- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

China: Uvunjaji Nyumba kwa Kutumia Mabavu

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Haki za Binadamu, Maendeleo, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia

Visa viwili vya uvunjaji nyumba kwa mabavu vimeibua hisia za kutaka kulindwa zaidi kwa haki za raia na utatuzi wa migogoro nchini Uchina.

Mnamo saa tarehe 13 Novemba,uamuzi wa serikali ya mtaa ya Chengdu wa kutumia mabavu ili kuvunja jengo [1] moja binafsi ulisababisha kujiua kwa mmoja wa wamiliki aliyejulikana kwa jina la Tang Fuzhen, ambaye alijimiminia mafuta ya petroli na kujiwasha moto. Jengo hilo liko mahali ambako panatakiwa kwa ajili ya mradi wa serikali wa kuunganisha barabara mbili. Ulinganishaji wa kisa hicho na kingine kilichotokea mwaka jana cha mwanamke mmoja katika wilaya ya Minhang Shanghai aliyewatupia mafundi waliokuwa wakijiandaa kuvunja nyumba yake mabomu ya petroli aliyoyatengeneza, katika eneo ambapo kutakuwa kitovu cha usafirishaji kwa ajili ya eneo la Kibiashara la Shanghai 2010.

Eneo lilikokuweko jengo la Tang Fuzhen

Eneo lilikokuweko jengo la Tang Fuzhen

Visa kama hivi vinajulikana kama ‘nyumba za misumari’, yaani ikimaanisha wenye nyumba wanaogoma kuhama kutoka katika maeneo yanayotakiwa kuvunjwa, mara nyingi ni kutokana na kutokubaliana kwao na kiwango cha fidia kinachotolewa. Kisa kilicho maarufu zaidi kilikuwa kile cha nyumba ya misumari ya Chongqing [2] cha mwaka 2007, ambapo wanandoa fulani walifikia makubaliano na mwendelezaji baada ya miaka mitatu ya mvutano.

Katika makala [3] ya siku za karibuni kwenye blogu, mwanablogu anayejulikana sana, Wuyuesanren (五岳散人) alilinganisha utafutaji ufumbuzi uliofanyika kwa amani katika kisa cha Chongqing na visa vilivyokuwa na vurumai kubwa vya mwezi uliopita:

不知道是否还有人记得那位“最牛钉子户”,在那个事件当中,拆迁者与被拆迁者虽然在进行着某种程度上的博弈,但双方都还是在规则之内,有笑容而无真正的伤害。

Sina hakika kama kuna anayekumbuka ‘nyumba ya misumari’ iliyokuwa na mivutano mikali zaidi. Katika kisa kile, japokuwa mbomoaji na mbomolewaji walikuwa katika upinzani, bado pande zote mbili zilifuata sheria fulani. Hatima yake ilikuwa ni tabasamu na hakukuwa na madhara yanayoonekana sana.

但从最近的事例看来,双方的耐心都似乎被消磨了,对抗的手段与结果都越发的激烈。前段时间,某直辖市的一份内部讲话资料曝光,其中明确提到强拆是一种合适的手段,并且要“形成巨大的压力,造成兵临城下的态势”。

Lakini kwa kutazama visa vya hivi karibuni, yaelekea kwamba subira ya pande zote mbili ilikuwa imekaribia kwisha kabisa. Vyote viwili, upinzani na matokeo yake vilikuwa na vurumai kubwa. Muda uliopita, hotuba ya ndani kwa ndani ya afisa mmoja iliwekwa bayana. Afisa huyo alisema kwamba uvunjaji nyumba wa kutumia mabavu ndiyo njia sahihi, na hata alisisitiza kwamba njia hiyo haina budi ‘kuleta hali ya uvamizi na utumiaji nguvu mkubwa’ dhidi ya wagandamizwa.

这些事例证明,在很多社会领域当中,某些利益相关方的对抗已经到了必须展示暴力的程度。作为强势的一方,由于各种条件都具 备,越发的没有了协商解决的耐心与诚意,而另外一方在财产损害更大、权益被侵害更多的状态下,也出以更激烈的方式进行对抗,这种对抗从哀求式的上访,开始 转变成伤害自身以求传播效力的最大化。

Mifano hii inaonyesha kwamba migogoro kati ya pande zinazohusika imefikia kiwango ambapo utumiaji nguvu unakuwa ni lazima. Upande ule wenye nguvu, ukitumia mazingira yanayoupendelea, hauna subira na unyoofu wa kuingia kwenye majadiliano. Upande mwingine, ambao uko kwenye nafasi ya kupoteza, unalazimika kuishia kutumia njia zilizo na ukali zaidi ili kujitetea. Kwanza wataanza na kujaribu kutafuta haki, kisha wataingia katika hatua ya kujiumiza ili kuvuta hisia ya watu wengi zaidi.

