17 Januari 2010

Habari kutoka 17 Januari 2010

Marekani: Raia wa Haiti Wapatiwa Hadhi ya Hifadhi ya Muda

Hadhi ya Hifadhi ya Muda (inayojulikana kama TPS) ni hadhi maalumu inayotolewa na Marekani kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi fulanifulani ambamo kunakuwa kumetokea aina fulani ya janga au pigo la karibuni, kama vile vita au tetemeko la ardhi. Jana, Utawala wa Rais Obama ulitoa hadhi hiyo kwa raia wa nchi ya Haiti itakayotumika kwa kipindi cha miezi kumi na nane ijayo. Jillian C. York anapitia jinsi suala hili lilivyopokelewa katika blogu mbalimbali.

17 Januari 2010

Misri: wanablogu Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutembelea kwao Naha Hammady

Leo Misri iliwatia mbaroni wanablogu 20 waliokuwa wakitembelea eneo la Naga Hammady huko Misri ya Juu ili kutoa heshima zao kwa watu waliouwawa katika shambulio la kidini mnano January 7 mwaka huu. Watu 7 waliuwawa kwa risasi huku wengine wengi wakijeruhiwa pale mwuaji alipowamiminia risasi Wakristo wa Madhehebu ya Kikopti waliokuwa wakitoka kanisani mara baada ya Misa ya Krismas (Wakopti husherehekea Krismas kila tarehe 7 Januari). Uamuzi wa kutembelea eneo hilo uliofanywa na wanablogu hao ulikuwa ni kwa lengo la kuungana dhidi ya uhasama wa kidini.

17 Januari 2010

Haiti: Uenezaji Habari na Taarifa

Sisi tulio nje ya Haiti tunaweza tu kujenga picha kichwani kuhusu hali halisi ya maisha ya kila siku yalivyo huko baada ya tetemeko baya la ardhi - lakini katikati ya juhudi za kuwatafuta wapendwa ndugu, juhudi za kuwahudumia waliojeruhiwa na jukumu zito na gumu la kuwafikishia msaada wa kiutu wale wanaouhitaji zaidi - wanablogu walio huko Port-au-Prince na maeneo ya jirani wanawasiliana na ulimwengu wa nje, ambao nao unahangaika kutaka kupata taarifa kutoka kwa wale waliokuwa katika eneo lenyewe kabisa la janga.

17 Januari 2010

Haiti: Twita Kutoka Eneo La Tukio

Wakati habari za tetemeko la ardhi huko Haiti zikitoa mwangwi duniani kote, wakazi majasiri, wanahabari wan je, na wafanyakazi wa misaada wanaandika jumbe za twita kutokea katika eneo lililoathirika. Baadhi yao wanafanya kazi ya kukusanya misaada na fedha, wakati wengine wanajaribu tu kuionyesha dunia mambo yanavyooendelea nchini Haiti.

17 Januari 2010