Australia: Mauaji ya Mhindi Yazua Mzozo

Mauaji ya mtu mwenye asili ya India mjini Melbourne yamewasha tena mjadala kuhusu ubaguzi wa rangi nchini Australia na usalama wa wanafunzi kutoka ng’ambo. Kadhalika yameathiri uhusiano kati ya Australia na India:

Wanadiplomasia wa Kihindi wanatarajiwa kukutana na wenzao wa Australia kwa ajili ya mazungumzo ya kutatua tatizo hili huko Canberra leo kufuatia kifo cha muhamiaji wa Kihindi mjini Melbourne.

Mauaji ya kijana wa miaka 21 Nitin Garg, ambaye pia ana shahada ya Uhasibu katika bustani za Yarraville Jumamosi usiku yalishutumiwa vikali na wanasiasa nchini India na Australia.

Matatizo ya kidiplomasia yazuka baada ya mauaji ya mwanafunzi wa Kihindi

Maoni ya wanablogu wa Australia yanaonyesha utofauti katika mitazamo.

Gerard Henderson, Mkurugenzi Mtendaji wa The Sydney Institute, anabashiri matokeo ya chini-chini katika mahusiano ya kisiasa katika kanda hii kwenye makala ya maoni ya gazeti la Sydney Morning Herald :

Tukio hili la kusikitisha limetokea wakati kuna kupooza katika uhusiano kati ya mataifa haya mawili katika miaka michache iliyopita. Wakati wa ziara nchini India mwishoni mwa 2008 nilishangaa kusikia kukosolewa vikali kwa Kevin Rudd katika ngazi za juu za serikali ya New Delhi. Lalamiko kuu la India lilizungukia katika uamuzi wa serikali ya Rudd kukataa kuiuzia india madini ya Uranium, uamuzi ambao uliipindua nia ya John Howard pamoja na mawaziri wake.

Kupigwa kwa wanafunzi kwafundisha masomo makali kuhusu ubaguzi wa rangi

Loon Pond, anayejulikana pia kama Dorothy Parker, anamchachafya Henderson:

Je ni mimi, au ni uchafuzi wa aina ya ajabu kuunganisha kupigwa na kuuwawa kwa Wahindi nchini Australia na sera za sasa kuhusiana na uuzaji wa madini ya Uranium kwa India?

Hiyo ni aina ya dansi ngumu ya kugongagonga kama inavyochezwa na Gerard Henderson katika makala ya Kupigwa kwa wanafunzi kwafundisha masomo makali kuhusu ubaguzi wa rangi.

Gerard Henderson, India, uranium, uhalifu wa mitaani, na makala chafu

Peter Maher anablogu kwa ajili ya redio stesheni ya Melbourne 3AW, anahofia kuwa kuna utamaduni wa kujidanganya au kupinga, ikiwa mauaji hayo yalisababishwa na ubaguzi wa rangi au la:

Kwa namna gani mtu yeyote anaweza kusema kuwa (mauaji haya) hayana uhusiano na ubaguzi wa rangi wakati hawayajui mazingira ya mauaji hayo na kama nilivyosema awali ni vigumu kuelewa.

Jambo ninalofahamu hata hivyo ni kuwa tabia hii ya utesi, ya ghasia, na ya kiuaji kwa Wahindi katika nchi hii imekuwa ya kawaida mno kusema kuwa hatuna tatizo na ubaguzi wa rangi katika nchi hii.

… Tu wepesi sana kusukumiza tabia hizi za kibaguzi chini ya zulia na kuupa ulimwengu picha inayotuonyesha kama watu wasio na ubaguzi na wakarimu.

Nafikiri muda umefika kwa sisi kujiangalia vyema katika nafsi zetu na kufanya kitu kuhusu ubaguzi wa rangi ambao upo katika nchi hii.

