- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Rwanda: Video za Wanaojitolea

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Rwanda, Muziki, Mwitikio wa Kihisani, Safari, Sanaa na Utamaduni, Wakimbizi

Kusafiri na kutengeneza video za yale tunayokutana nayo ni njia ya kushirikiana na dunia. Kufuatia mfululizo wa video zilizopakiwa na mtumiaji kdarpa kwenye YouTube [1], zinazoonyesha kundi la wafanyakazi wa kujitolea na watu waliokutana nao wakati waliposafiri kwenda Rwanda na kufanya kazi na jamii za sehemu hiyo.

Katika moja ya video zilizotumwa hivi karibuni ni hii [2] inayoonyesha onyesho la mwisho la warsha ya uigizaji, timu ya wanafunzi kutoka Shule ya Bethel ya Utume wa mambo ya Ajabu wanayopewa wahanga wa mauaji ya kimbari:

Makundi ya watu wazima na vijana pia yalikuwa na warsha za muziki, hiki ni kipande chake:

Warsha ya dansi pia iliandaliwa, na hili ni onyesho la mwisho [3]:

Na washiriki wa warsha ya uandishi pia walicheza ili kusherehekea [4] kilele cha warsha yao: