- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Colombia: Ugumu wa Kutofautisha Wazuri na Wabaya

Mada za Habari: Amerika Kusini, Colombia, Filamu, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Vita na Migogoro

Kamera yangu na Marcin Wichary

Kamera yangu na Marcin Wichary


Kwa kupitia upigaji video wa kiraia, asasi tofauti nchini Colombia zinatoa mitazamo yao kuhusu uhalifu, unyama na migogoro inayohusisha matumizi ya silaha, ambayo ni vigumu kuwatofautisha watu wazuri kutoka kwa wabaya.

Kwanza, mama wazazi na wanafamilia wanajitokeza ili kuandamana [1] dhidi ya hali ya wanajeshi kuwa juu ya sheria katika vifo vya vijana wa kiume [2] kutokana na kile kinachoitwa Ushahidi wa Uongo. Katika kisa cha hivi karibuni kabisa cha Ushahidi wa Uongo [3], inaonekana kuwa wanajeshi waliwashawishi vijana wafuatane nao kutokana na ahadi za kazi sehemu za vijijini ambapo (vijana hao) waliuwawa na kutambuliwa kama wanajeshi wa upinzani ambao waliuwawa katika shambulio. Hata hivyo wanajeshi 17 walioshtakiwa [4] waliachiwa baada ya mstari mfu wa kufika mahakamani kutotimizwa.

Kundi la pili ni lile la jamii ya wazawa ya Nasa [5], ambao kwa kupitia idhaa yao ya YouTube [6] wanapata fursa ya kusimulia upande wao wa habari ambao kwa kawaida vyombo vya habari huukwepa. Katika kesi hii, mabomu ya ardhini, makasha ya makombora na silaha nyingine zimechwa kwenye makazi yao, ambayo yapo katikati ya eneo linalogombewa na makundi yenye silaha ya kisheria na yale yaliyo kinyume cha sheria. Inayabidi majeshi ya usalama ya wazawa hao “kufagia” eneo hilo, pamoja na nyumba, ili kuondoa silaha hizo zilizoachwa na wote, jeshi la taifa na yale ya upinzani. Katika video, wanayataka majeshi yaache kuweka mabomu ya ardhini na angalau waje na kuyachukua yale ambayo hayakulipuka kabla ya wanajamii hawajayakanyaga.

Katika mfano huu wa tatu, gazeti la eneo dogo la majirani [7] linamhoji polisi na kutaka kujua salio la mwisho wa mwaka. Katika mahojiano [8], yaliyopewa jina la “Kaa chonjo na Jirani Mbaya” ofisa huyo anataja tukio ambalo wanachama wa genge la uhalifu walikuwa wanaishi katika nyumba ya kifahari na hata kuwastua sana majirani, walipogundua kuwa walikuwa wakisafirisha silaha ndani ya mifuko ya kubebea vifaa vya mchezo wa tenisi. Na jambo la kushangaza zaidi ni mapendekezo ya ofisa huyo kwa watu wote: waangalie majirani zako na kama ukiwaona vijana wa kiume wenye pesa nyingi wanaishi peke yao, wanakula nje (kwenye migahawa) wakati wote na kuingia na wasichana wanaovutia kwenye nyumba yao, hasa kama wasichana hao wanaonekana kama vile ni wafanyabiashara ya umalaya, basi vijana hao wanaweza kuwa ni majambazi wa kundi la mafia.

Je unafazifahamu jamii zozote na asasi ambazo zinatumia video kusimulia habari ambazo hazitangazwi na vyombo vya habari au kuelezea mitazamo tofauti katika habari zinazotangazwa sana? Tafadhali tushirikishe kwa kuandika katika kisanduku cha maoni au kwa kuniandikia barua fupi!

http://www.flickr.com/photos/mwichary
/ / CC BY 2.0 [9]