- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: wanablogu Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutembelea kwao Naha Hammady

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Dini, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala

Zaidi ya wanablogu 20 wa Misri wametiwa mbaroni mara baada ya gari moshi walilokuwa wakisafiria kuwasili katika kijiji cha Naga Hammady [1] huko Misri ya Juu. Walikuwa wakiongozwa na Dkt. Mostafa Al Naggar [2]. Wanablogu hao waliotoka Cairo, Alexandria na miji mingine ili kwenda kutoa heshima zao kwa familia za watu waliouwawa katika mauaji ya Naga Hammady [3]. Wakristo 7 wa madhehebu ya Kikopti walipigwa risasi katika mkesha wa sikukuu ya Krismas ya Kikopti mnamo Januari 7 mwaka huu. Wengine wengi walijeruhiwa. Shambulio hilo lilifanyika wakati Wakristo hao walipokuwa wakitoka kanisani mara baada ya misa ya Krismas.

Dkt. Mostafa Al Naggar [2] aliandika katika blogu yake:

ابتلانا الله بنظام قمعي متسلط ، أفسد حياتنا ووئامنا ، سرق منا الأحلام وجعلنا نعاني جميعا من بطالة وخوف وحرمان ، بعد أن كانت بلدنا هي نبع الأمان اذا بها تتحول علي يديهم الي أرض الخوف ، لا نأمن علي أنفسنا في بيوتنا فزوار الفجر قد يخطفوننا من مخادعنا ، لا نأمن علي أنفسنا في شوارعنا فقطاع الطريق قد يسرقوننا ويعتدون علي نسائنا والقتلة المأجورين قد يقتلوننا ونحن خارجين لتونا من صلواتنا

Tulilaaniwa na utawala wa mfumo unaokandamiza ulioyaharibu maisha na utengemao wetu. Tuliporwa ndoto yetu na kuachwa tukihangaika bila ajira, tukiwa wenye hofu, na tulionyang'anywa kila kitu. Misri ambayo kuna kipindi ilikuwa mbingu salama iligeuzwa kuwa dampo. Hatuko salama tena majumbani mwetu maana wageni waliovalia sare maalumu wanaweza kwa urahisi kabisa kufika na kutunyakua kutoka kwenye nyumba zetu mara kiza kinapoingia. Hatuko tena salama mitaani maana wahuni na wahalifu wanaweza kutukamata na kuwanyanyasa wanawake wetu. Leo tumeshuhudia jinsi wauwaji wanavyoweza kutupiga risasi kirahisi wakati tunamaliza sala zetu.

Ujio usio wa kisiasa wa wanablogu hao katika kijiji cha Naga Hammady ulizuiwa wakati wanablogu hao walipotelemka kutoka kwenye gari moshi. Kareem El Beheiry aliandika [4]:

القاهرة الساعة 9.30 صباحا
قامت قوات الامن بنجع حمادى صباح اليوم بالقبض على عدد من النشطاء التابعيين لعدد من الحركات والاحزاب السياسية اثناء توجهم من القاهرة الى نجع حمادى فور خروجهم من القطار لعقد مؤتمر لأدانة احداث نجع حمادى والتأكيد على الوحدة الوطنية
يذكر انه بعد القبض عليهم قامت قوات الامن بالحصول على بطاقتهم الشخصية والموبايلات الخاصة بهم ثم وضعتهم داخل سيارة ترحيلات ثم تبع ذلك تقسيمهم على سيارات متعددة واخذهم الى اماكن مجهولة حتى الان لم يتم معرفة وجهتهم

Cairo, saa 3:30 asubuhi – polisi wa kijiji cha Naga Hammady wamewatia mbaroni wanablogu na wanaharakati kutoka katika vyamba mbalimbali vya kisiasa na vuguvugu mara tu walipowasili kutoka Cairo kwenda kijiji cha Naga Hammady. Lengo la safari yao hiyo ilikuwa kwenda kuwapa mkono wa pole wanafamilia waliopoteza ndugu zao na kuchukua hatua ya kupinga migogoro inayohusishwa na dini. Kufuatia kukamatwa kwao, maofisa wa polisi waliwanyang'anya vitambulisho vyao na simu zao za mkononi na kuwachukua katika magari tofautitofauti na kwenda kusikojulikana.

Hii hapa ni orodha ya wanablogu wanaohisiwa kukamatwa:

1 – اسراء عبد الفتاح
2– وائل عباس مدونة الوعى المصرى

3- باسم سمير حزب الغد والمعهد المصرى الديمقراطى

4- باسم فتحى المعهد المصرى الديمقراطى

5- احمد بدوى شباب 6 ابريل

6– شريف عبد العزيز

7- ماريان ناجى رويترز

8- مصطفى النجار مدونة أمواج

9- رؤى ابراهيم طالبة فى الجامعة الامريكية

10- شاهيناز عبد السلام مدونة واحدة مصرية

11- ناصر عبد الحميد حزب الجبهة

12-محمد خالد مدونة دماغ

13- شريف عبد العزيز

14- أميرة الطحاوى

15-سمر عقل حزب الجبهة

16- أحمد أبو ذكرى

17- اسماعيل الاسكندرانى

18- حنان

19- أحمد فتحى البدرى حزب الكرامة بقنا والذى كان يستقبل الوفد

20- ناشطة فرنسية لم نستدل على اسمها

1- Esraa Abdel Fattah [5]
2- Wael Abbas [6]
3- Bassem Samir
4- Bassem Fathy
5- Ahmed Badawy [7]
6- Sherif Abdel Aziz [8]
7- Marian Nagy [9]
8- Mostapha Al Naggar [2]
9- Ro'a Ibrahim
10- Shahinaz Abdel Salam [10]
11- Nasser Abdel Hamid
12- Mohamed Khaled [11]
13- Sherif Abdel Aziz [8]
14- Amira Al Tahawy [12]
15- Samar Akl
16- Ahmed Abou Zekri
17- Ismail Al Askandarani [13]
18- Hanan
19- Ahmed Fathi Al Badry
20- Mwanaharakati wa Kifaransa ambaye hajatambulika bado.

Zeinobia alitoa maoni akisema [14]:

Wengi kama sio wote miongoni mwa wanablogu hawa ni kati ya waandishi wa habari wa kiraia walio maarfu zaidi. Sielewi kwa nini wanablogu hawa wametiwa mbaroni.