- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Brazil: Wito wa Kugomea Gazeti Linaloongoza Nchini

Mada za Habari: Amerika Kusini, Brazil, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari

Mwishoni mwa mwezi Novemba, vuguvugu mbili tofauti za kupinga lakini zenye kuhusiana ziliibuka katika ulimwengu wa blogu na twita nchini Brazil. Vuguvugu moja iliwataka wanablogu wote kuunga mkono kampeni za watu kuondoa usajili wao kutoka kwenye gazeti kubwa zaidi nchini Brazili, Folha de São Paulo, pamoja na tovuti yake ijulikanayo kama UOL. Vuguvugu la pili lilikuwa katika muundo wa maandamano mbele ya makao makuu ya kampuni hiyohiyo inayochapisha gazeti hilo, safari hii vuguvugu liliandaliwa na “Vuguvugu la Wasio na Chombo cha Habari” na liliongozwa na blogu ya Cidadania [1] [pt] likipinga kile walichodai ni upindishaji na habari zinazoegemea upande mmoja unaofanywa na Kampuni hiyo ya Folha.

Vuguvugu zote mbili, lile la mgomo na lile la maandamano yalichochewa na madai ya hivi karibuni kwamba gazeti hilo limekuwa likijaribu kumchafua Rais Lula da Silva kupitia makala iliyoandikwa na César Benjamin, ambaye alikuwa mtu wa karibu na Rais huyo na ambaye sasa ni mwandishi wa makala wa gazeti hilo la Folha, ambapo anadai kwamba Lula alikiri kuwa mwaka 1994, Lula alijaribu kumlazimisha mfungwa mwenzake kufanya ngono [2] alipokuwa amefungwa kwa kosa la kisiasa katika miaka ya 80. pamoja na watu wanaodaiwa kuwepo katika mazungumzo hayo kukataa na hata wale waliofungwa pamoja na Lula wakati wa utawala wa kidikteta, ikiwa ni pamoja na mfungwa huyo anayedaiwa kutendewa hayo, mwandishi wa makala aliomba msamaha kwa kosa hilo na gazeti hilo lilitakiwa kuchapisha habari mpya ili kukanusha shutuma hizo siku chache baadae.

Pamoja na hayo, vuguvugu zote mbili ziliunganika kuwa upinzani mkubwa zaidi kuwahi kufanywa kupitia ulimwengu wa blogu dhidi ya kile wengi walichokiita “PIG”, kifupi cha Chama cha Unyang’anyi wa Madaraka kwa Kupitia Vyombo vya Habari, ambalo ni neno lililoundwa ili kuelezea vyombo vya habari vya Brazili vinavyochapisha habari zenye kuelemea upande mmoja ili kutetea maslahi ya kisiasa. Watumiaji wa Twita @Dolphindiluna [3] na @Aritana [4] walibuni beji ambazo mwanzoni zilipandishwa kwenye Arlesophia [5], blogu za Blog do Tsavkko [6] na Maria Frô [7], wakiwakaribisha wasomaji kuondoa usajili wao kutoka kwenye vyombo vya habari vya kampuni hiyo. Mabango hayo yamekuwa yakienea kwa kasi kubwa katika ulimwengu wa blogu hasa pale Folha lilipomtumia onyo mtalaamu mmoja wa mambo ya mtandaoni na mwanablogu Antonio Arles, likidai kwamba kumekuwa na matumizi yasiyofaa ya alama za biashara za kampuni hiyo:


Arles anaeleza [8] hali ya mambo kwa ufupi [pt] na kusema kwamba anaamini ametishiwa na gazeti lililo kubwa zaidi nchini Brazili:

CENSURADO
Acabo de ser notificado extrajudicialmente por escritório de advocacia representando a Folha para que retirasse os selos da campanha #CancelandoFOLHA #CancelandoUOL, sob pena de processo por suposto uso indevido das marcas. Sendo assim, retirei imediatamente os referidos selos.
No momento não poderei desenvolver um post explicando melhor o caso, mas deixo aqui meu protesto por mais este ato de censura contra blogs.

UDHIBITI KATIKA VYOMBO VYA HABARI

Ndiyo kwanza nimetaarifiwa nje ya mahakama na kampuni moja ya wanasheria inayowakilisha kampuni ya Folha [de São Paulo] kuachana na kampeni ya beji za #CancelandoFOLHA #CancelandoUOL (#unsubscribeFolha, #unsubscribeUOL) vinginevyo nitarajie kukabiliana na hatua za kisheria kwa shutuma za kutumia vibaya alama za biashara. Kwa hiyo, nimeamua kuondoa mara moja beji hizo.
Kwa sasa, siwezi kuandika makala kuelezea kesi hii zaidi,hapa ninapinga kitendo kingine hiki cha kudhibiti upashaji habari kupitia blogu.

Je, hii ilikuwa kweli kitendo cha udhibiti wa upashaji habari? Flávia Penido [9] [pt] anaeleza kwamba kwa kutumia alama za biashara zilizosajiliwa, wanablogu walitoa mwanya kwa wanasheria wa gazeti hilo kupinga kisheria kampeni hiyo. Anafafanua kidogo kuhusu Sheria Na. 9279/96:

CAPÍTULO III – DOS CRIMES CONTRA AS MARCAS
Art. 189 – Comete crime contra registro de marca quem:

I – reproduz, sem autorização do titular, no todo ou em parte, marca registrada, ou imita-a de modo que possa induzir confusão; ou
II – altera marca registrada de outrem já aposta em produto colocado no mercado.

Pena – detenção, de 3 (três) meses a 1 (um) ano, ou multa.

Não tem o que espernear, certo?

SURA YA III – JINAI DHIDI YA ALAMA ZA BIASHARA

Kifungu cha 189 – Kosa la jinai dhidi ya alama ya biashara hufanywa na wale ambao:

I – wanatengeneza bila kwanza kupata ruhusa ya mwenye nayo, iwe yote kamili au kipande tu, alama ya biashara au kitu kinachofanana nayo katika namna inayoweza kuleta mkanganyiko, au
II – wanabadili alama ya biashara ya mtu mwingine ya bidhaa ambayo tayari ipo sokoni.

Adhabu – kifungo cha kati ya miezi 3 (mitatu) mpaka mwaka 1 (mmoja) au faini.

Kwa hiyo hakuna sababu ya kununa, au siyo?

Flávia Penido [9][pt] anaendelea, huku akitaja:

No entanto, que fique claro a proibição da utilização da marca da Folha de São Paulo, não tem o condão de coibir a manifestação daqueles que pretendem boicotá-la – basta que se faça outro selo, sem usar o logo da FSP (atentando também para os crimes de injúria, calúnia, difamação – há que ser mais liso que um bagre, se é que me entendem, mas dá pra fazer, com relativa facilidade). […]

Minha questão aqui é fazer com que todos pensem nas formas de se exercer a livre opinião – e mais do que isso, fazer com que as pessoas deem o correto valor às coisas: o que é mais importante? Fazer o protesto ganhar corpo, crescer, ou ficar dando murro em ponta de faca? Sério que o logo da FSP é tão importante assim pra campanha decolar? Eu acho que não.

Hata hivyo, tukubaliane kwamba kuzuiwa kutumia alama ya biashara ya Folha de São Paulo's si jambo kubwa kiasi cha kuzuia watu kuacha kuligomea gazeti hilo – unachohitaji kufanya ni kutengeneza beji nyingine pasipo kuweka nembo ya Folha (vilevile, uangalie usije kufanya makosa kama vile ya kuchafua jina la mtu, kusengenya, kusemea mtu uwongo – huna budi kuwa mtengeneza beji mjanja, nadhani mnanielewa, lakini kwa unaweza kufanya hivyo kwa urahisi kwa kiasi fulani). […]

Ninachokisema hapa ni kutaka kila mmoja wetu afikirie njia ambazo kwazo tunaweza kuudhihirisha uhuru wa kujieleza – na zaidi ya hilo, kuwafanya watu wathamini mambo kwa njia zilizo sahihi: je, kuna kilicho muhimu kuliko jambo hilo? Ili kusaidia kuufanya mgomo huu ufanikiwe, ukue na kuendelea kupigilia msumari? Je, ni lazima kweli kuwa na nembo ya Folha ili kuendelea na kampeni yetu hii? Sidhani.

 Antônio Arles, katika picha iliyopigwa na Aritanã Dantas. Imetumika chini ya Leseni ya Creative Commons.

Antônio Arles, katika picha iliyopigwa na Aritanã Dantas. Imetumika chini ya Leseni ya Creative Commons.

Antônio Mello [10] [pt], ambaye ndiyo kwanza amefuta usajili wake kwenye tovuti ya ya kampuni inayochapisha gazeti hilo UOL ameanzisha kampeni mpya. Anajenga hoja kwamba ikiwa wengi katika ulimwengu wa blogu wakichapisha upya beji zilizopigwa marufuku, Folha haitaweza kumwarifu kila mwanablogu na jambo hilo litalazimisha gazeti hilo kuacha vitendo vyake:

As publico aqui, convocando-os para que façam o download delas para seus computadores e depois subam-nas para seus blogs ou redes sociais. Eles vão ter que notificar a blogosfera toda. Assim vão aprender que os tempos mudaram e não existe mais informação de mão única.

Nimezichapisha (beji hizo) hapa, na ninamwalika kila mmoja wenu kuzinakili kwenye kompyuta aenu ili mzitumie kwenye blogu na mitandao yenu ya kijamii. Itawalazimu watu wa gazeti hili kumpelekea kila mwanablogu onyo. Jambo hilo litawafanya wajifunze kwamba nyakati zimebadilika na kwamba habari sasa hazitiririki kuelekea upande mmoja tu.

Marco Aurélio Weissheimer [11] [pt] naye amejiunga na kampeni hii na amefuta usajili wake kwenye bidhaa za kampuni hiyo inayochapisha gazeti hilo:

A razão: uso indevido da inteligência do assinante.

Sababu: matumizi mabaya ya akili za mtu aliyejisajili.
Folha inachapisha nyaraka zisizo halisi. Ondoa usajili wako kwao!

"Folha inachapisha nyaraka zisizo halisi. Ondoa usajili wako kwao!"

Uamuzi wa Folha wa kumpa onyo Arles ulisababisha upinzani mkubwa, na muda mfupi tu tangia beji halisi zipigwe marufuku, nyingine zinazofanana nayo [12] nyingi tu zilikuwa zimekwishajitokeza katika tovuti. Rodrigo Vianna, anayetokea Escrevinhamentos [13] [pt], amechapisha bango, upande wa kushoto, ambalo lina rejeo la habari inayodhalilisha iliyochapishwa na Folha [14] mapema mwaka huu [15] dhidi ya mtu ambaye pengine anaweza kuwa mgombea urais, Dilma Roussef, kwa kutumia baruapepe boya kama chanzo chake kikuu cha habari. Mwanablogu huyu anasema kwamba kampeni siyo kwa ajili ya kuligomea Folha, bali kuacha kulisha mitazamo yake:

A “Folha” não gosta de “banner” na internet que peça cancelamento de assinaturas do jornal. O diário da família Frias tentou até intimidar um blogueiro que publicou esses “banners”.
Mas a “Folha” gosta de ficha falsa na primeira página. Ah, ficha falsa pode!!
Então, o povo da internet resolveu bolar um “banner” novo, aproveitando a ficha falsa.

“Folha” halipendi “mabango” kwenye Intaneti yanayowataka watu kufuta kujisajili kwenye gazeti hilo. Gazeti la kila siku la familia ya Frias limejaribu kumtishia maisha mwanablogu aliyechapisha mabango haya. Lakini “Folha” linapenda kuchapisha taarifa za uwongo [za polisi] kwenye ukurasa wake wa mbele. Kumbe, rekodi za uwongo zinaruhusiwa!
Kwa hiyo, watu wameamua kutengeneza bango lao la kwenye Intaneti wakitumia fursa ya rekodi isiyo halisi.

Wimbi hili la pili la mgomo wa mtandaoni limechangia kuwahamasisha watu kushiriki kwenye maandamano ya Jumamosi ya tarehe 5 Desemba, ambapo dazeni za watu walimiminika mitaani katika jiji la São Paulo na kukusanyika mbele ya makao makuu ya kampuni ya gazeti la Folha kupinga msimamo wa gazeti hilo. Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja [16] ambapo ulimwengu wa wanablogu umehamasisha watu kuandamana pale. Kwa kauli mbiu inayosema “Folha inabaka taaluma ya uandishi wa habari”, nakumbuka sababu nyingi za kuitisha maandamano kwenye blogu yangu [17]:

Foi Ditabranda, Ficha falsa da Dilma, defesa descarada do Golpe em Honduras, defesa do DemoTucanato de forma inveterada, defesa de Israel, acusações infundadas contra o governo no caso do Blecaute – que em nada lembra o apagão e racionamento de FHC -, oposição sistemática ao governo de forma burra, mentira e violenta, baseada na franca manipulação, e, agora, o golpe de misericórdia, o artigo absurdo e criminoso acusando Lula de ser estuprador ou, ao menos, de ter tentado sê-lo.

