- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Lesotho, Fasihi, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Wasifu wa Wanablogu

Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele.

Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho.

Tunazipitia baadhi.

Poéfrika
ni blogu ya uandishi wa kibunifu wenye mahadhi ya Afrika. Blogu hiyo ina sehemu kwa ajili ya mashairi yanayoanndikwa na washairi kadhaa wa Kiafrika, mahojiano na washairi, waandishi vile vile na habari na taarifa juu ya washairi wa kimataifa na waandishi hali kadhalika.

Blogu hiyo pia ina zana nyingi kwa washairi wanaochipukia kwani ina orodha ya viungo vinavyoelekea kwenye majarida yanayochapisha ushairi, waandishi ambao wameonyeshwa kwenye blogu na viungo vingi vinavyovutia waandishi hii ikiwa ni pamoja na picha za sura zao.

Poéfrika inaendeshwa na Rethabile Masilo [1] mwananchi wa Lesotho ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa. Pia anaendesha Canapic Jar [2] na Basotho [3] ambazo vilevile zinajihusisha na sanaa za uandishi na zanaa za maonyesho.

Fikira Zangu [4] ni blogu ya Kikenya inayoendeshwa na Bonyo Boungha Anthony anayeishi Nairobi, Kenya. Kauli mbiu ya blogu yake ni

“Mawazo makali kama watu washughulikao, huja na kwenda hututembelea na kupotea, yakiacha mlango umefunguliwa kidogo.”

Hivi ndivyo anavyosema kuhusu yeye mwenyewe

….Mimi maneno yangu yalisahau, na kufikiri nilivyowahi kuandika; Ni mwombolezaji achekaye, Mawazo yavumayo na ala za maandishi, Mawazo yatembeayo na matembezi yafikiriyo….

Ningesema kwamba ni kipande cha utenzi pale pale.

Ushairi wake ni mfupi na wenye ujumbe mahsusi wenye mistari isiyozidi 10. Maudhui kutofautiana kuanzia mapenzi mpaka kwenye siasa na changamoto zake kama mshairi.
Kipande kutoka kwenye ushairi wake –Utaendelea kuwa wangu? [5]

Je utaendelea kuwa wangu asubuhi
Baada ya huba ya jioni kufifia
Baada ya raha za usiku uliopita
Zikiwa zote zimepeperushwa mbali

Je utaendelea kuwa wangu
Baada ya mabishano machungu na ugomvi
Baada ya kubadilishana maneno makali
Utakunjua mikono yako na kuniruhusu nirudi

Blogu ya Marten [6] ni ya picha peke yake inayoendeshwa na Marten Schoonman anayeishi Nairobi Kenya lakini ni mtu ambaye husafiri sana kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na ng’ambo.
Blogu hii ni kitabu chake cha kumbukumbu cha mtandaoni kilicho na mtindo wa picha kikionyesha matukio mengi yanayosisimua na picha zilizopigwa kwa ustadi mkubwa za watu na vitu.
Pia anaonyesha picha na baadhi na maeneo alipopigia picha ambayo yamemsisimua yeye.

Mwamba wa Afrika –Picha haki ya Marten Schoonman

Mwamba wa Afrika –Picha haki ya Marten Schoonman

Merlin [7] ni mwanafunzi wa Chuo aliyezaliwa mwaka 87. Anajieleza kwenye blogu yake iitwayo, iceboxmerlin [7].

nina furushi la kutenda ninayosema, wakati mwingine kusema ninayotenda, lakini mara zote mtu mkweli mwenye bashasha ambaye ungependa kuwa naye!”

unaweza kuona kutoka kwenye kichwa cha picha kwamba ni shabiki mkubwa wa mijongeo. Anaiita blogu yake “The Phanton Thought…..”
Tamko lake,

“Haya ni mawazo yangu juu ya ulimwengu, maisha na aono ya jinsi dunia inavyoendelea. Dalili za ufahamu unaojihusisha na namna za maisha, ni akili na baadae mwenye akili zisizo za kawaida anayeishi. Ni wazo lililopatikana kwa hewa nzito!

Blogu yake ina mashairi mengi na mapingiti ambamo kwayo hupitia mausala na maudhui mbalimbali.

Kipande cha utenzi wake, “Hewa ni nzito! [8]

Ambapo hewa ni nzito!
Nimekwenda mahali,
Kama ambavyo safari ingekuwa…
Na nikapata sharubati ya maembe tamu na nzito,
Kayamba akicheza kwa nyuma,
Kama lile kundi la watu wajiitao Kayamba Afrika
Kulikuwa na mtu hata hivyo,
Rasta aliyekuwa akitafuna huko Muguka
Jani la kijani na kitu fulani anachokiropoka
Kati ya kitu kuujaza mdomo wake.
Na kupuliza sigara,
Na hewa hapa bila kukosea ni nzito
Na hivyo ndivyo anavyosema kwa sauti nzito,
“Bwana mdogo!”
“tuandikie baadhi ya hiyo micharazo mnayoiita ushairi…”
“niko kwenye hali ya utayari kwa chochote”
Na hewa nzito ikanijia,
Kuweka hisia za kujua ndani yake!

Boyd Oyier [9] ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika chuo kikuu nchini Kenya. Kadhalika ni msanii waliyejifunza mwenyewe anayependa kufanya majaribio na kwa sasa anafanya kazi mkaa na rangi za chokaa.

Picha ya kuchora ya Malcom X iliyochorwa na Boyd Oyier

Picha ya kuchora ya Malcom X iliyochorwa na Boyd Oyier


Picha zake za watu wenye ushawishi ulimwengu zimefanywa kwa hisia ambazo mtu anaweza kuzigusa.

Blogu yake haina zaidi ya mwezi mmoja, aliianzisha baada ya kuhudhuria warsha ya kublogu na mitandao ya kijamii mjini Nairobi.

Kwa sasa anakusanya mkusanyiko wake wa kwanza ambao ameupa jina la “Siasa katika rangi Nyeusi na Nyeupe”

Hivi ndivyo anavyoeleza lengo la sanaa:

“Kazi kubwa ya sanaa inapaswa kuwa kuwaunganisha watu. Kila mmoja wetu anapenda sanaa kwa namna mmoja ama nyingine, lakini tunazimwa na “wasomi” walioamua kuifanya sanaa iwe ngumu kwa kutumia nembo kama ‘surreal’, ‘enzi mpya’ na ‘uleo’. Sanaa nzuri ni sanaa ile unayoipenda!”

Tunatarajia kuona mkusanyiko huo mtandaoni.

Tafsiri Hii [10] ni mwanablogu wa Kenya mshairi anayeendesha afropoem, blogu kuhusu Utenzi wa Mwanamke mweusi.

Hivi ndivyo anavyojieleza mwenyewe:

“Weusi; kuanzia kwenye msokoto wa unywele mpaka kwenye kidole cha mguu wangu…Uafrika; uko kwenye damu ukitiririka kwenye mishipa yangu, ala kwenye sauti yangu, mdundiko kwenye tembea yangu…Mpenzi wa maneno; yaliyoandikwa, yaliyochorwa, yaliyokwanguliwa….Upenzi wa nguvu ya maneno yaliyosemwa; yawe yameandikwa, kutamkwa, kufuchwa au kuonyeshwa wazi”.

Blogu yake ambayo ni ya kadri ya mwmaka mmoja inazungumzia masuala kama usafirishaji wa wanawake wa Kiafrika [11] kwa ajili ya ukahaba, mapenzi, utamaduni na usherehekeaji wa Wanaume wa Kiafrika kati ya dhima nyinginezo.

Blogu hizi ni uthibitisho kuwa kuna zaidi kwenye Afrika zaidi ya siasa kama ilivyoonyeshwa na wanablogu wengi wa Kiafrika. Tunaweza kuwa na uhakiaka wa kuona zaidi blogu kama hizo.

(Makala hii ilichapishwa kwanza Mwezi wa Sita 2009)