Mahojiano ya video [en] ya Kyo Kageura, mkuu wa mradi wa Minna no Honyaku (みんなの翻訳, Tafsiri kwa Wote) [ja], jukwaa jipya la tafsiri ambalo linazisaidia Asasi Zisizo za Kiserikali na zile Zisizo za Kibiashara kueneza ujumbe wao, shukrani kwa wafasiri wa kujitolea.
Global Voices Japan ilimuuliza kuhusu changamoto za Minna no Honyaku [en], matatizo na nyanja mpya ya kutafsiri kwa kujitolea.
Mradi wa Minna no Honyaku au Tafsiri kwa Wote ni matokeo ya wazo la Kundi la Kutafsiri la Maktaba na Chuo Cha Taifa cha Habari na Teknolojia ya Mawasiliano pamoja na Maabara ya Sayansi ya Habari ya Chuo Kikuu cha Tokyo, kwa kushirikiana na shirika la Uchapishaji la Sanseido.
Ulibuniwa kama sehemu ya Mradi wa Shiitake, na kukamilika kwa jukwaa la kutia nguvu ukuaji wa tafsiri katika wavuti una dhamira maalum:
Mfumo huu hatimaye utawawezesha wafasiri binafsi kujenga mtandao, bila ya jitihada nyingine za ziada, ambapo wafasiri wanaofanya kazi katika sehemu moja au sehemu zinazofanana wanaweza kukusanya kwa pamoja takwimu za tafsiri na kushirikiana habari zenye umuhimu kwa kazi zao. Hili, tunaamini, litaboresha shughuli za wafasiri na kuwapa moyo wale wanaotaka kuwa wafasiri kujiunga. Kwa hiyo, mradi wa Shiitake ni mradi wa kijamii.
Na mwisho, huku kukiwa na lengo la kurahisisha kutafsiri hata kwa wafasiri wasio na uzoefu, timu ya Profesa Kageura iliunda Minna no Honyaku, kwa kushawishika kuwa:
Tafsiri za habari na taarifa za wale wanaojitolea zinatoa huduma muhimu sana katika huu mtiririko mbadala wa habari.