Mchakato wa Amani Nepal Unayumba

Maandamano ya usiku ya ki-Mao. Picha na mtumiaji wa Flickr izahirsky. Imetumika chini ya haki miliki huru.

Maandamano ya usiku ya ki-Mao. Picha na mtumiaji wa Flickr izahirsky. Imetumika chini ya haki miliki huru.


Mchakato nyeti wa kuleta amani nchini Nepal unasitasita katikati ya mapambano yanayozidi kuongezeka kati ya watu wa kundi la ki-Mao na serikali. Wakiwa hawajafurahia uamuzi wa Rais Ram Baran Yadav wa kumrejesha madarakani Kiongozi wa jeshi aliyefukuzwa kazi Rookmangud Katwal (Katwali alifukuzwa kazi na serikali iliyoongozwa na kundi la ki-Mao), wapiganaji hao wa zamani wa upinzani walizindua maandamano makubwa nchini kote. Ombi lao kubwa ni “kusimikwa tena kwa mamlaka ya watu”, ambapo wanataka kupunguza mamlaka ya rais kwani rais si ofisa nayechaguliwa. Ndiyo kwanza wametangaza duru la tatu la vitendo vya kupinga, baada ya duru mbili za kwanza kushindwa kutoa matokeo yoyote.

Blogu ya lugha ya Kinepali Mynsasar ina maelezo mafupi ya programu za kupinga ambazo kundi la ki-Mao limepanga kuzizindua.

“राष्ट्रपतिको कदम सच्याउनु पर्ने माग गर्दै संसद र सडकमा आन्दोलन गरिरहेको माओवादीले आफ्नो अल्टिमेटम सकिएको भोलिपल्ट घोषणा गरेको कार्यक्रमले खुसी र चिन्ता दुवै ल्याएको छ। खुसी यस कारण कि माओवादीले सोमबार, मंगलबार र बुधबार तीन दिन संसद खोल्न दिने भएको छ। बजेट पास गर्नका लागि उसले चार महिनादेखि ठप्प संसद खोल्न दिएको बताएको हो। तर उसले देश भने बन्द गर्ने कार्यक्रम पनि ल्याएको छ। त्यो पनि एक दिन हो र, तीन तीन दिन। तीन दिन बन्द हुँदा पनि माग पूरा भएन भने अनिश्चितकालका लागि बन्द गर्ने रे। तीन दिन बन्दका लागि पुस ५, ६, ७ गतेका लागि दिन तोकिएको छ।”

Kundi la ki-Mao ambalo limekuwa likiandamana kwenye barabara na bungeni kumtaka rais asahihishe uamuzi wake limetangaza programu ambazo zimeleta ahueni na mkanganyiko. Ahueni kwa sababu kundi la ki-Mao litaruhusu bunge kufanya kazi siku za Jumatatu, Jumanne na Jumatano. Wanaruhusu bunge kufanya kazi ili kwamba majadiliano ya bajeti ya mwaka yaweze kufanyika. Lakini pia wametangaza migomo nchini kote. Migomo hiyo pia, si ya siku moja, bali ni kwa siku tatu nzima. Kama matakwa yao hayataweza kufikiwa baada ya siku tatu za maandamano, wataeingia kwenye mgomo usio na kikomo. Mgomo wa siku tatu utaanza kwenye poush 5 na kumalizika kwenye 7 (Disemba 20-22)

Umoja wa mataifa umeeleza wasiwasi wake, anaandika mwanablogu Mohan Nepali katika GroundReport, juu ya namna ambayo serikali na watu wa kundi la ki-Mao wanavyoonekana kudharau ahadi zilizowekwa wakati wa kusaini mkataba wa amani mwaka 2006.

“Ofisi ya balozi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) leo hii alizitaka nguvu za kisiasa nchini Nepal, zikijumuishwa zile zilizo serikalini, kuhakikisha kuwa haki za binadamu wote zinalindwa. Imewataka wote, Serikali ya Nepal na wapinzani wa ki-Mao kutofanya ghasia zozote kwani kufanya hivyo kunaweza kuharibu mchakato wa amani mabo umekuwa ukiendelea tangu mwaka 2006.

OHCHR imeelezea wasiwasi wake juu ya uwezekano wa ghasia katika jina la waandamanaji wa ki-Mao na vitendo vya serikali vitakavyofuatia”

Waziri Mkuu Madhav Kumar Nepal yuomo kwenye shinikizo kubwa la kutatua mgogoro na watu wa kundi la ki-Mao lakini mpaka sasa hajaweza kuwaridhisha hao wanamgambo wa zamani wa upinzani. Maila Baje katika Nepali Netbook anasema kuwa jaribio la hivi karibuni la Bw. Nepal la kuataka kumaliza kugota kwa mahusiano na watu wa kundi la ki-Mao limeshindwa kutengeneza mawimbi yoyote.

“Waziri Mkuu Madhav Kumar Nepal alionya siku ile kuwa baraza la wawakilishi linaweza kuvunjwa, lakini bunge ambalo ni kivuli cha chombo kilichochaguliwa haliwezi, alikuwa mwepesi kubainisha. Kama mpatanishi mkuu alitegemewa kujaribu kupita njia ya kati katika kugota huku kwa mahusiano ambako kunazidi kuongezeka kina, basi hakutuvunja moyo. Hasa kwa kuwa alimtupia mpira Rais Ram Baran Yadav.”

Krishna Hari Pushkar, amabye anafanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nepal, anaziweka baadhi ya lawama za mchakato wa amani unaoweweseka kwa “watendaji wa kigeni”:

“Inaonekana kuwa watendaji wa ndani na wa nje wanaonekana wazi jinsi wanavyopinga maadili ya mchakato wa amani na jinsi wanavyodunda mbali na ukingo wa mkataba wa amani. Hivyo, ni kwa jinsi gani mkataba wa amani wa Nepal utaenda sawa katika hali kama hiyo na kelekea hitmisho linalotarajiwa? Kwa masikitiko, ni jambo la kusikitisha kueleza kuwa hakuna mtendaji hata mmoja wa moja kwa moja au wa vinginevyo walio na dhati na waliojitoa kwa vitendo kuhakikisha mafanikio ya mchakato wa amani nchini Nepal. Kama hali hii itaendelea, haitashangaza pale vikosi vya ki-Mao vitakapoamua kurejea msituni au serikali itakapoweka chaguo maalum dhidi ya wapiganaji wa kikabila. Ni jambo la kusikitisha kuwa baadhi ya wanasiasa wenye maslahi wanasema kuwa mapambano mengine yanafanywa katika kutafuta amani, hata hivyo imethibitika kuwa ni uamzi wa kijinga kulazimisha “vunja amani ili kuleta amani”

Mpaka sasa maandamano ya upinzani yamekuwa ya amani, katika sehemu nyingjne yaliyojaa rangi na muziki. Hii ni video fupi ya moja ya maandamano hayo ya upinzani.

Na kwa kuwa sasa watu wa kundi la ki-Mao wameamua kuzindua duru la pili la maandamano na wanatishia kuingia kwenye mgomo kwa kipindi kisicho na ukomo kama madai yao hayatakidhiwa, inaonekana kuwa mchezo huu wa kuigiza utaendelea kwa muda.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.