Katika mahojiano [4] na International Herald Leader, ambalo ni gazeti rasmi la Uchina, alitoa maoni kwamba visa vya utumiaji mabavu katika uvunjaji nchini Uchina hupitia hatua tatu:

最初,对抗是单向压制,因为那时传播媒介是有限的;第二阶段是上访以寻求司法救济;第三阶段,伤害自身同时也伤害对方,有时集体对抗,更极端的是自焚造成社会伤害。

Mwanzoni, mtiririko wa kutaka jambo hilo lifanyike huwa ni wa kutoka upande mmoja, yaani kutoka kwa mkandamizaji kwenda kwa mgandamizwa. Katika hatua hii vyombo vya habari vinakuwa bado havijaanza kuhusishwa. Katika hatua ya pili, mkandamizwaji analazimika kutafuta utetezi zaidi na kwenda mahakamani. Katika hatua ya tatu, wakandamizwaji wataishia kujidhuru wenyewe pamoja na kuwadhuru wakandamizaji wao. Mara nyingine, kunaweza kuwepo na ukabilianaji unaojumuisha watu wengi au hata kujitoa mtu mwenyewe nafsi yake.

Mwanablogu mmoja, Yao Hongen (姚鸿恩), alizungumzia kisa cha nyumba ya misumari huko Marekani ili kulinganisha na visa vinavyotokea Uchina. Mnamo mwaka 2006, Edith Macefield [5] alikataa kupokea jumla ya dola za Marekani milioni moja ili auze nyumba yake kupisha ujenzi wa eneo la kibiashara katika mji wa Ballard huko Seattle. Baada ya kifo cha Macefield, ilikuja kujulikana kupitia wosia ulioachwa kwamba nyumba hiyo irithiwe na msimamizi mkuu wa mradi huo wa ujenzi, Barry Martin, kutokana na uhusiano mzuri na kujali alikomwonyesha yule bibi kizee wakati wa ujenzi.

Nyumba ya Edith Macefield

Nyumba ya Edith Macefield

Yao Hongen alisema:

老太没有请律师,没有写信到有关部门,没有上首都华盛顿讨个说法,更没有自己制造燃烧弹或以自焚抗议,只是对开发商说一个很简单的词“No”。

Bibi yule kikongwe wala hakuweka mwanasheria; hakutafuta utetezi popote; wala hakwenda jijini Washington ili kupiga kelele za upinzani; na wala haina hata haja ya kusema kwamba hakuwa na haja ya kutengeneza mabomu ya petroli ili kujilipua. Alichofanya ni kumwambia mwendelezaji ‘hapana’.

Miongoni mwa maoni ambayo makala hiyo ilipata ni pamoja na:

新浪网友 (2009-12-06 13:59:47): 中国的小老百姓都是弱势群体,政府想拆就拆,才不管你以后有没有房子住!我们这儿政府就打着灾后重建的旗号,要修建商业街。要强行收回土地,要我们搬走。我们的房子可都是有土地证和房产证的!

Raia wa Uchina ndiyo walio katika hali ya kuweza kudhurika. Dola inaweza kuvunja eneo wakati wowote wanaotaka, wala haitajali kama utakuwa au hutakuwa na mahali pa kuishi baadae! Serikali yetu ilitumia mabango ya matangazo yanayoashiria kuwepo kwa majanga ya baada ya kujenga ili kuchukua ardhi kwa nguvu. Wakati huo huo, sisi tuna hiyo ardhi pamoja na vyeti ya kumiliki mali hiyo!

新浪网友 (2009-12-06 16:31:24): 开玩笑,在中国政府就是最大,执政者就是最狠,逆我者杀!

Ni utani. Nchini Uchina, dola ndiyo lenye nguvu zaidi na lililo katili zaidi. Wale wote wanaoleta upinzani wanauwawa.

新浪网友 (2009-12-06 13:21:37): 估计我的有生之年在中国史看不到这样的事情的

Nadhani sitakaa nione matukio kama hayo yakitokea katika Uchina katika maisha yangu.