Wakati siku ya kwanza ya Warsha ya Pili ya Mwaka ya Wanablogu wa Uarabuni [1] ikifungwa, tutaangalia tafakuri za washiriki kwa siku nzima, kujua wamejifunza nini na namna wanavyojisikia.
Siku ilianza kwa kishindo, wakati waandaaji wa Global Voices Sami ben Gharbia [2], Amira Al Hussaini [3], na wafadhili wetu kutoka Mfuko wa Heinrich Böll [4] waliwakaribisha washiriki kutoka kote Uarabuni na nje ya mipaka. Kufuatia utambulisho, watoa mada Noha Atef [5] wa idara ya Utetezi ya Global Voices na Eman Abdulrahman [6] wa Global Voices (na mwanzilishi wa Koleana Laila [7]) walishirikisha dondoo na mawazo kuhusu namna ya kutengeneza kampeni bora mtandaoni. Mshiriki wa Kimauritania weddady aliandika kuwa Kolana Laila inatafuta kujenga ushirikiano kote Uarabuni katika twita yake:
Siku nzima, kulikuwa na warsha mahsusi, kuhusu kila kitu kuanzia namna ya kukabiliana na ugumu na kuficha jina (mada iliyotolewa na Jacob Applebaum [8]) mpka uanahabari wa kiraia (mada iliyotolewa na Amira Al Hussaini [3] na Salam Pax [9]) njia za kuhifadhi video mbadala wa YouTube (ilitolewa na Slim Amamou [10] na Marcin Gajewski). Kwa hili la pili, Lina ben Mhenni alikuwa na maoni haya:
Hata hivyo, mada iliyowafanya washiriki washikwe na hasira, ilikuwa ni ile iliyotolewa na mshiriki wa ki-Syria Razan Ghazzawi [11] juu ya tafiti inayotengeneza ramani ya ulimwengu wa blogu wa Kiarabu [12] iliyofanywa na Kituo cha Berkman kwa Ajili ya Intaneti na Jamii. Ingawa kulitokea mjadala mkali (ambao unaweza kupatikana kwa kutafuta kwenye alama #ab09 kwenye Twita), hapa kuna dondoo kidogo: mshiriki wa Misri lastoadri [6] alishangaa [13]kwenye Twita ikiwa washiriki walikuwa wamefahamishwa kikamilifu kuhusu utafiti huo:
Nasser Weddady [14] aliona [15] mantinki muhimu iliyoletwa na Razan:
Mwisho, Muiraki Salam Pax [9] alikubaliana na Razan katika suala hilo, akisema [16]:
Salam Pax akikubaliana na mtoa mada kwa kuandika: