Habari kutoka 30 Januari 2010
Rais wa Malawi kutangaza rasmi penzi lake siku ya Valentine
Wamalawi wanatafakari taarifa kuwa mnamo tarehe 1 Mei, rais wa nchi Dkt. Bingu wa Mutharika anatarajiwa kumuoa waziri wa zamani wa utalii Callister Moyo. Harusi hiyo itatanguliwa na sherehe za kitamaduni za uchumba wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino tarehe 14 Februari. Wanabloga wachache wamemtakia heri rais katika mapenzi mapya aliyoyapata baada ya kifo cha mkewe Ethel miaka mitatu iliyopita.
Naijeria: Uzoma Okere ashinda kesi dhidi ya jeshi
Nigerian curiosity anaandika kuhusu kesi ya Uzoma Okere huko Naijeria: “Uzoma Okere ni msichana wa Kinaijeria ambaye kipigo alichopata kutoka kwa maafisa wa jeshi kiliondokea kuwa video iliyosambazwa sana na...
Eritrea: Utawala Ulio Madarakani Uondelewe Haraka
Kwa mujibu wa Mohammed Hagos, mradi wa demokrasi katika Eritrea unapaswa uanze kwa kuuondoa madarakani utawala uliopo sasa: “Kikwazo kinachowazuia watu wa Eritrea kujieleza ni utawala wa Issayas. Njia ya...
Philippines: “Muswada wa Mkataba wa Ndoa Jadidifu”
Kikundi kimoja cha masuala maalum ya jamii nchini Philippines kinataka kuwasilisha sheria ambayo itaufanya mkataba wa ndoa kuwa na nguvu kwa miaka kumi tu. Pendekezo hilo la kipekee limezua mjadala mkali kwenye ulimwengu wa blogu.