- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Video: Vijana duniani kote wajieleza kwa sekunde 60

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia ya Kati, Asia ya Kusini, Nchi za Caribiani, Ulaya Mashariki na Kati, Antigua na Barbuda, Bangladesh, Mongolia, Naija, Poland, Elimu, Filamu, Haki za Binadamu, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana

Nembo ya OneMinutesJr

Nembo ya OneMinutesJr


Mradi wa OneMinutesJr [1]unawapa vijana wa umri wa kati ya miaka 12 na 20 kutoka kona mbalimbali za dunia fursa ya kujieleza, kusema na kujifunza ujuzi wa kutengeneza kazi za sauti-na-kuoangalia ili kuwasiliana zaidi ya mipaka yao, lugha zao na umbali zaidi kwa kutumia video ya sekunde 60.

Mradi wa OneMinuteJr umetokana na jitihada za pamoja za Mfuko wa Utamaduni wa Ulaya [2], Mfuko wa One Minutes Jr [3] na Unicef [4], vile vile na mashirika mwenza mengineyo. Katika wavuti yao, unaweza kuperuzi video za dakika moja moja zenye thamani ya mwaka mmoja kutoka katika nchi mbalimbali, nyingine zikiwa zimetumwa na watu binafsi, na nyingine zimetokana na warsha [5] ambapo vijana wanafundishwa mbinu za kuandika, kupiga picha za video na kuhariri mawazo yao.

Video hizi fupi fupi zinaonyesha masuala, mawazo na ndoto za vijana wanaotokea asili tofauti tofauti, na kutupa kidirisha cha kuyachungulia maisha yao ya kila siku. Kwa mfano, kutoka Poland, Ludmila Kierczak [6] anatengeneza video na kueleza yeye ni nani. Ili kuiangalia video, tafadhali bofya kwenye picha hapa chini ili kwenda kwenye tovuti ya OneMinuteJr [6].

Huko Bangaladesh, Mobasshera Tarannum Adiba anaonyesha vifungu kadhaa kutoka Makubaliano ya Haki za Mtoto [7]. Katika video yake, iitwayo Nataka Uhuru [8], anagusia Kifungu cha 12: Watoto wana haki ya kusikilizwa maoni yao na sauti zao ziheshimiwe na Kifungu cha 16 ambacho kinasema kwamba kila mtoto ana haki ya faragha.

Kutoka Mongolia, Tuvdenjamts (Tuvden) Altankhyag anaonyesha [9]haki ambayo kila mtoto anayo kwa utamaduni wake mwenyewe:

Na katika video hii inayofuata, Simon Tonge kutoka Antigua na Barbuda, anatumia haki yake ya uhuru wa kujieleza katika video iitwayo Maungamo ya msichana aliyebalehe [10]:

Ibrahim Ide kutoka Niger anaonyesha haki ambayo watoto wanayo kwa familia inayowapenda na kuwalindia haki zao katika video ya Pamoja au Pasipo [11]:

Kwa video zaidi za dakika moja, unaweza kuangalia kwenye tovuti kuu kwa ajili ya mradi huo kwenye TheOneMinutesJr.org [1] au unaweza kutembelea Idhaa ya UNICEF One minutes Jr kwenye Youtube [12] ili kuona video nyingi zaidi zenye sekunde 60 zilizotengenezwa na vijana kwenye mada ya Haki za Watoto.