- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

China: Tangazo la Google Kusahihisha Uvumi Limezua Utabiri Mwingine

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Teknolojia, Uchumi na Biashara, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari

Ni nini kinachoendelea Google? Mamilioni ya wanamtandao wa China wanajiuliza.

Katika blogu ya lugha ya Kichina inayoendeshwa na Google.cn, Ubao wa Google nchini China, [1] (Google China’s Blackboard), kuna makala yenye kichwa ‘safisha upepo wa uvumi’ inasema:

过去几天里,我们看到有很多关于谷歌中国以及谷歌员工的不真实的传言,一 些报道称我们已经关闭了在中国的办公室,还有一些报道称我们在中国的员工已经接到通知将于近期离职。这些都是不真实的。目前,谷歌中国的员工同过去一样在 办公室正常工作,讨论产品开发,与客户进行沟通。尽管谷歌总部管理层近期宣布他们将会在未来的几个星期与中国政府就一些事宜进行商讨,谷歌中国的员工们仍 在一如既往地努力向我们的用户和合作伙伴提供最好的产品和服务,用户和合作伙伴对谷歌是非常重要的

Katika siku chache zilizopita tumesikia uvumi mwingi kuhusu Google China na wafanyakazi wake. Kuna walitoa ripoti kuwa tumefunga ofisi zetu nchini China na wengine wanadai kuwa wafanyakazi wetu wa China watapoteza kazi zao katika siku chache zijazo. Uvumi huo siyo wa kweli! Wafanyakazi wa Google.cn wanafanya akzi ofisini kama kawaida, wanajadili maendeleo ya bidhaa na wanaongea na wateja wetu. Japokuwa utawala wa makao makuu ya Google yametangaza uamuzi wao wa kujadili masuala kadhaa na serikali ya Uchina, wafanyakazi wake wa China wanafanya kazi kwa juhudi kama kawaida ili kutoa huduma na bidhaa bora zaidi kwa wateja na na wadau wake, ambao ni kuhimu kwa Google.cn. Januari 19

Wiki iliyopita, Google ilitangaza katika blogu yake rasmi [2]uamuzi wake wa kushangaza wa kusitisha kuchuja maudhui katika tovuti yake ya Uchina, hatua ambayo ilitafsiriwa na wengi kama tishio la kuondoka katika soko la China kama italazimika. Uamuzi huo ulisababisha mwitiko mkubwa toka kwa wanamtandao wa Kichina ambao waliiunga mkono hatua hiyo.

Hata hivyo kisa hiki ni kigumu zaidi ya watu walivyofikiri. Uvumi kuhusu makusudio hasa ya Google mara ulisambaa kwenye wavuti. Tafsiri tofauti na mitizamo juu ya uwezekano wa kutoka (kwa Google nchini China) iliambazwa na unyeti wa suala hilo bado haujakoma.

Jasusi ndani
Iliripotiwa kuwa Google inawachunguza wafanyakazi wake kuhusu tuhuma za uhujumu kutokea ndani (ya shirika). Kama makala ya Reuters inavyoashiria [3]:
Vyombo vya habari vya ndani ya nchi, vikinukuu vyanzo ambavyo havikutajwa majina, viliripoti kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Google China walizuiliwa kutmia mitandao ya ndani ya shirika baada ya januari 13, huku baadhi ya wafanyakazi walipewa likizo na wengine walihamishwa kwenda ofisi tofauti za Google kanda ya Asia Pasifiki.

Hebu tuangalie nakala mama katika lugha ya Kichina [4] ambayo imenukuliwa sana na kusambazwa kwenye wavuti.

Google总部在声明退出中国之后,立刻取消了所有中国工程师访问Google代码服务器的权限。
他们都是在上班后发现服务器的home目录进不去了。事先根本没有通知。

Wahandisi wa Kichina walikuta njia zao za kufikia mitambo ya Google zimefungwa wakati Makao Makuu ya Google yalipotangaza uamuzi wa kuondoka nchini China. Bila ya taarifa yoyote ya awali waligundua kuwa hawawezi kufikia mitambo mama wakati walipofika kazini

如果Google是有预谋的撤离,为什么要采取这种手段?他完全可以让员工继续工作,做一些善后工作。为什么Google突然那么不信任中国这边的团队?

Ikiwa kujitoa kwa Google kulikuwa kumepangwa, kwa nini basi walifanya mambo kwa haraka namna hiyo? Wangeweza kuacha kila mmoja aendelee kufanya kazi na kusaidia katika mchakato wa mpito. Kwa nini Google, kwa ghafla, hawana tena imani na wana timu wa Kichina?

唯一的原因就是,Google内部的技术人员中被安插了党的特务(就在Google上海办公处)事实真相就是,这个人在受到党的派遣,应聘Google成功之后,就把Gmail的关键代码down下来然后上交给了组织。而这个组织破解gmail系统的目的就是为了获取“人权团体”的邮件,这些在Google官方的声明都有

Ni lazima, sababu pekee ni kuwa walikuwa ni ‘majasusi’ kanzu, waliotumwa na Chama, waliovumbuliwa pale kwenye ofisi za Google mjini Shanghai wakifanya kazi kama mafundi. Baada ya kuajiriwa walipakua kanuni muhimu za siri za Gmail na kuzigawa kwa mashirika ya Kichina. Lengo lilikuwa ni kudukiza mfumo wa Gmail na kuingilia mawasiliano ya barua pepe za makundi yanayotetea haki za binadamu, na msukumo huo unaonekana katika tangazo la Google.

这样一来会暴露gmail系统的所有漏洞,而且Google官方不能承认这个事情,否则他在国际上的声誉会大受影响。特工这次的窃密行动,使Google有面临全面破产的危险(Google官方博客也说了,牵涉到知识产权的问题),说白了,再在中国呆下去,可能要威胁到整个公司的生存,所以才如此仓促的把中国部门的一切工作全部停掉

Kwa vyovyote vile Google haiwezi kuweka wazi ukweli huu kwani kufanya hivyo kutaweka hadharani mapungufu yote ya Gmail na sifa yake kama mtoaji huduma mwenye usalama itaharibika vibaya. Ujasusi huu umekuwa ni tishio kubwa kwa Google na ni kwa sababu hiyo Google ilisema kuwa masuala ya umiliki wa haki za kitaalamu yalihusika. Ni wazi kuwa Google iliamini kuwa uhai wa kampuni ungekuwa hatarini ikiwa kampuni ingeendelea kuwepo nchini China kwa muda zaidi kwa hiyo Google ilisitisha kazi zake nchini Chini mara moja.

Zaidi ya hayo, makala hiyo inadai kuwa kulikuwa na majasusi watatu, wote hao walikuwa watumishi wa Chama. Hata hivyo, maoni machache yanakejeli (madai hayo) kuwa ni ubashiri wa udaku tu.

Uamuzi Makini

Katika Boxun.com [5], mwanahabari alitoa muhtasari wa matatizo yaliyoikabili Google tangu ilipoingia China.

2006年2月 牌照门
2006年11月 辞职门
2007年2月 地图门
2007年4月 词库门
2007年5月 抄袭门
2007年6月 报告门
2007年7月 流氓软件门
2007年8月 恶搞门
2007年10月 税务门
2008年3月 抄袭门2.0
2008年3月 漏税门
2008年6月 捐款门
2008年6月 泄密门
2008年11月 广告门
2009年1月 低俗门
2009年4月 低俗门2.0
2009年6月 涉黄门
2009年10月 版权门
2009年12月 涉黄门2.0

Sehemu ya tafsiri:

2007/2 kwenye Ramani za Google, kuna mji wa Kichina uliopwekewa jina kutoka enzi za Uvamizi wa Japani
2009/1 Google ilikosolewa na serikali kwa uhuni
2009/10 Google ilishutumiwa kwa kukiuka hakimiliki.
2009/6 Google ilibainika kuwa inaonyesha maudhui ya matusi

试想,有哪一个跨国公司架得住如此频繁的折腾?据统计Google在中国的收入大概是其全球总收入的1%,即使退出中国市场也不影响Google的整体业绩,损失不大,丢脸的是中共独裁政府。

Hebu fikiria, kampuni gani ya kimataifa inaweza kumudu matatizo yote hayo? Mapato ya Google nchini China yanafanya takriban 1% ya mapato yake kwa ujumla, kwa hiyo hata kama italiacha hili soko haitadhurika sana, lakini serikali ya China itapata aibu. Hivyo basi, baadhi ya watu wanaamini kuwa tishio la kujitoa ni simulizi tu ya kuziba mapungufu yake (Google) nchini China.

Mwanablogu Yemingzhu anaona [6] kuwa google imechukua nafasai ya kujitoa China kama kisingizio cha kushindwa kwake kibiashara.

另一种说法是谷歌退出中国,采取这样高调的方式是为了掩饰其在中国的商业失败,从数据上讲,谷歌在中国是属于典型的叫好不叫座,赢得美誉度,没有得到实惠,还投入巨大的成本,从商业上讲,对股东要有交代,退出不是不可以解释。

Mwingine anasema kuwa kujitoa kwa mbwembwe kwa Google kuna nia ya kuziba kushindwa kwake biashara nchini China kwa sababu sifa ya Google haiiongezei mapato. Ukichukulia gharama kubwa iliyopo, kujitoa huko kunaeleweka.

