- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Baada Ya Tetemeko la Ardhi, Jumbe za Twita Kutoka kwa Walioshuhudia

Mada za Habari: Nchi za Caribiani, Haiti, Habari za Hivi Punde, Majanga

Kutokana na janga la tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 ambalo limeikumba Haiti jioni ya leo [1] (Januari 12), “Haiti” ni mada kuu hivi sasa kwenye huduma ya Twita. Miongoni mwa lundo la jumbe zinazotumwa tena na tena za taarifa za habari kutoka za vyombo vya habari vikubwa na jumbe nyingine za twita zinazotuma sala au dua pamoja na salamu za heri kwa taifa hili la Karibea, pia kumekuwepo taarifa za mashahidi waliopo kwenye tukio kama vile mwanamuziki na mwendesha hoteli Richard Morse [2], ambaye anatwiti kwa jina la @RAMHaiti [3]. Morse alituma ujumbe huu wa kwanza wa twita [4] kwenye majira ya saa 12 jioni kwa saa za Haiti, akiripoti kuwa:

Tuko salama hapa oloffson [hoteli anayoiendesha] .. intaneti inapatikana!! Hakuna simu! Natumaini wote wako salama… majengo mengi makubwa hapa PAP [Port Au Prince, mji mkuu wa Haiti] yameporomoka!

Mfululizo wa jumbe za twita zilizotumwa saa moja baadaye ziliripoti:

Karibu kila taa imezimwa katrika mji wa Port au Prince… watu bado wanapiga mayowe lakini sauti zao zinafifia kadiri giza linavyotanda. [5]

kuna uvumi kuhusu majengo gani yaliyoanguka… jingo la Castel Haiti nyuma ya oloffson ni biwi la kifusi… lilikuwa jingo la ghorofa 8 kwenda juu [6]

Wageni wetu wamekaa nje kwenye barabara ya gari… hakuna uharibifu mkubwa hapa Oloffson lakini majengo mengi makubwa yaliyo jirani yameanguka [7]

Nimeambiwa kuwa sehemu za kasri (ikulu) zimeanguka… UNIBANK hapa mtaa wa Capois imeporomoka [8]

watu wanawaleta watu kwa machela

Port au Prince iko kwenye giza isipokuwa kwa mioto michache [9]

Hospitali kubwa iliyokuwa inajengwa mkabala na Oloffson imeporomoka [10]

magari yanaanza kuzunguka.. Ninaziona taa kwa mbali kuelekea dagoni [11]

Baadaye, Morse alituma tena ujumbe wa twita [12] @isabelleMORSE, ambaye aliripoti “uharibifu mkubwa kwenye mtaa wa Grand (Ave Dessalines) Daniel Morel’s iko sawa, stesheni ya polisi, Downtown teleco, kanisa la Mtakatifu Anne yote yameangamia” [12].

Mara baada ya saa 1 jioni kwa saa za Haiti, Morse aliandika kwamba:


Simu zinaanza kufanya kazi. Nimepokea simu kutoka kwa mtu ambaye nyumba yake iliporomoka, mtoto kaumia lakini salama.
.Watu wachache wanaanza kujitokeza @Oloffson.. barabara hazipitiki kutokana na kuta zilizoanguka..maangamizi makubwa katika mtaa wa Grand. Nasikia hospitali kuu imeporomoka [13]

watu wanahitaji madawa na vifaa vya matibabu, chakula, malazi; sijui kuhusu hali ya maji

Kisha, kwenye majira ya saa 1:45 jioni:

tetemeko jingine dogo.. watu wanapiga mayowe na kukimbia kuelekea uwanjani.. wanaimba na kusali sana katika makundi makubwa

Na kwenye majira ya saa 2:40 usiku kwa saa za Haiti:

tetemeko jingine dogo.. limechukua muda mrefu zaidi.. mayowe mengi mjini.. huu utakuwa usiku mrefu [14]

Pia zinazotawala katika Twita ni picha za maangamizi na uharibifu zilizopigwa na raia kama hizi hapa chini, inadaiwa [15] kuwa zilitumwa kwa mtumiaji wa Twita @marvinady [16] na mwanahabari Carel Padre [17] wa Radio One Haiti.

@LisandroSuero [18] pia ametuma picha [19] za maangamizi, pamoja nah ii hapa chini: