China na Hong Kong: Walinzi na Wauaji

Bodyguards and Assassins (Walinzi na Wauaji) ni filamu ya kuchangamsha iliyotolewa wakati wa Krismasi huko China, Hong Kong na Taiwan. Ikiwa ni filamu ya kizalendo, awali ilipangwa kutolewa mwezi Oktoba ili kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Watu wa China lakini ikacheleshwa mpaka mwisho wa mwaka 2009. Tofauti na filamu ya Founding of a Republic! (Mwanzo wa Jamhuri ) ambayo inaonyesha mashujaa wa taifa, filamu hiyo inaonyesha waigizaji kadhaa kutoka chini, ambao hawafahamu kitu chochote kuhusu mapinduzi lakini wanajitolea maisha kwa ajili ya nchi yao. Simulizi hii inatoa masomo yenye utofauti na tafsiri kuhusu Historia ya China na siasa.

Maoni yaliyotolewa Na Sun Yat-sen, Baba WA Taifa la China katika filamu hiyo, inasemekana kuwa yamenukuliwa sana kwenye wavuti:

欲求文明之幸福,必经文明之痛苦,而这痛苦,就叫做革命。

Ikiwa ukitaka kutafuta furaha ya watu (katika utamaduni au ustaarabu fulani) ni lazima kwanza upitie uchungu ya watu hao, na uchungu wa namna hii unaitwa mapinduzi.

Sheng Haifang aliguswa sana na mstari huo:

应该说这是我见过的关于革命最好的解读,它让我在某种程度上,终于和“革命”这个词握手言和。我可以厌恶革命,可以反对主 义,但是对于革命者,对于为主义而赴死的人,甚至被主义吞噬的人们,我心怀尊重。我今日之所感所知所思所享,无不来自于百年来这些努力去实现臆想中“中国 明天”的人们。他们或伟大或浅薄或愚蠢或无私或卑劣或聪明或成功或失败或一代领袖或千古罪人,我可以评判他们,同时心怀某种敬畏与感激。

Ninaweza kusema kuwa hii ni tafsiri nzuri zaidi ya mapinduzi niliyowahi kuiona. Inanifanya nijumuike na neno “mapinduzi” kwa kiasi fulani. Ninaweza kuchukia mapinduzi na kupinga Umaxisti, ninawapa heshima yao. Kitu ninachohisi, ninachojua, ninachofikiri na kitu kinachoniburudisha vyote vimetoka kwa wale waliopigania China ya kesho katika karne iliyopita. Wnaweza wakawa wakuu, wasio na kina, wajinga, wasiojali nafsi, wanaoweza kudharauliwa, werevu, walio na mafanikio, wanaweza kuwa viongozi au watenda dhambi wa umri, ninaweza kuwahukumu, lakini pia ninawasujudia na kuwashukuru.

Hata hivyo, Sheng alipumua kwa ahueni kutokana na kufifia kwa shauku, na utumiaji mbaya wa misamiati ya kianamapinduzi.

我们已经无法体会到当初那些热情,因为我们失去了那个感知热情的时代环境。革命、民主、自由、主义、共和、共产、大同……都是曾经被用以呼唤理性、现代性、个性、人性与新的时代,同时也这些词也被用以唤起多数人的暴力,用以巩固权力,用以践踏权利与扭曲人性、创造同质化。

Hatuwezi tena kuhisi hisia za zama zile, kwa sababu hatuna mazingira yanaweza kusababisha hisia zile. Mapinduzi, demokrasi, uhuru, Umaxisti, jamhuri, Ukomunisti, raha kuu, haya ndio maneno ambayo yaliwahi kutumika ili kuamsha uleo, ubinafsi, utu na zama mpya. Vivyo hivyo, maneno hayo yalitumika pia kuamsha udhalimu na kuimarisha nguvu, kukanyaga-kanyaga haki na kupindisha asili ya binadamu, ili kuwafanya watu wote wawe sare.

