Habari kutoka 6 Januari 2010
Sri Lanka: Kulipia Vyombo Vya Kimataifa Vya Habari kwa Ajili ya Uchaguzi wa Ndani
Kampeni kabambe ya Rais wa Sri Lanka aliye madarakani, Mahinda Rajapakshe inajumuisha manunuzi ya nafasi za matangazo katika tovuti mashuhuri za vyombo vya habari duniani. Groundviews anahoji sababu ya kuvilipa...
Slovakia, Hungaria: Heri ya Mwaka Mpya!
Uhusiano kati ya nchi mbili jirani za Slovakia na Hungaria ulianza kutetereka katika mwaka uliopita - lakini baadhi ya wananchi wa Slovakia na Hungaria wanafanya juhudi kurekebisha hali hiyo kwa kuzindua kampeni ya mtandaoni inayojulikana kama "Štastný nový rok, Slovensko! / Boldog Új Évet Magyarország!" ("Heri ya Mwaka Mpya, Slovakia!/Heri ya Mwaka Mpya, Hungaria!).
Kuchapisha Bloguni kuhusu Utamaduni na Ndoa za Watu wa Asili Tofauti
Idadi kadhaa ya familia zinazoundwa na watu wa rangi na dini tofauti wanasimulia kuhusu uzoefu wa maisha yao katika familia zao kupitia ulimwengu wa blogu. Majaribu na mahangaiko ya wanandoa wenye asili tofauti yanaonyesha, kama kioo, jinsi sisi, kama watu tuliostaarabika, tulivyotoka mbali na hasa katika kupokea na kuheshimu tofauti zetu.
Lebanoni: Matukio ya Wafanyakazi Kujiua ‘Yanadharauliwa’
Matthew Cassel anaripoti tukio la kujia la Theresa Seda, mfanyakazi wa ndani wa Kifilipino jijini Beirut. Soma habari za kina za kutisha za jinsi vifo vya namna hiyo vinavyoongezeka kwa...