ndani ya miezi kuelekea uchaguzi wa Rais Hohn Evans Atta Mills, wa-Ghana wengi, pamoja na wale walio nje ya nchi, waliohofu kwamba ushindi wa chama cha New Democratic Congress (NDC) ungeweza kugeuka kuwa utawala mwingine wa mwanzilishi wa chama hicho na mtawala wa zamani wa kijeshi, Rais Jerry John Rawlings. Mpito ulikuwa mzuri, na uhusiano kati ya Marais Rawlings na Mills, ulionekana kuwa mzuri.
JJ Rawlings, blogu isiyo rasmi iliyotengenzwa kutoa dondoo za kazi na mawazo ya rais huyo wa zamani iliweka taarifa nzuri tarehe 18 Mei, 2009 kuhusu safari ya Rais Rawlings kwenda Afrika Kusini kwa niaba ya Rais Mills. Ilitaarifu:
Rais Mills alimshukuru Rais Rawlings kwa kuiwakilisha Ghana katika kuapishwa na alimuhakikishia kuwa kutakuwa na hatua za kufuatilia kuzitumia fursa za mahusiano ya faida kwa pande zote kati ya Ghana na Afrika Kusini.
Lakini hivi karibuni, hali mbaya ya hofu imekuwa ikiamka kati ya Rais Mills na wanachama wnegine wa chama cha NDC pamoja na Rais Rawlings.
Ato Kwamena Dadzie hivi karibuni aliandika kwenye makala yake, “Rais Aliyezingirwa?”:
Rais Mills amezingirwa (kana kwamba na nguvu pinzani). Hakuna mashaka kwenye hilo. Amekuwa shabaha rahisi mno kiasi kwamba watu wengi wanajipanga kumtungua. Kinacholeta hofu zaidi ni kwamba wacheza mchezo huo ni watu wa chama chake mwenyewe. Upinzani unaweza kuchukua likizo.
Juma lililopita tu, alikuwa kiongozi wa chamachenye viti vingi bungeni, Alban Bagbin. Alisema rais anayependa kujionyesha kuwa yeye ni kondoo mnyenyekevu, amejizungushia wasaidizi na maswahiba ambao wanaonyesha tabia za mbwa mwitu, fisi na simba. Watu hawa, kwa mujibu wa Bw. Bagbin, humtisha na kumsumbua yeyote anayejaribu kutoa ushauri wa maana kwa rais.
Siku kadhaa kabla ya maoni ya Bw. Bagbin, mtu aliyembadilisha aliyekuwa Prof. Mill kutoka mtoza kodi kuwa mwanasiasa, Jerry John Rawlings, na kundi la wenyeviti wa majimbo ya chama tawala walionyesha hasira zao kwa namna ambavyo rais amekuwa akifanya ndani ya ofisi hiyo.
Bw. Rawlings anaamini sana kwamba mwanafunzi wake amewaajiri ‘wanaharamu’ wasio na ujuzi wowote ambao wanatumia vibaya ukaribu wao na madaraka kukidhi maslahi yao.
Ingizo la blogu mapema mwaka huu kwenye Vibe Ghana liliripoti kuwa:
Kwesi Pratt, mchambuzi wa jamii na Mhariri Mtendaji wa jarida la The Insight, alimlaumu Rais msaafu Jerry John Rawlings kwa kuweka miiba kwenye uendeshaji mwanana wa utawala wa Rais John Evans Atta Mills.
Kwa mujibu wake, matamshi ya Jerry Rawlings kuhusu mtindo wa utawala wa rais aliyepo madarakani si tu kuwa yanatia aibu, lakini pia yanaitusi akili ya profesa wa sheria.
Maoni kwenye majibu ya posti hiyo na mtu aliyeitwa Prince, yanasema:
Nadhani rais wa zamani Rawlings atajifanyia vyema yeye mwenyewe na chama chake cha NDC kama ataonyesha tabia za kistaarabu – kwanza ni muda wa kuangaliwa wa miaka minne – uonekano wowote wa Atta Mills kama kibaraka na sio mtu anayejitegemea mwenyewe utatangaza kiama cha chama chake kwa ujumla na Rawlings hasa hasa.
