- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

China: Kwa Heri Google

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Teknolojia, Uchumi na Biashara, Uhuru wa Kujieleza

Kufuatia tangazo la Google leo [1] kuwa ikiwa serikali ya China haitaruhusu tawi lake la China kusitisha uzuiaji wa matokeo ya kutafuta tawi la Google nchini China litafungwa, wanamtandao walitembea mpaka kwenye ofisi za Google mjini Beijing ili kuweka maua [1]. HABARI MPYA: picha zaidi hapa [2], uwekaji rasmi wa maua (ya rambirambi) kwenye ofisi za google umepangwa kufanyika baadaye leo.