China: Adhabu ya Kifo kwa Akmal, ni Tendo la Kufuta Aibu ya Zamani

Akmal Shaikh, raia wa Uingereza aliyeshtakiwa kwa kuingiza mihadarati kinyume cha sheria nchini China, aliuwawa siku ya Jumanne japokuwa familia yake pamoja na serikali ya Uingereza waliomba adhabu ipunguzwe, wakidai kuwa alikuwa ni mgonjwa wa akili.

Mahakama Kuu ya China hata hivyo ilikataa ombi la kuangalia hali ya akili ya Akmal kwa sababu hati zilizotolewa na Ubalozi wa Uingereza hazikuweza kuhakikisha kuwa Akmal ana matatizo ya akili.

Baada ya Akmal kudungwa sindano ya sumu, serikali ya Uingereza na baadhi ya mashirika ya kupigania haki yalijibu vikali. Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown alishutumu mauaji hayo na kusema kuwa “anaguswa hasa na ukweli kuwa hakuna tathmini yoyote ya akili iliyofanywa.”

Ikikabilia na kukosolewa, China ilieleza vikali kutoridhika. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje alisema kuwa shutuma hizo hazina msingi na kuonya kuwa kuingiliwa kunaweza kuharibu mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Katika China, upitishaji wa madawa ya kulevya unachukuliwa kama kosa la jinai. Adhabu ya kifo itatolewa kwa kubeba au kuuza mihadarati ya zaidi ya uzito wa gramu 50 kwa mujibu wa sheria za China, na alikutwa na zaidi ya gramu 4000.

Kwa raia wengi wa wavuti wa Kichina, tukio hili limewakumbusha Vita ya Pili ya Mihadarati iliyopiganwa katika karne ya 19 ambapo majeshi ya Uningereza yaliivamia China kwa sababu maofisa wa Kichina walichoma moto mihadarati iliyozwa kwa Uingereza. China ilishindwa vita na kuteseka kutokana na “miaka 100 ya aibu” tangu hapo.

Katika 163.com, huduma ya tovuti kubwa nchini China, zaidi ya watu 3000 waliunga mkono maoni yaliyoachwa hapo baada kipande cha habari, kilichoandikwa:

老外就了不起了…..贩毒就该杀

Je kuna chochote kilicho tofauti kwa mmagharibi? Mfanyabiashara wa madawa ya kulevya ni lazima auwawe.

Acekingfang, zaidi ya yote, alifikiri kuwa kuuwawa huko kunaonyesha kuwa China anakua.

同样是没收“鸦片”、惩办英国毒贩,170年的1839年林则徐的“禁烟”引发清王朝的世纪第一战,英国人靠鸦片和大炮打 开了中国的大门…. 1856年清政府在“亚罗号”上逮捕了几名海盗,这一本属于中国内政的事件被英军当做发兵的借口而发动了第二次鸦片战争,150年前的1859年第二次鸦 片战争中英法联军在天津大沽口战胜清军,进而向北京城发兵,此年火烧圆明园,烧杀抢掠,虏走中国无数的文物、财宝,使得中华民族遭受历史上最沉重的灾难和 损失之一。

Tofauti na ilivyokuwa, kukamatwa kwa mihadarati na kuadhibiwa kwa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya Waingereza miaka 170 iliyopita ilipelekea vita ya kwanza ya China katika karne, ambayo kwayo Waingereza walifungua kwa nguvu lango la China kwa kutumia mihadarati na mizinga. Mwaka 1856 Uingereza ilianzisha Vita nyingine ya Mihadarati, kwa kuchukulia kukamatwa kwa maharamia wachache wa ufalme wa Qing kama kisingizio. Majeshi ya mseto ya Waingereza na Wafaransa yalilishinda jeshi la China kisha wakaingia mjini Beijing, wakaichoma moto Kasri ya Zamani ya Majira ya Kiangazi, na kupora tani za hazina, kitu ambacho kilikuwa ni janga la kutisha zaidi katika historia ya China.

而今当英国贩毒分子在我们的国土上做出法律所不容的事情,我们可以正大光明的用我们自己法律的手段惩治毒贩,绝不留情,不用看别人的脸色,这也从侧面显示:中国可以不高兴,后果很严重!

Leo hii wakati mfanyabiashara ya madawa ya kulevya Muingereza alipokiuka sheria katika ardhi yetu, tunaweza katika uwazi na kwa haki kumuadhibu bila huruma yoyote. Hatuhitaji tena kufuata amri za wengine. Hii inaonyesha kuwa China inaweza isifurahi, na matokeo ya kuichokoza China ni makubwa.

Maoni ya zha811 yalionyesha fikra kama hizo:

比如把大英博物馆的一些中国收藏拿来我们也许会认真考虑的!!

Kama mngerudisha baadhi ya hazina za China zinazotunzwa kwenye makumbusho ya Uingereza ambazo ziliporwa kutoka China, tungeliweza kuyachukulia mapendekezo yenu kwa makini.

zhun2875 alisema,

这是我们的内政,关英国人什么事?

Hili ni suala letu la ndani. Linahusiana vipi na Waingereza?

Nchini China, kwa muda mrefu imelalamikwa kwamba watu wan chi za nje, hasa Wamagharibi, wanatendewa kama vile wana hadhi ya juu. Katika mwaka 2008, treni ilisimama kinyume na ratiba ili kuwapeleka abiria kadhaa wa Kijapani uwanja wa ndege na hata magari ya polisi yalitumika kuwasindikiza. Hata hivyo, katika kesi nyingine raia wa China mwenye ugonjwa wa akili alifungwa kwenye kiti cha treni na wahudumu na kuachwa hadi kufa bila ya mtu yeyote kumhudumia. Wakati huu, uamuzi wa mahakama unaowatendea watu wote sawasawa inaelekea kuwa unapata washangiliaji.

Wang Wen, mhariri wa global times, anaamini:

归根结底,外国人在华犯罪,由谁来判,怎么判,必须严格按中国的法律程序来办。洋人犯法,能否与国人同罪,是一个司法公正的问题。

Baada ya yote, swali la ni nani na kwa jinsi gani kumhukumu nje anayetuhumiwa ndani ya China linapaswa kutazamwa kwa mujibu wa sheria ya China. Ni suala la haki za kisheria.

Baadhi ya maoni yanashikilia kuwa huku ni kushindwa kwa diplomasia kwa serikali ya Uingereza kwa sababu inashindwa kuelewa jinsi Wachina wanavyofikiri. Maoni haya yanatoa mwangwi katika maoni haya:

我很同情阿克毛和他的亲人们,死刑是一个残酷的刑罚,我个人一直觉得,这是一个非常不人道的做法。但,就司法本身的刚性原则显示,只要中国还没有废除死刑,只要别的死刑犯还在遭受这样的待遇,阿克毛就没有任何可以例外的理由。否则,人为制造的区别,将带来更多的悲剧。

Nina huruma kwa Akmal na familia yake. Adhabu ya kifo ni kali na, haina utu, kama vile ninavyofikiri siku zote. Lakini kwa kuwa China bado haijakomesha adhabu ya kifo, na kwa kuwa wahalifu wengine wanaadhibiwa katika njia hiyo hiyo, Akmal hapaswi kuwa tofauti. Vinginevyo, tofauti ikifanywa kwa makusudi itasababisha dhahama nyingine nyingi.

在以往中国因种种罪犯的引渡问题与别国的交涉时,中国总是无一例外的被拒绝。哪怕需要引渡的是恐怖分子,西方也都会用本国 法律中的相应条款直接拒绝。最直接的借口是,欧美国家的三权分立和绝对的司法独立,是一道谁也越不过去的门槛。但这次英国举国上下几乎都忘记了司法独立的 最高原则,而是寄希望于中国高层对司法的直接干预,试图让阿克毛逃脱一死。

Huko nyuma wakati China ilipojaribu kuwarejesha hata magaidi nchi za magharibi mara nyingi zilikataa kwa kunukuu vipengele vya sheria zao. Kisingizo cha moja kwa moja ni kile cha taratibu na mizani ya madaraka pamoja na uhuru wa vyombo vya sheria. Lakini wakati huu, Uingereza inaonekana kuwa imesahau kanuni hiyo na kusimika matumaini katika kuingilia ukiritimba.

当西方试图群起将一个罪犯的生命与更多的东西挂钩,逼中国高层就范时,阿克毛,其实就已经不得的不死了。原因太简单,13亿中国人都在用天枰称着自己和那个叫阿克毛的鬼佬在国家里的重量。鬼佬的生命是命,我们自己就天生是草?

Pale Uingereza ilipojaribu kutengeneza kesi kubwa kuliko ilivyo ili kuilazimisha serikali ya China kulegeza (adhabu ya) kifo kwa Akmal kila kitu kilikuwa kimekamilika. Ni rahisi kuona watu bilioni 1.3 wanavyopima maisha ya Akmal dhidi ya maisha yao. Kama maisha ya mtu wa magharibi yana thamani kubwa, je maisha yetu hayana thamani?

3 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.