Canada Imesema Nini? Upotoshaji wa Habari Kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi

Serikali ya Canada inasemekana imetoa tamko la jazba leo, ikikanusha upotoshaji wa habari zinazodaiwa kufanywa nayo kwa mujibu wa Jarida la Wall Street likidai kwamba Canada imebadili sera yake na itakuwa ikikubaliana na malengo ya kupunguza hewa ya ukaa na kutengeneza mpango kwa ajili ya mfuko wa kukabiliana na tabianchi kwa nchi zinazoendelea.

Kwa hakika, inaonekana kana kwamba yote hayo uzushi, hii ikiwa ni pamoja na makala ya jarida la Wall Street (zingatia, anuani ya URL ni europe-wsj.com na mwandishi anaonekana kuwa si halisi). Kwa mujibu wa Jason Linkins kwenye jarida la Huffington Post tamko hilo la kukanusha lenyewe pia ni uongo. Likichanganya mambo zaidi, inaonekana kuna hata tamko la tatu bandia lililotumwa kutaka radhi kwa mchanganyiko huo, likiacha watu wakishangaa nini ni kweli na nini kisicho.

Waandaaji wa masihara haya ni jamaa wanaoitwa The Yes Men ambao wamepata hadhi ya uhalifu wa kidunia kwa kuyadhalilisha mashirika na serikali, mara nyingi kwa kutoa matamko ya uwongo kwa kutumia majina yao.

Tovuti hiyo ya upotoshaji inaitwa www.enviro-canada.ca inaeleza sera mpya zinazofikiriwa kuwa za Canada.

Tovuti ya upotoshaji ya Canada

Tovuti ya upotoshaji ya Canada

Kwa mujibu wa kanusho bandia, serikali ya Canada ilikuwa imechanganyikiwa kwamba habari za kubadili msimamo wake zilipokelewa vizuri na nchi zinazoendelea kwenye Mkutano wa Umoja wa mtaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi(COP15) mjini Copenhagen. Walitoa kiungo kwenda kwenye video ya tamko lisilonasubira lililotolewa na mbunge na mjumbe wa Kamati ya Tabianchi ya Uganda, Margaret Matembe (jina la kutunga) akiwa na afisa bandia wa Canada pembeni mwake. HABARI MPYA: Utambulisho wa ukweli wa mbunge huyu wa Uganda umefunuliwa kwenye video hii hapa.

Ingawa tovuti ambapo video imewekwa inaonekana kuwa rasmi, ina anuani tofauti ya URL(cop-15.org) tofauti na ile halisi ya Umoja wa Mataifa (cop15.dk). Yeyote aliye nyuma ya upotoshaji huu ameweza kwa kiasi kikubwa kucheza na hisia za kutokuamini walizonazo wanaharakati kuhusu kushindwa kwa viongozi wa dunia kuchukua hatua kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Upotoshaji wenye akili –mbunge bandia wa Uganda akitoa tamko la haraka haraka

Upotoshaji wenye akili –mbunge bandia wa Uganda akitoa tamko la haraka haraka

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.