Kulikuwepo na makala ya maoni ya Ditabranda, [aliyekuwa mgombea urais] rekodi za uwongo za polisi za Dilma, utetezi wao usio na chembe ya aibu wa mapinduzi nchini Honduras, utetezi wao usio na akili wa kile kinachoitwa DemoTucanato [vyama vya siasa vya DEM na PSDB], utetezi wao wa Israeli, shutuma zao zisizo na msingi dhidi ya serikali kuhusu kukatika kwa umeme – hawakumbuki kukatika kwa umeme na mambo ya mgao wa umeme wakati wa Fernando Henrique Cardoso [rais aliyepita] – kupiga kwao vita serikali iliyopo kwa njia za kijinga, kidanganyifu na mara nyingine za kutumia mabavu, kwa kutumia upindishaji mambo uliyo wazi kabisa, na sasa mapinduzi kwa kuchafua sifa za mtu kupitia makala ya kishenzi na yenye kujaa jinai inayomshutumu Lula kwamba ni mbakaji, au walau kama mtu aliyejaribu kubaka.
Folha de São Paulo: Makao Makuu ya PIG - Chombo cha Habari cha Kupindua serikali. Picha na Aritanã Dantas. Imetumika chini ya leseni ya Creative Commons.

"Folha de São Paulo: Makao Makuu ya PIG – Chombo cha Habari cha Kupindua serikali". Picha na Aritanã Dantas. Imetumika chini ya leseni ya Creative Commons.

Mtayarishaji wa maandamano ya Jumamosi, Eduardo Guimarães [18] [pt], alieleza kuwa yalikuwa ya mafanikio, maana watu wengi sana walimiminika kutoka katika majimbo ya São Paulo, Santa Catarina, Rio, Minas Gerais:

Missão cumprida e alma lavada. Perdeu quem não veio. Foi uma festa democrática.

Kazi imetimia na roho yangu imeburudika vya kutosha. Wale ambao hawakujitokeza walikosa mengi. Ilikuwa ni sherehe ya kidemokrasia.


Kuumiza mifuko

Claudinei Vieira [19][pt] anajiuliza endapo kampeni hiyo italilazimisha gazeti hilo kubadili mtazamo wake, maana mgomo huo mpaka sasa unaonekana kwamba umekuwa na ufanisi mkubwa kiasi cha kulilazimisha gazeti la Folha kuuchukulia kwa uzito:

Isso significa, portanto, de imediato, duas coisas: que uma campanha pela internet realmente está incomodando a Folha, que resolveu revidar. Opa. E de tal modo que está atacando a toda blogosfera e, de quebra, ao direito de expressão. Outro Opa. […]

Eu só fico pensando se eles realmente acreditam que essa campanha depende mesmo e somente de duas únicas imagens…

Kwa hiyo, kwa haraka haraka, jambo hili lina maana mbili kubwa: kwamba kampeni ya Intaneti kweli inalihangaisha gazeti la Folha, ambalo limejaribu kujibu mapigo. Oooh! Na linajaribu kuushambulia ulimwengu mzima wa blogu na, kama hitimisho kwa kuushambulia uhuru wa kujieleza. Ooo! nyingine. […]

Najiuliza tu endapo wanaamini kwamba kampeni hii inategemea tu beji hizo mbili…

Baadhi ya wanablogu, kama vile Rodrigo Vianna [20] [pt], wanaamini kwamba kuliumiza gazeti hilo kimapato ni njia yenye ufanisi zaidi ya kulipunguzia hadhi kuliko kushiriki kwenye maandamano:

Acho que a melhor forma de atacar essa turma é no bolso. Conheço uma dúzia de pesoas que cancelaram assinatura do jornal nas últimas semanas. Deve haver muitas outras por aí. Então, sugiro uma manifestação sóbria, em loval público, para um ato coletivo de cancelamento de assinaturas. […]

Não é preciso “queimar jornal” (não gosto disso, lembra os rituais fascistas nos anos 30), nem gritar. Basta dizer: não darei mais meu dinheiro a você. Essa linguagem eles entendem.

