kwa miaka 50, ambao unajulikana kama DUAT, au “Haki ya Kutumia Ardhi na Manufaa Yake”. Mikataba hiyo ya DUAT haina nguvu kwa muda wote wa miaka 50 mpaka pale kipindi cha kwanza cha miaka miwili kitakapopita, wakati wawekezaji wanapopaswa kuthibitisha kuwa wanaitumia ardhi hiyo kuzalisha.
Shauri la Mradi wa Procana, ulipo kwenye eneo kubwa linalopakana na Mbuga ya Taifa ya Limpopo ambayo imetanda mpaka nje mpaka wa nchi, lilikuwa na utata pamoja na mvutano mkubwa tangu (shauri hilo) lilipoanza mwanzoni mwa mwaka 2007. Jamii zilikuwa zihamishwe kutoka kwenye eneo la mbuga kwenda kwenye eneo ambalo kabla ya hapo lilikuwa limetolewa kwa Procana kwa ajili ya kuzalisha miwa. Jamii hizi ziliitaji ardhi kwa ajili ya kulisha mifugo, kwani jamii hizo hujikimu kutokana na ufugaji wa ng’ombe. Inaonekana kuwa hapakuwa na mipango yoyote ya kukabiliana na mgogoro ambao ulikuwa unatokota. Na zaidi ya hilo, kulikuwa na hofu kuwa mahitaji ya maji ya Procana yangetibua uzalishaji wa chakula wa sehemu hiyo. Vikundi vya Jamii za Kiraia viliziunga mkono jamii katika majadiliano yao na maofisa wa Mbuga kwa kupitia mradi unaoitwa Lhuvuka, lakini inaonekana kuwa hapakutokea maendeleo yoyote kati yao na Procana.

Picha ya shule ya Massingir iliyopigwa na Ralph Pina, na kuchapishwa kwa idhini ya Creative Commons
Tovuti ya Lhuvuka ina makala ambayo imekusanya madai kati katika mgogoro huo [pt]
[…] na ausência de uma decisão firme por parte do governo face ao processo de reassentamento das comunidades vivendo no PNL; politização do processo de reassentamento das comunidades vivendo no PNL, sem respeitar todos seus direitos e interesses; uso abusivo da força por parte dos investidores, não respeitando os direitos básicos das comunidades previstos nas legislações moçambicanas por saberem que por detrás deles há sempre pelo menos um membro do governo que os protege e predominância de gestores mais virados para “yes mans” por temerem perder os cargos que actualmente ocupam.
.

Picha ya miwa na Denn, iliyochapishwa kwa idhini ya Creative Commons
Tovuti ya Ki-Brazili “Reporter Brasil”, ambayo inatilia makini athari za mazao nishati kijamii na kimazingira, ilichapisha makala mwanzoni mwa mwezi Disemba ambayo ilitamka [pt]
Cerca de 30 mil hectares de savana nativa deve rão ser convertidos em canaviais em Massingir, a região mais seca do país africano, provocando perda de biodiversidade e consumo excessivo de água (aproximadamente 409 bilhões de litros por ano para irrigação). E 38 mil moradores do entorno do Parque Nacional do Limpopo serão obrigados a deixar suas terras.
A Constituição de Moçambique decreta que todas as terras do país são propriedade do Estado, que pode conceder autorização de uso a empresas por períodos de 50 anos. Essa concessão, no entanto, está condicionada à ausência de comunidades tradicionais no território. Pelo jeito, lá, como no Brasil, boas leis não são garantia de boas práticas.
Katiba ya Msumbiji inasema kuwa ardhi yote nchini ni mali ya taifa, ambalo linaweza kutoa kibali cha matumizi kwa makampuni kwa kipindi cha miaka 50. Kibali hiki hata hivyo, kinategemea kutokuwepo kwa jamii asili katika eneo. Hii in maana, pale (Msumbiji), kama ilivyo Brazil, sheria nzuri hazihakikishi utekelezaji mzuri.
(Jarida la Reporter Brasil linaivulia kofia makala katika jarida la Mother Jones la mwezi Machi 2009 kuhusu Procana.)
Mwanablogu wa Msumbiji anayeandika sana Carlos Serra alichapisha habari ya Procana tangu mwanzo mnamo mwisho wa 2007. Awali nusu ya Kampuni hiyo ilikuwa inamilikiwa na Kampuni ya kimataifa CAMEC, inayojulikana kama kampuni ya migodi/uchimbaji. Waanzilishi wa CAMEC wanajulikana kwa mikataba yao kwenye nchi zenye matatizo kama vile Sudani Kusini, DRC, na Zimbabwe. Serra aliandika miaka miwili iliyopita:
Mas convinha – este é um recado especial para o ministro da Agricultura, Erasmo Muhate -, também, estudar a trajectória de Phil Edmonds, chairman da CAMEC.
Serra kwa mara nyingine alidhihirisha umuhimu wake kama mchambuzi wa siasa na uchumi wakati alipoonekana kuonya mwanzoni mwa mwezi Disemba 2009 kuwa serikali imeigeuka Procana.
Baadhi ya habari katika wavuti zinadai kuwa wawekezaji wakuu ndani ya Procana walipoteza imani katika kampuni mwanzoni mwa 2009. Serikali ilibatilisha rasmi kibali cha ardhi kutokana “kutokuwa na uzalishaji” – wamesafisha Hekta 800 tu za jumla ya Hekta 30,000 katika miaka miwili ya kwanza ya uendeshaji, na kushindwa katika kutengeneza ajira. Kama ilivyo katika mkataba wowote wa ukubwa wa kiasi hiki – mwanzoni ulikadiriwa kuzidi Dola za Kimarekani Milioni 500 – tunaweza kusema kuwa kulikuwa na masuala lukuki ya kisiasa na kiuchumi katika mchezo.
Katika tathmini yake ya hali ya kiuchumi ya Msumbiji, mwanablogu Basilio Muhate aligundua kuwa shauri la Procana lilikuwa la kipekee [pt]
[…] as medidas de política económica levadas à cabo para fazer face as crises alimentar e financeira recentes, que incluiram subsídios aos pequenos agricultores e instalação de silos, os projectos da área de biocombustíveis iniciados em 2008 (A PROCANA foi uma excepção na medida em que pouco ou nada alcancou em relação às previsões), estão a ter impactos positivos no sector da agricultura
Ni vigumu kubaini kama kisa cha Procana kinawakilisha mfano mpya wa udhibiti wa ardhi nchini – kama serikali ya Msumbiji itachunguza idadi inayoongezeka kila wakati ya mikataba ya ardhi na wawekezaji wa nje katika namna hii hii. Au kama kisa hiki kinawakilisha tu tukio la kipekee – na utendaji mbaya wa kipekee kwa upande wa wawekezaji wa nje. Au vyote.
Mwandishi anapenda kueleza kuwa: anafanya kazi kwa shirika la maendeleo la kimataifa ambalo lilidhamini kazi ya Lhuvuka, lakini hajafanya kazi moja kwa moja katika mradi huo. Anaandika kwa ajili ya Global Voices kwa kujitolea na katika nafasi binafsi.