Qingnianganjiang alilinganisha filamu hiyo ya Walinzi na Wauaji na salamu za kuadhimisha miaka 60 ya filamu ya Mwanzo wa Jamhuri! katika ingizo lake la kwenye blogu “Saluti Iliyochelewa” na kuonyesha kuwa ujumbe wa siasa katika filamu umepishana na itikadi rasmi:

《十月围城》。它不会和我讲大道理,它更加不会强迫我接受主旋律的洗脑。我这30年来,实在是受够了,害怕了精神上的洗 脑。。。《十月围城》里的日与月,是为了中国未来。欲求文明之幸福,不得不经文明之痛苦。中国求解解放、文明、自由的路,从来是走的辛苦。那群牺牲的人 民,我们从来是要用崇敬的眼光去看待他们。不因历史变迁,不因空间改变,更不能因改朝换代而把他们遗忘。

Walinzi na Wauaji haitanihubiria mawazo makubwa na kunilazimisha kuosha akili yangu na kukubali itikadi rasmi. Nimeteseka vya kutosha katika miaka 30 iliyopita na ninahofia kuoshwa akili. Watu wa kwenye filamu kwanza waliteseka na uchungu wa utamaduni mzima wa watu wao ili kutafuta furaha ya baadaye ya watu wa China. China imefuata njia ngumu na ya uangalifu kufikia uhuru na ustaarabu. Ni lkazima tuwaenzi wale waliokufa katika njia hiyo na tusiwasahau kutokana na mabadiliko ya nguvu tawala katika historia.

Tubingenmujiang pia alizilinganisha filamu hizo mbili lakini alizisoma tofauti: Mwanablogu huyu anaamini kuwa filamu zote mbili zimetengeneza tena ngano ile ile ya zamani ya “Kiongozi ndiye wa kwanza”:

在我看来,《十月围城》也是一部神话片——当国家消亡的神话被民族国家的神话所取代时,《十月围城》的骨子里无非是又一部 《建国大业》,只不过后者囿于具体指向而主要局限在海峡一隅传播,《十月围城》则把落脚点放在了两岸都能接受的“中华民族最大公约数”那里,明后年就是民 国建国百周年纪念,想必《十月围城》剑指金马奖,已是司马昭之心。

Kwa maoni yangu, filamu ya Walinzi na Wauaji pia inajaribu kutengeneza ngano – ngano ya taifa linalokua. Filamu hii, katika kiini chake, ni nyingine ya (filamu) Kuanza Kwa Taifa, lakini hii ya pili ililenga soko la China Bara, wakati Walinzi na Wauaji imetengeneza jambo kubwa linalowashirikisha wote katika Mkondo wa Taiwan. Wakati miaka mia moja ya kuanza kwa China inakaribia, ninadhani kuwa Walinzi na Wauaji inalenga kwenye Tuzo ya Farasi wa Dhahabu.

《十月围城》在一个波诡云谲的时代背景里,打造了一出关于救世主的神话。不过陈德森很聪明,他并没有简单的树立一个高、 大、全的神主牌位,而是着力打造了从财主到乞丐,从大亨到流氓的牺牲群像,用断片切面的手法较为全面的展现了那个时代的香港风貌。所以,整部《十月围城》 看下来,便是一出仁人志士舍生取义“让领导先走”的神话催泪弹。

Walinzi Na Wauaji ikiwa mbele ya picha kubwa ya wakati wa kihistoria wenye vurugu, inatengeneza tena ile ngano ya mkombozi wa taifa. Mkurugenzi, Chan Tak Sum, ni mjanja sana. Hakutengeneza mnara mkubwa wa kitu kinachofanana na mungu, lakini alitilia makini watu wa kawaida (mfanyabiashara, ombaomba, na magenge) ambao waliamua kujitolea maisha yao kwa ajili ya kiongozi wa mapinduzi. Filamu hii inaonyesha picha ya Hong kong ya zamani, na inawatoa machozi watu wa kawaida kwa hadithi yake ya ngano kuhusu imani ya watu ya “muachia kiongozi atangulie”.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.