- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msumbiji: Je, ni Lugha Ngapi Zinazungumzwa Nchini?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Lugha

Kuna lugha 20 zinazozungumzwa nchini Msumbiji, kwa mujibu wa tovuti ya serikali [1], zaidi ya lugha ya serikali ya Kireno. Carlos Serra [2] [pt] anajiuliza kama kuna lugha nyingine zaidi, kwa mujibu wa wataalamu wa lugha mashuhuri:”Kuna mtu aliniambia kuwa zipo kati ya 20 na 26; mwingine akaniambia zipo 17 zilizoandikwa na nyingine bado hazijaweza kuandikwa”.