- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Haiti: Maoni ya Mwanzo Kuhusu Tetemeko la Ardhi Lenye Ukubwa wa 7.0

Mada za Habari: Marekani ya Kaskazini, Nchi za Caribiani, Haiti, Marekani, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Majanga, Uhamiaji na Uhamaji

Posti ya kwanza ya blogu iliyoandikwa kwa lugha ya Kifaransa kuhusu tetemeko la ardhi huko Haiti imetokea nje ya nchi hiyo, ikitangaza habari mbaya za kuanguka kwa Kasri ya Rais [1], hospitali [2] na majengo mengine na pia tishio la tsunami [3]. Kwa mujibu wa MetropoleHaiti [4], Marekani tayari imekwishapendekeza misaada ya kibinadamu.