Australia Amkeni! Sisi ni wabaguzi

Dave, anayeblogu kama True Blue Aussie, hana mashaka juu ya asili ya ubaguzi wowote wa rangi:

Naam kila mmoja katika Melbourne anafahamu, kuwa Footscray, ambacho kilikuwa ni kitongoji cha Australia, hivi sasa kimejaa Wasudani Waislamu, Waarabu wa Mashariki ya Kati na Wasomali. Hakuna Waaustralia wanaoonekana Footscray. Kwa hiyo, karibu katika shimo la kuzimu la tamaduni mbalimbali kuishi pamoja, utofauti wa makabila na uhamiaji ambapo wahamiaji (katika shauri hili inawezekana kabisa wakawa Waislamu) wanawashambulia wahamiaji wengine na Waaustralia ndio wanaolaumiwa. Dave

Wahamiaji wabaguzi watalaumiwa kwa ajili ya Muhindi kuchomwa.

Kundi la Facebook, Waaustralia wa Kweli 1,000,000 Wanaopinga Ubaguzi wa Rangi, lina mtazamo tofauti kabisa juu ya maana ya kuwa “Mu-australia”

Kusitisha wale wachache wenye sauti kubwa ambao wanatumia Facebook na vipindi vya kupiga simu redioni kuifanya nchi hii nzuri kuonekana kama vile ahera ya WABAGUZI (wanaojulikana kama rednecks)

Andrew Bartlett, seneta wa zamani wa Chama Cha Democrats na mgombea wa Chama cha Greens katika uchaguzi ujao wa taifa, anataka vitendo zaidi kutoka kwa wote, viongozi wa majimbo na wale wa kitaifa. Akiandika kwa ajili ya Asian Correspondent anadai:

Wakati kila kosa linatakiwa kutendewa kutokana na ubora wa vigezo, na kwamba hatutakiwi kudhani kuwa kosa hili jipya zaidi la jinai lilisababishwa na ubaguzi wa rangi, historia ya mashambulizi mengine ya huko nyuma, na mwendo wa pole wa mamlaka za Australia katika kulichukulia suala hili kwa umakini unaofaa, vinamaanisha kuwa tukio moja tu lenye uzito kama hili kimelifanya gazeti la Hindustan Times kuripoti kuwa, maofisa wa serikali ya India ‘watalazimika’ kutoa maonyo (ya safari) katika mtindo wa kuwaonya wale ambao wanataka kufanya kazi au kusoma nchini Australia, ikiwa mamlaka ya Australia hayatachukua hatua kali wakati huu.

Ni wajibu wa serikali na viongozi wa jamii kuchukua hatua zenye ufanisi ili kuwahakikishia watu kuwa (a) suala hili linashughulikiwa kwa uzito wa hali juu, na (b) kila jambo linalowezekana linafanywa ili kuhakikisha usalama wa watu. Ikiwa kuna mashaka kuwa watu wanalengwa kutokana na rangi yao, ni muhimu kila kitu kifanywe ili kupunguza hatari kwa watu hao.

Mauaji ya kusikitisha yarudisha mwangaza juu ya usalama wa Wahindi nchini Australia

Wakati huo huo usalama wa wanamichezo na wageni kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola mwezi Oktoba 2010 ni suala linaloendelea ambalo linaweza kulipuka wakati wowote. Idara ya Mambo ya Nje na Biashara ya Australia ina Kiwango cha Juu cha Tahadhari katika ushauri wa safari kwenda India. Nipe nikupe pengine?

HABARI MPYA JANUARI 6, 2010

Gazeti la The Times of India linaripoti kuwa onyo lile lilitokana na:

Baada ya kusalimu amri kutokana na hasira za walio wengi juu ya mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wanafunzi wa Kihindi nchini Australia, siku ya Jumanne serikali ilitoa onyo la kuwaasa wanafunzi wanaoelekea Australia kwa masomo na kwa wale ambao wako huko tayari.

Wizara ya Mambo ya Nje iliwatahadharisha wanafunzi kuwa vitendo vya vurugu vimeanza kuiathiri jamii kubwa zaidi ya Wahindi nchini Australia. Wasia huo umekuja siku tatu baada ya mhitimu wa shahada ya uhasibu Nitin Garg kuchomwa kisu mpaka kufa, kifo cha kwanza katika mashambulizi hayo. Pia wasia huo ulikuja katika siku ambayo maofisa wa Australia na India walipokutana huko Canberra ili kutafuta njia nzuri zaidi za kukabiliana na vitendo viovu – wakati huo huo ambapo mwili uliongua kiasi wa Mhindi mwingine ulipopatikana.

Onyo linawataka wanafunzi wawe waangalifu wanapokuwa Australia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.