Hivi sasa Google ni injini tafuti ya pili kwa ukubwa katika China bara na ina takriban 30% ya soko wakati Baidu ina 60%

Ma Yun (马云), rais wa alibaba.com, tovuti ya biashara za wavuti ambaye anajulikana sana, aliwakosoa Google:

他说,谷歌在美国的成功是一种创业者精神的成功,是一种永不放弃的精神的成功。而进入中国市场后,则变成了以为可以用钱去改变市场,忽略了过去用脚踏实地、用梦想去改变别人的精神。

Google iefanikiwa nchini Marekani kutokana na uajsiriamali na msisitizo wa wito wake. Hata hivyo, katika China inaota ndoto za mchana kuwa pesa zinaweza kupindisha soko huku wakipuuza ukweli kuwa inawapasa washikilie msimamo wao ili kuwabadilisha wengine kwa ari yao, hatua kwa hatua

.

Pia aliuita uamuzi wa haraka wa Yahoo wa kuiunga mkono Google.

Njama za kisiasa

Gaoren alifikiri [7]kuwa kujitoa kwa Google kunatokana na sababu za kisiasa, zinazodhaminiwa na serikali ya Marekani.

Google是在中国政府的网络监察制度更严格的时候进入中国市场,希望在中国市场分得一羹。在中国政府的网络监察制度越 来越宽松的情况下退出市场,但站出来高调批评网络监察制度,这本身就是滑稽的,也是站不住脚的。至少表明Google和其声明中的道德是格格不入的。 Google只不过是利用政治作为撤出中国市场的遁词。

Google iliingia katika soko la China wakati kulipokuwa na uchujwaji wa habari mkali zaidi na ilijaribu kujinyakulia sehemu kubwa ya soko. Lakini leo hii inajitoa wakati ambapo vizuizi vinazidi kulegezwa. Ni jambo la kushangaza kwa (Google) kusimama na kushutumu vizuizi hivyo katika wakati huu. Haidumishi ili nafasi yake ya kimaadili ambayo inaelezwa kwenye tamko lake na inatumia siasa kama kisingizio cha kujitoa katika soko la China.

按照Google自己的高调标准,Google本身是一个高举道德大旗的魔鬼。2008年印度22岁的IT专业人士 Rahul Krishnakumar Vaid因为在Orkut网站写下“我恨索尼娅甘地(I hate Sonia Gandhi)”而遭逮捕。 Orkut是Google在印度的一个社交网络网站。Google立即向印度警方提供了Vaid的Gmail电子邮件信息。

Kwa kutumia viwango ilivyojiwekea, hili ni zimwi. Mwaka 2008 Rahul Krishnakumar Vaid alikamatwa nchini India kwa kuwa aliandika “Ninamchukia Sonia Gandhi” kwenye Orkut, tovuti ya kijamii. Google mara moja ilitoa taarifa zake za Gmail kwa polisi ilipoombwa kufanya hivyo.

2010年1月7号,国务卿希拉里.克林顿(Hillary Clinton)在国务院请吃饭。这是一场小规模的晚宴,规 模虽小,来客却都是通讯科技界的重量级人物。客人名单上有谷歌首席执行官埃里克.施密特(Eric Schmidt)、Twitter联合创始人杰克.多 尔西(Jack Dorsey)、微软首席研究与战略官克瑞格.蒙迪(Craig Mundie),以及Mobile Accord总裁James  Eberhard, Cisco的行销总裁Susan Bostron,纽约大学教授Clay Shirky, Personal个人民主组织创始人 Andrew Rasiej等。这是美国国务院利用信息技术来推进美国外交目标的努力的一部分。

没过几天,在2010年的1月12日Google就跳出来。Google是否在为美国政府的政治目的服务呢?大家拭目以待。如果Google成为美国政府的政治打手,那中国政府对其政治约束是完全必要和合理的。

Mnamo Januari 7, 2010, Hillary Clinton alialika majina makubwa katika nyanja ya teknolojia ya habari kwenye dhifa, pamoja na Eric Schmidt (Google), Jack Dorsey (Twitter), Craig Mundie (Microsoft), James Eberhard, Susan Bostron (Cisco), Clay Shirky (Professor in NYU), Andrew Basiej (Human Rights Group). Kitendo hiki kilionekana kama sehemu ya mchakato wa Marekani katika kusukuma malengo yake ya kidiplomasia kwa kutumia teknolojia ya habari.
Siku chache baadaye, Google ilijitoa kwa hiyo, inatumikia maslahi ya serikali ya Marekani? Hebu tusubiri. Lakini, kama hii ni sehemu ya mpango wa kisiasa wa Marekani, basi ni sawa tu kwa serikali ya China kuudhibiti.