Nafikiri njia bora zaidi ya kuwashambulia washenzi hawa ni kwenye mifuko yao. Nawafahamu baadhi ya watu walioamua kufuta usajili wao kutoka kwenye kampuni hiyo katika wiki za karibuni. Lazima kuna watu wengi wa aina hiyo katika sehemu mbalimbali. Kwa hiyo, napendekeza kuwe na maandamano yasiyo ya jazba katika maeneo ya umma kwa ajili ya kuweka nguvu ya pamoja katika kufuta usajili kutoka kwenye huduma za kampuni hiyo. […]

Hakuna sababu ya kuchoma moto magazeti (sipendi njia hii maana inanikumbusha kafara za kifashisti za miaka ya 30), au kupaza sauti. Sema tu: sitaendelea kuwapeni fedha zangu. Wanaelewa vizuri zaidi lugha hiyo.

Usisome wala kujisajili kutumia huduma za Falha de São Paulo. Falha ni uchezeaji wa neno Folha, maana yake kushindwa.

"Usisome wala kujisajili kutumia huduma za Falha de São Paulo". Falha ni uchezeaji wa neno Folha, maana yake "kushindwa".

Maurício Caleiro [21] [pt] pia anafuata msimamo huo wa fikra akikubali kwamba wanablogu waweke mkazo zaidi katika kampeni ya mgomo wa mtandaoni:

Deixar de comprar e deixar de comentar qualquer matéria da Folha: este me parece o melhor caminho para legar ao jornal a irrelevância que ele, por suas próprias ações, faz por merecer.

Acheni kununua na acheni kutoa maoni kuhusu chochote kwenye gazeti hilo: Hii ni njia bora zaidi ya kulitunukia gazeti hilo hali ya kujiona halifai, kwa kutumia vitendo vyake lenyewe, ambavyo linavistahili.

Maria Frô [22][pt] anafikiri kwamba ile kuondoa tu usajili kutoka katika kampuni hiyo ya chombo cha habari haitoshi. Amechapisha orodha ya makampuni yanayotangaza bidhaa zao kupitia gazeti hilo na hivyo kuwaalika wasomaji kugomea bidhaa zao pia:

Além de cancelar assinaturas da FOLHA/UOL, proponho que boicotemos empresas e produtos que anunciem neste grupo empresarial. Quem deseja ter sua marca assinada a um jornal que pratica anti-jornalismo não merece que os cidadãos de bem prossigam consumindo seus serviços/produtos.

Zaidi ya kuondoa usajili wetu kutoka kwenye bidhaa za FOLHA/UOL, napendekeza kwamba tuzigomee bidhaa za makampuni yanayotangaza bidhaa zao kwenye kampuni hii. Wale wanaotaka alama zao za biashara ziendane na ile ya gazeti hili ambalo linafanya vitendo vya kuua fani ya uandishi wa habari hawawastahili raia wanaoishi kwa kufuata sheria za nchi kuendelea kutumia huduma na bidhaa zao.
Folha liliunga mkono udikteta. Ondoa usajili wako kutoka kwao!

"Folha liliunga mkono udikteta. Ondoa usajili wako kutoka kwao!"

Lauro Mesquita, kutoka kwenye blogu ya Guaciara [23][pt], anasema yaelekea kampuni hiyo imeanza kiandama njia ya kufilisika kwake:

Assinatura do Uol e da Folha não rolam mais aqui e não é só pela ameaça ao blogueiro. Se um jornal é burro assim pra tratar com a discordância, imagina o tanto que é pior a sua opinião sobre as coisas do mundo. […]

Do jeito que tá, até 2015, o grupo empresarial chega a meta da tiragem zero e seus proprietários vão gerir dois fanzines e 50% de um blog. Eu não vou sentir nenhuma saudade.

Hatujisajili kwenye UOL au Folha na hii si kwa sababu tu ya kitisho kilichotolewa dhidi ya mwanablogu [Arles]. Kama gazeti linashughulikia kutokukubaliana katika namna iliyo ya kipumbavu kama hiyo, hebu fikiria watakuwa na mtizamo gani wa vitu vingine duniani. […]

Jinsi mambo yanavyokwenda, mpaka kufika mwaka 2015, kampuni hili la vyombo vya habari litakuwa limefikia lengo lake la kujiondoa lenyewe katika uwanja wa uchapishaji habari na wamiliki wake watamudu tu kuwa na vijigazeti vya ucheshi viwili na nusu blogu. Wala sitajali kutoona bidhaa zao tena.