Ghana Pundit hivi karibuni aliweka makala kuhusu majibu ya rais Rawlings kwa mjadala uliopo hivi sasa:
Itakuwa ni jambo la ajabu kuiruhusu NPP ambayo imekataliwa na Waghana kutuambia kile tunachopaswa kufanya. Kama wanachama wote wa NDC na wabunge wamejitokeza kuonyesha hisia zao hadharani, basi NPP ambayo imekataliwa haitakuwa na chochote cha kusema.
Makala hiyo hiyo ilijumuisha maoni ya Kofi Adams, msemaji wa rais msaafu:
Bw. Kofi Adams alisema Rawlings anaamini kuna haja ya watu ndani ya chama kuiwajibisha serikali na wateuliwa wake badala ya wapinzani wao kwenye chama cha New Patriotic Party (NPP).
Adams anaendelea kusema:
Ni jambo jema kwa chama. Itakuwa vibaya kwa NPP kutuambia nini cha kufanya baada ya kukataliwa na ikiwa watunga sheria wote wa chama na wengine wamefikia kutambua kumwacha rais Mills afahamu hisia za wanachama na Waghana, basi ni vyema kwetu.
Hii ni kwa sababu, kama tutawaruhusu NPP kuendelea kutuambia, itakuwa kama mhitimu wa chuo kikuu kusahihishwa na watoto wa darsa la sita.
Ato Kwamena Dadzie amepokea zaidi ya maoni 70 kwenye makala yake, “Rais amezingirwa?” Essuman-Cape Coast, mmoja wa waliojibu makala hiyo aliandika:
Waandishi wa habari wametuangusha, wakati NPP ilipounda nodi ya ajira kwenye ofisi yao ya mkoa wa Accra na kuitumia kuwaingiza wanajeshi wa nchi kavu kwenye ajira hakuna aliyeuliza maswali (fahamu kutoka kwa Kojo Asante –CDD). Nenda na angalia wadaiwa walioshindwa kulipa vyombo vya mikopo vya MASLOC na LEAP na itakushangaza kwamba wote ni wabeba kadi mashabiki wa chama cha NPP. Mashabiki wa NDC wanatambua mbinu zote za NPP na itakuwa ni sawa na kujimaliza kwa Mills kuwapuuza wale waliopigana kwa juhudi kwa ajili yake ili awe rais. Namna Mills anavyodhibiti nia za mashabiki wake na Waghana kwa ujumla ni utatuzi wa matatizo haya. Hata hivyo, naomba nitaje kwamba, baadhi ya vigogo wa NDC wanatabia za kitoto. Maneno ya ukosoaji kama ‘ ya wastani/kawaida’ Timu B na Wanaharamu Walafi yanatoka kwetu. Ninalipwa vizuri lakini sitamruhusu bosi wangu kunitukana kila siku. Je, kuna mtu yeyote anayeamini kuwa chini ya JJ, kila mwanjeshi wa nchi kavu wa NDC alikuwa vizuri, kwa hakika la hasha lakini hakuna aliyewachochea kuwa na hasira dhidi yake. Ninaweza kukubaliana kwamba Mills amekuwa mzito kwenye jambo moja tu, yaani, kutokuwatia nguvuni wauaji wa Molbila mapema Januari 2009 na hata mmoja wao akatoroka. Mills angefanikiwa na mzunguko huu wa ghasia unalovikuta vyama vinavyoshindwa uchaguzi lingekomeshwa.
Ato Kwamena alijibu kwa kusema:
Nchi hii si ya kikundi chochote cha wanajeshi –iwe wa aridhini ama ama wa kwenye magari ya kijeshi ya hemvee! Baada ya yale yote NPP waliyofanya (nani hakujua kuwa MSLOC na LEAP walikuwa kwa ajili ya maslahi ya wafuasi wa chama fulani?) wanjeshi wao wa nchi kavu walilalamika kwamba Kufuor hakuwatendea vya kutosha. Wanataka nini? Maridhiano ya dhahabu au maeneo yanye mafuta?