- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Malawi: Wanablogu Wajadili Matetemeko ya Ardhi 30 Katika Wiki 3

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Malawi, Majanga, Mazingira, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia

Katika kile ambacho baadhi ya wataalamu wa miamba wamekieleza kama matukio ya nadra, Wilaya ya Kaskazini ya Karonga [1] nchini Malawi imeshuhudia jumla ya matetemeko ya ardhi 30 katika wiki tatu zilizopita ambayo yamesababisha vifo 5, zaidi ya watu 200 kujeruhiwa na zaidi ya watu 3,000 kupoteza makazi. Habari mpya zinasema kuwa tetemeko jingine liliikumba Karonga Jumapili tarehe 27 Disemba na mengine yanatarajiwa.

Tangu rais wa Malawi Bingu wa Mutharika aliposema rasmi kuwa Karonga ni sehemu ya janga la kitaifa, rai za kuwasaidia waliathirika zimekuwa zikimiminika ili kuwasaidia watu katika wilaya hii ya migodi ya madini ya uranium [2].

Wanablogu kadhalika wamekuwa wepesi katika kushirikiana maoni. Swali ambalo linaendelea katika fikra za Wamalawi wengi ni sababu za matetemeko hayo ya radhi. Katika makala ya kina iliyopewa kichwa cha Vipande Vinavyokosekana Katika Kitendawili cha Matetemeko ya Ardhi Huko Karonga [3], Muza Gondwe anajaribu kuliweka na kulijibu swali:

Tetemeko la kwanza lilitokea jioni ya Jumapili tarehe 6 serikali [4] na Msalaba Mwekundu wanatoa misaada kwa walioathirika na tetemeko la ardhi lakini sawa na hivyo serikali inapaswa kutoa majibu juu ya nini kilichotokea? Je watu wanaelewa nini kinachosababisha matetemeko ya ardhi: je wanadhani kuwa ni tendo la Mungu, adhamu ya mizimu yenye hasira, au ishara ya siku za mwisho?

Disemba, halafu tetemeko kubwa zaidi asubuhi ya siku iliyofuata, lililofuatiwa na mitetemo katika Wilaya ya Kaskazini ya Karonganchini Malawi. Ardhi ilikuwa inatetemeka hata kufikia Mzuzu, mbali kwa Kilometa 150 huku tetemeko kubwa zaidi ya yote lililokuwa na kipimo cha 5.9 katika kipimo cha Rikta. Wazazi wangu wanaoishi Rumphi katikati ya Mzuzu na Karonga, walikimbilia nje ya nyuma wakati wa kila tetemeko wakijiuliza kama hizi ndio siku za mwisho. Mitetemo kumi na miwili ilihisiwa katika tatu. Makazi na majengo yameharibiwa, na kifo kimoja ambapo mtoto alifariki baada ya ukuta kumuangukia.

Wakati Muza anajaribu kutoa mtazamo wa sayansi ya miamba, Ndagha [5] anaeleza kughafirika kwake na kutojihusisha kwa vyama vya kisiasa vya Malawi ambavyo anadai vingemiminika Karonga kama ungekuwa wakati wa kampeni.

Je vyama vya siasa havina fedha za kuwapa walioathirika au eneo hili si muafaka kwa kampeni? Nakumbuka kuwa mapema katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa 2009, wanasiasa walishindana kwa kugawa pesa kwa ‘walioathirika’ katika ajali ya moto kwenye soko la Nyirande kule Blantyre.

Unaweza kusajili kuwa hakuna aliyeripotiwa kufa au hata kujeruhiwa nab ado walioathirika walipata jumla ya Kwacha Milioni 5.linganisha hilo na Karonga ambapo ni Kwacha milioni 2.5 tu zilizotolewa na Dk. Bingu wa Mutharika!

Nyie vyama vya siasa, kuweni wawajibikaji na onyesheni kuwa mko vile ambavyo mnadai kuwa. Hapa ndipo majimbo yenu yanawahitajini sana.

Wakati huo huo Wizara ya Maliasili, Nishati na Mazingira imepinga uvumi kuwa matetemeko ya Ardhi huko karonga yamesababishwa na kazi za migodi huko Kayekereka ambayo ipo Kilomita 35 kutoka makao makuu ya wilaya. Wizara imesema kuwa mgodi wa uranium ni mgodi shimo lililo wazi na halina kazi za chini ya ardhi kwa hiyo hauna uhusiano na matetemeko ya ardhi.

Kabla tu ya matetemeko huko kaskazini ya Malawi, Malawi ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa nne kiuchumi katika maeneo ya mafuta, fedha za nje, umeme na maji. Changamoto hizi zimemfanya mwanablogu Austin Madinga kujiuliza ikiwa uongozi wa Malawi unajifunza chochote kutoka kwa na matukio haya [6]:

Tuna uhaba wa maji jijini Blantyre, upungufu wa umeme na mafuta nchi nzima na ukosefu wa jumla wa fedha za nje. Vikiachwa bila kuangaliwa hivi vitu vina uwezo wa kuwa na madhara ya kudhoofisha kukua kwa uchumi wetu. Wadau mbalimbali wameahidi kutatua au kupunguza shinikizo lililopo lakini lini? Swali ambalo ninaendelea kujiuliza ni kuwa je Wamalawi wataweza kutoka katika matukio haya wakiwa na werevu zaidi?

Kuhusu tatizo la mafuta, mwanahabari Richard Chirombo [7]alijaribu kuliweka tatizo katika muktadha wa kihistoria na kuonyesha kuwa shehena ya Malawi ilikwama huko Msumbiji kutokana na kupungua kwa matumizi ya bandari ya Beira.

Katika miaka kumi iliyopita Malawi imesajili kupungua sana kwa matumizi ya bandari ya Beira nchini Msumbiji, kwa mujibu wa takwimu za usafiri silizopatikana kutoka kwa mamlaka ya bandari hiyo. Taarifa kutoka kwa Cornelder de Mozambique, kampuni ambayo ilipata zabuni kutoka kwa serikali ya Msumbiji mwaka 1998 ya kuendesha bandari hiyo, zinaonyesha kupungua kwa kasi kubwa katika matumizi ya waagizaji na wasafirishaji kwenda nje wa Malawi kwenye bandari hiyo. Taarifa hiyo inasema, kwa mfano, kuwa, wakati usafirisahji wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje na zile zinazosafirishwa kwenda zilifikia tani za metriki milioni 570 katika mwaka 1998 – na ziliendelea kufikia kilele cha tani za metriki milioni 1,3 kufikia mwaka 2000- Malawi imeshindwa kufifikia rekodi yake ya kilele cha 2006.

Waagizaji wa mafuta na serikali za Msumbiji na Malawi wanalaumiana kuhusu tatizo la mafuta lililoikumba Malawi kwa zaidi ya wiki nne mfululizo katika mwezi Novemba na Disemba.