- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Poland: Blogu Zataka Malipo

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Poland, Harakati za Mtandaoni, Teknolojia, Uchumi na Biashara

Wasomaji wa blogu zinayoongoza za lugha ya Kipolish ni lazima wameshangazwa kuona kivinjari skrini mpya ya ukaribisho kwenye moja ya tovuti zinazopendwa: Imetangaza kwamba, kuanzia Disemba 14, 2009, blogu hiyo haitapatikana bila ya malipo.

Utambulisho mpya umewapa wasomaji machaguo matatu:
1. 5 PLN + VAT kwa siku 7 (takriban EURO 1.25)
2. 9 PLN + VAT kwa mwezi mzima (takriban EURO 2.1)
3. Ondoka kwenye tovuti

Jambo hili, ambalo ni limewashangaza watumiaji wa Kipolish, linaweza kutatuliwa baada ya wasomaji kuamua na kuonyesha uamuzi wao kwa kutobonyeza chochote kati ya vifungo au machaguo hayo matatu. Skrini ya pili itajitokeza, na kuwashukuru wasomaji kwa… kuwa sehemu ya utafiti maalum, na kuahidi kutuma matokeo baada ya muda mfupi. Kuna uvumi kuwa kampuni ya Autentika [1] iko nyuma ya kisa hiki.

Hata hivyo watu wengi waliamua kuondoka kwenye tovuti kabla ya kubonyeza chochote, jambo ambalo limepelekea maoni hasi kwenye tovuti za blogu fupi fupi za Kipolish kama vile Blip.

Pamoja na kipengele cha kibiashara nyuma ya jambo hili, nim ara ya kwanza kwa taasisi moja kuweza kuwaunganisha kwa ajili ya kutenda wanablogu wengi muhimu na wenye kusomwa sana (tumewahesabu sita miongoni mwao).

Global Voices itafuatilia kisa cha tangazo hili la biashara la namna yake na kuchapisha matokeo ya utafiti mara yatakapotolewa.